Wanazuoni UDSM waionya serikali kuhusu DOWANS, wasema "Tanzania is a failed state" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanazuoni UDSM waionya serikali kuhusu DOWANS, wasema "Tanzania is a failed state"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mponjoli, Feb 2, 2011.

 1. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Wanazuoni wa chuo kikuu cha dar es salaam leo mchana walikuwa na panel discussion kuhusu DOWANS na masuala mengine mtambuka yanayolikumba taifa letu, iliyoandaliwa na UDASA. Baadhi ya mambo yaliyozungumzwa ni pamoja na yafuatayo

  1. Scandals kama DOWANS, EPA, TICTS na nyinginezo ni symptoms za failed state
  2. Dowans=Richmond=Rostam Aziz. ROstam ndiye aliyemtuma mtu Marekani kwenda kujadili kuhuisha mkataba wa kuzalisha umeme kutoka richmond kwenda dowans. Rostam Aziz aliweka pressure kubwa sana kwa wanasiasa wetu (akina Lowassa) kuwa mkataba wa Richmond usainiwe. Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO ilifikia mahali alitishiwa maisha yake kama hatasaini mkataba wa Richmond
  3. Serikali ikiilipa Dowans itawaudhi sana Watanzania na serikali iwe tayari kwa action zitakazochukuliwa na wananchi
  4. DOWANS ni zao la bad politics inayotumia wanasheria maslahi kulihujumu taifa la Tanzania. Madhara ya kuilipa DOWANS kwa uchumi ni makubwa sana.
  5. Wanasheria wa TANESCO walishindwa kuibua "plead of bribery and corruption" kwenye mchakato wa zabuni ambayo tayari iliibuliwa na kamati ya bunge ambayo kwa maelezo ya wanasheria ingekuwa ni hoja nzito kuliko hoja zote walizotoa.Wanazuoni wanahoji Rex Attorneys na wanasheria wengine wa TANESCO wanadhani wanastahili malipo ya $2.4 million (karibu 3.6 billion) kama legal fees kwa kazi waliyoifanya? Maana mambo ya msingi sana waliignore.

  6. Imependekezwa mass action (nguvu ya umma) kama solution kwa matatizo ya kushindwa kwa taifa. Hili lilipata upingamizi sana mwanzoni baada ya Tundu Lissu kulipendekeza. Lakini baada ya mjadala mrefu uliokuwa huru wanazuoni walikubaliana kuwa mass action ndiyo njia pekee ya kuirudisha nchi kwenye mstari mnyoofu. Wanasema kinachohitajika ni "developmental state" na muelekeo tulionao kila mradi unafail sababu state system imefail. Wametoa mifano kama kushindwa kwa miradi mingi ya maendeleo kama elimu, afya, maji, kilimo na kadhalika kama viashiria kuwa state system imeshindwa na inatakiwa kuwa overhauled na kutengeneza institutions mpya kabisa zenye nguvu.

  Mfano: Iweje mtu mmoja kama Rostam Aziz awe na nguvu kuliko institutions kama TANESCO, BUNGE, PPRA, na kadhalika kiasi kwamba hata sheria zitapindishwa au kubadilishwa ili biashara zake zifanikiwe? inaonyesha kwenye nchi hii kuna watu wana nguvu kuliko hata Rais wa nchi, hivyo mamlaka ya urais kama institution uanatakiwa kuwa overhauled.

  Mwenyekiti wa UDASA, Prof Kibogoya ametoa hitimisho kama ifuatavyo:

  Ameulizawanasheria, kuna namna yoyote kuipeleka serikali mahakamani? Wakamjibu inawezekana lakini serikali itafurahi sana, kwani serikali watafanya hujuma kuichelewesha hiyo kesi hata kwa miaka zaidi ya 10.

  Hivyo Prof akatoa tamko kuwa njia pekee ni mass action.

  Pili amezungumzia malalamiko na maneno kuwa UDSM ni sehemu ya upinzani. Akasema UDASA chini ya uongozi wake itasimamia ukweli. Kama kuusimamia ukweli ni upinzani basi atashangilia sana kuitwa mpinzani.

