Wanazuoni UDSM waionya serikali kuhusu DOWANS, wasema "Tanzania is a failed state"

Hawa wanafunzi kama wanaona wana haki ya kufanya siasa vyuoni kwanini wao wasifungue kesi ya Kikatiba kudai haki yao ya msingi na badala yake wanaiomba serikali iwaruhusu kana kwamba wanaishi chini ya utawala wa kifalme?
Mwanakijiji:Nadhani we si mgeni na hii serikali,unaweza ukafungua kesi ata 90 na usishinde ata moja so kwa wanafunzi kukimbilia mahakamani ni Wastage of time.
Muhimu kupita yote kwa wana JF wote ni kwamba tunapenda sana kuonyeshana umaridadi wa kuandika maneno humu na kujifanya tuna data za kila kona but UTENDAJI zero!! We need ACTIONS now sio porojo. Itafika kipindi hizi nyimbo za Dowans,Tanesco,EPA,KATIBA mpya,maisha magumu,uonevu wa walalahoi,mauaji ya innocent people etc etc zitazoeleka na watu kuona kama udaku tu. Wengi wetu tunakereka kusikia hizi habari bila kuchukuliwa hatua nzito kwa uoga wa wengi au kutafuta sifa humu JF then basi.
Ushauri wangu,Hatua kali zichukuliwe kuikomboa nchi na si kumwachia RA na EL wake watuweka pabaya kila kukicha
Enough is enough! Viongozi wa kisiasa au yeyote anayekubalika kny jamii tamko lake we need muongozo na sio mambo ya kilelemama kwani tunaumia sana na hali ya sasa kama sio wasomi bwna.
KINACHOKERA:Wengi wetu ni wepesi wa kusahau matukio na linapotokea jipya tunakimbilia kulalamika humu JF kama watoto vile. Mfano wapi issue ya EPA,KIWIRA,LOLIENDO,mauaji ya kina zombe,chemicals za mgodini Mara,uwizi wa kura,etc na sasa Dowans.
Hitimisho:Tuache kuwaza sana mambo madogo ambavyo vinamzuia mtu kuwa mjasiri wa kuchukua maamuzi. Tusipotake action kali within this month JF itakuwa sawa na blog ya udaku ktk kila nyanja na sio GreatThinkers km ilivyo.
Tuache porojo we need ACTION ACTION x10. Inakera porojo kila siku. Bora tukae kimya kama hatuwezi lkn hamna mtu wa kukusikiliza kilio chako kwa watawala wote lao moja.
Nawakilisha
 
hakuna haja ya wanafunzi kufungua kesi kuomba ruhusa kufanya siasa shuleni kwani haijaandikwa popote kuwa hairuhusiwi. haya ni maneno ya kilevi ya kikwete.

watawala wanaogopa kwa kuwa wanajua kuwa wananchi wameamua kuchukua nchi yao waliyoporwa. wanaogopa zaidi kuona kuwa wasomi wameshindwa kuendelea kunyamaza na wameamua kuacha unafiki!:msela:

tunashukuru kwa post nzuri.
 
Asante kwa mada nzuri. Yote yaliyozungumzwa yanajulikana kwa mapana yake kwenye jamii ya wasomi Tanzania. Bila shaka wengi wetu wanajua kuwa hata uongozi wa kitaifa ni kama umebakia tu kwa jina, kwani maamuzi mengi anayotekeleza Rais inaonekana kama ni ya Azizi na sio matakwa ya wananchi. Wamepiga filimbi wengi, akiwepo hata Sitta kumtaka Rais awe mkali kidogo, ikiwa ni maana ya kumwambia kuwa kama vile kiti alichokalia kinampwaya kwa kuwa anatekeleza majukumu ya kuagizwa na Azizi.

Kilichonifurahisha ni hitimisho kuwa "Nguvu ya Umma" ndio suluhisho pekee. Naamini hili likitumika linaweza kuibadili nchi hii na sio kutegemea vyombo vya sheria na usalama ambavyo navyo "by implication" vitakuwa vinatekeleza maagizo ya Azizi.
 
Back
Top Bottom