Wandugu hili Dubwana LA IPTL ndio wakati wa kulitumbua sasa

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,104
6,822
Wandugu kuna ile kampuni iliyoingia mkataba na Tanesco,linataka kurenew mkataba wa kinyonyaji tena na tanesco na kipindi cha nyuma kamati ya bunge wallitoa tamko kwamba hawana Sifa,sasa Ewura wanakusanya maoni eti tuliruhusu liendelee au lisiendelee ,Wandugu hili likampuni halistahili hata kulitolea maoni
 
Ii nchi we achaneni nayo tutafute sehem nyingine,..yaan kuna watu wanafanya ii inchi sijui Kama kitu gani,wana roho mbaya kweli kweli
 
Wandugu kuna ile kampuni iliyoingia mkataba na Tanesco,linataka kurenew mkataba wa kinyonyaji tena na tanesco na kipindi cha nyuma kamati ya bunge wallitoa tamko kwamba hawana Sifa,sasa Ewura wanakusanya maoni eti tuliruhusu liendelee au lisiendelee ,Wandugu hili likampuni halistahili hata kulitolea maoni
Usiwe kama LHRC wakurupukaji tu.
Kisheria EWURA ni lazima ikusanye maoni kwanza,kwa hiyo kama una sababu peleka tu EWURA
 
Watoe utaratibu Wa kutoa maoni maana imekuwa no kilio cha muda mrefu hivyo wakati umefika hilo li IPTL kuondoka.
 
Pia katika kuongeza muda Wa leseni huwa kunakuwa na masharti ya leseni na tunaamini IPTL ilikiuka masharti ya leseni Mara nyingi na ndio maana kulikuwa na malalamiko juu yao hivyo kiuzalendo tunategemea pamoja na kukusanya maoni Wasipewe leseni tena ili tusiendele kulalamika.
 
Wandugu kuna ile kampuni iliyoingia mkataba na Tanesco,linataka kurenew mkataba wa kinyonyaji tena na tanesco na kipindi cha nyuma kamati ya bunge wallitoa tamko kwamba hawana Sifa,sasa Ewura wanakusanya maoni eti tuliruhusu liendelee au lisiendelee ,Wandugu hili likampuni halistahili hata kulitolea maoni
Nimewasikiliza EWURA wao wanasema wana renew generation licence lakini suala la mkataba hawana uwezo na hawajawahi kuona huo mkataba unafananaje.
Kwa lugha nyingine mkataba wao ni sealed and confidential
 
Back
Top Bottom