  Tatu amekosoa siasa za ubaguzi kwamba vyuoni hakutakiwi siasa wakati hao wanaokataza wanafanya siasa vyuoni. Amesema wanafunzi waruhusiwe wafanye siasa vyuoni kwani duniani kote mageuzi makubwa yalianzia vyuoni. Hata wao CCM (TANU hapo kabla) walikuwa na tawi hapa UDSM kwenye jengo ambalo kwa sasa linatumiwa na NBC Mlimani branch. CCM wanaogopa siasa vyuoni kwakuwa wanajua vyuo ni kiini cha mabadiliko.

  My Take:

  Mjadal ulikuwa mzuri sana na huru. Maoni yalikuwa yanaheshimiwa na kulikuwa na uvumilivu sana wa kisomi. Ila inaonyesha kuwa Watanzania wamepoteza matumaini ya maendeleo. Kipindi cha mwalimu, watu walikuwa wanaishi maisha magumu lakini wakiangalia mwalimu alivyokuwa akilihangaikia taifa hili walikuwa wana matumaini kuwa "one day yes". Lakini kinachoonekana sasa watu wanasubiria "time bomb". Kila mtu ukimsikiliza kwa umakini anazungumzia Tanzania ijayo kama hatua hazitachukuliwa tunaweza kuingia katika machafuko ya kisiasa. Mwenye masikio na asikie maneno haya.
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  lazima niisome tena baada ya supper.... taarifa imekwenda shule kubwa hii
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hongera sana na tunashukuru sana kwa taarifa mzee bora wasomi wamekaa chini na kuliona kua ni tatizo hilo sasa kilichobaki ni utekelezaji kama serikali ni sikivu itabadilika tu ila kama ni sikio la kufa basi wataona kama ni upuuzi natizo lingine sisi ni wepesi sana wa kusahau kwa mfano mambo ya EPPA watu walishasahau,richmond japo inazungumziwa sio kama kipindi kile na mauaji ya arusha naona kuna dalili tayari za kusahau sijui tuna tatizo gani kwamba vitu vingi huwa tunavichukulia umuhimu kwa muda mfupi sana then tunasahau kama havikuwepo vile!!!
   
 4. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Safi sana!
   
 5. Mtembea_peku

  Mtembea_peku Senior Member

  #5
  Feb 2, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  safi munoo......dats wat we need....kila jiwe litageuzwa this tym around....
   
 6. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kikwete hawezi kusikia haya.. baada ya kupachikwa kwenye kamati ya usuluhushi wa Ivory coast, ndiyo amepata mlango wa kutokea kukwepa shinikizo linalomkabili hapa ndani..tutaanza kushangaa kusikia safari za ajabu zisizo na kichwa wala miguu.
   
 7. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hii taarifa imenigusa sana, na umei-present kwa kina, ahsante sana!

  hii inazidi kutupa ukweli na picha ya jinsi taifa letu linavyokaa ktk ukingo wa mwisho ktk madhara yanayoletwa viongozi mafisadi, waliooza kiuongozi kifikra na kiuongozi, wakitawaliwa na tamaa na nguvu ya mafia na fisadi mkuu RA.

  Nchi inatakiwa ukombozi. hii ni lazima na sio ombi.
  wanazuoni wametoa dira kitaifa, vyama na taasisi za kiraia vijiandae kuikomboa nchi.
   
 8. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2011
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Safi saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana. Nafikiri sasa RA huko aliko anatakiwa kujua kuwa watanzania walio wengi walishatambua ya kuwa shida na matatizo mengi tuliyo nayo yeye ni chanzo kikubwa. Akae atafakari na abadili njia zake za kuifilisi hii nchi yetu vinginevyo watanzania watainuka juu yake na ataihama hii nchi. Kwa kweli haiingii akilini mtu mmoja na kikundi chake wana mapesa yasiyohesabika huku waTZ wakiishi maisha ya shida. Huduma za jamii mbovu zikiwemo afya, maji, umeme, elimu n.k kisa pesa za walipa kodi wa TZ zinaishia mifukoni mwa RA na kundi lake. Kwa kweli hili halikubaliki.
   
 9. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mungu akubariki kwa thread iliyokwenda shule. Angalau sasa wasomi wetu wameanza kutimiza jukumu lao muhimu la kutathmini mambo ya nchi kisiasa, kijamii na kiuchumi. Kwa staili hiyo, wataisaidia sana nchi yetu.
   
