Wanazuoni na Wanafunzi wa vyuo vikuu, Bodi ya Mikopo (HESLEB) haiwatendei haki. Amueni hatima yenu 2020 hii, mnaweza kuitosa CCM

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Kama navyosema siku zote mimi ni kada hai wa CCM na naendelea kukipenda CCM. Lakini nitafurahi sana chama changu kiadabishwe awamu moja au kichachafwe ili kipate adabu kisirudie makosa yale yale na kiache kudharau wanyonge wahali ya chini.

KWANINI NASEMA CHAMA CHANGU KIADABISHWE?
1. Serikali ya chama changu imeweka ubaguzi mkubwa sana kwenye utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, eti mtu anakopeshwa halafu anawekewa vigezo kibao. Unamwekeaje masharti kijana ambaye amesoma shule ya kulipia kama pesa ni ya mkopo na atarudisha?

Kijana wa miaka zaidi ya 33 ana kadiploma chake anataka apate mkopo huenda ada ya chuo ni ndefu imsaidie apandishe elimu yake wewe unamnyima mkopo eti ni umri?

Mbona wakati wa JK wanafunzi wote wenye sifa walipata mikopo bila kujali backgrounds zao wala umri ilimradi ni Watanzania tu?

*#Kama huwezi kutoa mkopo kwa watu wote wenye sifa unawaweka masharti magumu wasipate ujue wewe huna pesa ya kutosha na huwezi kuwapa wote. Wewe hufai kuendesha serikali.

2. Makato ya marejesho ya mikopo kutoka asilimia 8%-15%, hivi kwa mishahara yetu hii hii ya Tanzania kwa ngazi ya shahada hasa ualimu iwe private au sekta za umma, unampandishia mtu makato ili tu makusanyo yaongezeke ukidhi mahitaji yako wewe si uonevu huo? Kwani ukimkata 8% mtu huru katika taifa lake na alikopa pesa ya Umma unaumia nini?

Mtu unakata 15%, mshahara hujsmpandishia miaka 5 sasa, kodi kubwa, sasa unataka aishije?

Narudia tena, Chama changu kiadabiwe angalau awamu moja haya makosa hayatojirudia tena.

Nawatakia weekend njema.

CCM OYEEE!!!
 
Hii ni nafasi adhimu kabisa kuiondoa CCM na kuleta mabadiliko kupitia vyama vingine.
 
Hakuna mwanachuo atakaye mchagua Magufuli. Kampeni inayotumika kumponda Magufuli ni" Ewe mwanchuo ukimaliza chuo hupati ajira".
Kwasabb serikali hii
  1. Imeua sekta binafsi.
  2. Imeua biashara.
  3. Imegoma kutoa ajira serikalini.
  4. Imeua masoko ya mazao ya kilimo .
Mwanachuo ukimaliza utafanya nn?
Kwa maneno haya wanachuo wote wanaichukia ccm na serikali yake.
 
Hakuna mwanachuo atakaye mchagua Magufuli. Kampeni inayotumika kumponda Magufuli ni" Ewe mwanchuo ukimaliza chuo hupati ajira".
Kwasabb serikali hii
  1. Imeua sekta binafsi.
  2. Imeua biashara...
Watu wenye jinsia mbili akili zenu zilisha ondoka na upepe wa magharibi...
 
Serikali kupitia bodi ya Mikopo, huu ndio wakati wakuvuna mlichopanda ndani ya miaka mitano.
 
Hakika wanatetemeka sana . Mana huku mtaani tupo wanyonge wengi sana ambao hatuta wachagua mwaka huu.
 
Kama navyosema siku zote mimi ni kada hai wa CCM na naendelea kukipenda CCM. Lakini nitafurahi sana chama changu kiadabishwe awamu moja au kichachafwe ili kipate adabu kisirudie makosa yale yale na kiache kudharau wanyonge wahali ya chini.

KWANINI NASEMA CHAMA CHANGU KIADABISHWE?
1. Serikali ya chama changu imeweka ubaguzi mkubwa sana kwenye utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, eti mtu anakopeshwa halafu anawekewa vigezo kibao. Unamwekeaje masharti kijana ambaye amesoma shule ya kulipia kama pesa ni ya mkopo na atarudisha?...
Tusiangalie itikadi zetu, tujiunge kwa pamoja kumsaidia kamanda Lissu tumpe Nchi ipige spana . Tupate nchi yenye mifumo mizuri ya sheria hata ikitokea wewe unakua Rais utaweza kutuongoza bila shida .
 
Hakuna mwanachuo atakaye mchagua Magufuli. Kampeni inayotumika kumponda Magufuli ni" Ewe mwanchuo ukimaliza chuo hupati ajira".
Kwasabb serikali hii
  1. Imeua sekta binafsi.
  2. Imeua biashara.
  3. Imegoma kutoa ajira serikalini...
Kwab uzoefu wangu, sijuai ni kwa kutojua kwao au kwa ujinga wao auu kwa mkumbo wao tu, wanafunzi wengi wa vyuo huwa hawaipigii kura CCM. Na ndio sehemu pekee wapinzani hasa Chadema inapotegemea kupata kura. Bahati mbaya nchi nzima hawafiki laki tano. Sisi tulioko mtaani TUNATOSHA!


TUKUTANE OKTOBA 28!
 
Bodi ya mikopo ni chombo kinachowanyonya WATUMISHI WA UMMA nchini kwa kuweka riba ya 15% huu ni uuaji kabisa
 
Kama navyosema siku zote mimi ni kada hai wa CCM na naendelea kukipenda CCM. Lakini nitafurahi sana chama changu kiadabishwe awamu moja au kichachafwe ili kipate adabu kisirudie makosa yale yale na kiache kudharau wanyonge wahali ya chini...
Wakati JPM ana saka kura 2015 alisema ana shangaa vijana kunyimwa mikopo waksti watairudisha, akarnda mbali zaidi na kusema haoni sababu ya kubagua wanufaika wa mikopo kwa vile kazi zote zina tegemeana. Ameingia cha kwanza ni kuongeza asilimia ya marejesho.

Waoitishaji kwa mbwembwe ni wabunge wa Ccm wana tetea chama chao na sio wapiga kura wao.. Nitashangaa sana wanavyuo mkiipa Ccm kura. Za wazee na mafao shauri yenu, maana mneelimishwa hamsikii.

Acheni mfe na Ccm shingoni nafao yenu tuta kula sisi. Wakulima kaeni mdanganywe kama kawaida yenu muendelee kuwa maskini.. Ati ruhusa safirusha tani moja bure. Ikizidi lipa ushuru.. Mtakoma
 
Kama navyosema siku zote mimi ni kada hai wa CCM na naendelea kukipenda CCM. Lakini nitafurahi sana chama changu kiadabishwe awamu moja au kichachafwe ili kipate adabu kisirudie makosa yale yale na kiache kudharau wanyonge wahali ya chini...

Mbaya zaidi kwa sera ya mikopo iliyopo mwanafunzi analipa hata tuition fee pia.

Kwa maana nyingine elimu sasa hivi privatized. Vyuo vyote kimsingi ni binafsi.

Kama kuna uwezekano wowote ni bora kutochukua mikopo kabisa.
 
Back
Top Bottom