 10. S

  Societa Jesuit JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapa hakuna kusubiri serikali ushauri ni mzuri ni mass action tu ....serikali ni rostam azizi sasa tumsubiri rostam azizi wanini? hivi yale maprocurement laws alivyoyapindisha huyo rostam mbona ni kichefuchefu mbaya zaidi analindwa na usalama wa taifa...hivi uchawi hapa bongo upo kweli kwanini wasimroge rostam azizi? ...wachawi wana waroga wezi wa kuku tu.....nina hasira hadi nataka niizabe kibao laptop yangu.
   
 11. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #11
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,573
  Likes Received: 3,873
  Trophy Points: 280
  hitimisho zuri, mpango mzuri, mwanzoni sikupenda Lissu awemo ili tupate ladha tofauti, lakini I was wrong ndie aliyependekeza mass action! this is great kama amesema Tindu lissue then wow! what can I say he is at right position to initiate this!!!

  tuingie mitaani!
   
 12. S

  Societa Jesuit JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wasomi hawa ni wale ambao ni new generation na ambao mgao wa umeme unawagusa ok mimi natoa big up kwao....ingawa naona pia walete tija kwa raia wa kawaida ambao kwetu sisi kurusha mawe kwa ffu hatuoni kazi ila ni kututia ujasiri tu....big up sana masomi yetu ya bongo
   
 13. KiJo

  KiJo Member

  #13
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  :clap2: .... The goverment has ignored the role of the literates in its decision making everything is politics, we need critical minds that can think beyond in making decisions that will build a better nation.. "the important thing is not to stop questioning"
   
 14. m

  mabogini Member

  #14
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wanajadili and then what actions do they take?STUPID
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  :msela:Nguvu kazi:msela:
   
 16. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #16
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Great post. Big up.

  Let us clearly what is mass action.....like in Cairo, Tunis..... If yes when and how do we start? it is becoming too late.
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Feb 3, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hawa wanafunzi kama wanaona wana haki ya kufanya siasa vyuoni kwanini wao wasifungue kesi ya Kikatiba kudai haki yao ya msingi na badala yake wanaiomba serikali iwaruhusu kana kwamba wanaishi chini ya utawala wa kifalme?
   
 18. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #18
  Feb 3, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145

  Mjadala mzuri.
   
 19. M

  Mindi JF-Expert Member

  #19
  Feb 3, 2011
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Angalia Scenario hii: wanafungua kesi ya kikatiba na serikali inafanya moja ya yafuatayo: mosi, inaichelewesha sana kesi. sasa wanafunzi ni title lakini watu wanabadilika kila intake, wanagraduate hawa wanaingia hawa. unaweza kuwa na wanafunzi active wanaondoka wanakuja vilaza. au kwa upande mwingine hata kama ni wanaharakati-material, lakini hawana depth katika kuchambua mambo, wanakuwa defeated technically. lakini wanaweza pia kuvutwa shati over time.

  Pili, serikali inaweza kuwa-defeat over technicalities, kama hawatakuwa wamejijenga vizuri na kupata support kubwa. na wakishadefeat, matter closed forever...

  kwa hiyo msingi wa mafanikio ya wanafunzi katika hili ni ku-mobilise support kutoka maeneo mbalimbali. huu ni mwelekeo wa kisiasa zaidi. ni kwa pressure ya aina hii nadhani wanaweza kuwa na mafanikio makubwa, na kwa kuegemea misingi ya haki za binadamu ya kikatiba katika free association and expression of opinion, wanaweza kufanya mengi. lakini hata hivyo hii hoja ya kutofanya siasa vyuoni is such a joke! CCM inafanya siasa sana vyuoni, hilo linajulikana. crying wolf ni kwa sababu mazingira ya vyuo ni mahali ambapo opposition inafanya vizuri zaidi. na wala sioni scenario ambapo utaondoa siasa vyuoni kabisa. ama zitakuwa overtly au covertly.
   
 20. M

  Mindi JF-Expert Member

  #20
  Feb 3, 2011
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Huko kujadili tu ni contribution kubwa sana. you must keep it running in the public domain. kuhamasisha, kuhabarisha, kuwapa watu hoja. hiki ni kisima cha fikra na msingi wa ujengaji hoja. uliona lile kongamano la katiba pale UDSM lilivyokuwa so informative? hata mtu ukijenga hoja unajua katiba ni kitu gani, na kwa nini tunataka katiba mpya! hata ukipandisha mzuka, unapandisha mzuka kwa misingi inayojulikana. huu ni mchango mkubwa sana. having a just and clear cause is a very necessary ingredient in a revolution
   
Loading...