Wanayofanyiwa watuhumiwa wa ugaidi Segerea

Ukada wa ccm, cdm ama cuf unahusunini kwenye masuala yaufafanuzi wa jambo?
Bado watu tunamhemuko kutokana na maneno yako uliyotuvuruga humu kutokana na post zako zaudini bado tu unaendeleza ngebe zako si ndiyo?

Kada kajifundishe kuandika vizuri , Lumumba itakuuwa
 
Unao ushahidi walifanya ugaidi ??? Maana sasa ni zaidi ya miaka mitatu wako ndani na Polisi wanatafuta ushahidi , labda utawasaidia kupeleka mahakamani
Nahsi wewe ni mmoja wao au una undugu nao, kama sivyo basi yakikukuta utaelewa nn namaanisha.
 
Kwa maandiko ya barua hii inaonesha wew ni mchochezi wa kidini...inaonekana kilichokuweka ndan mpaka sas unaeneza udini, serikali ya Tanzania haina udini..acha chuki za kidini
 
Itazame upya imani yako,inakuwaje unatoa mia kwa mia kuwa jamaa ndo mkosaji,?

Muislam yupo peke yake humo ndani mbona hatujaona wengine wakilalamikiwa naamini tulifata sheria kwa askari wetu hawaweI kutusumbua
 
Hii barua nimeishia nusu, ila niseme hivi:
1.) Mahabusu wamejaa walalahoi tu, hii si haki.
2.) Barua hii alipaswa apewe JPM mwenyewe mkononi kutokana na uzito wake wa kipekee..
Ngoja niendelee kuisoma kwanza hii barua..
 
Eti Kanisa Katoriki lina kitengo cha kutetea haki, hivi unafikiri hilo kanisa la RC halimjui Shekh Farid na madhara ya movement yake ya uamsho dhidi ya welbeing ya ukristo ZNZ.?

Jibu la swali lako wanakupa Wamerekani ambao ni Wakiristo, baadhi yao wengi ni Wakatoliki, na wanajua Ukiristo, na wanaofuata Ukiristo unavyotakiwa kwa haki. Waliojitokeza kupinga dhuluma zinaendelea dhidi ya Waislam duniani pamoja na sera za kibaguzi wa kidini za Donald Trump. Tungekujibu kabla ya hapo usingeelewa. Nadhani umeshuhudia mwenyewe. Tunazijua itikadi zenye chuki zinapandikizwa kwenye dini, na haziko Kwa Waislam tuu bali hata dini nyingine. George Bush alivyokwenda kuivamia Iraq kinyume na matakwa ya Umoja wa Mataifa, alisema nini? Eti Mungu ndio kamtuma, wakati Makanisa ya Kilokole ndio yalibariki aibu hii ya vita ambayo vimeleta aibu katika historia ya binaadamu. Mwislamu mzuri ni yule anayemlinda Mkiristo, kama vile tulivyoona hapo jirani kwetu Rwanda wakati wa mauaji ya kimbali. Mkiristo mzuri ni yule anayemlinda Mwislam, kama vile Mfalme Mkiristo wa Ethiopia alivyowalinda Waislam enzi ya Mtume Muamadi. Huu ni ndio Ubinaadamu, ndio maua na bustani ya dini. Dini sio klabu ya mpira au chama, tusiwe na ugonjwa wakishabiki. Ubinaadamu Kwanza. Shukraan
 
SIJAISOMA HATA KUIMALIZA HII TAARIFA ILIYOKAA KICHOCHEZI,KICHWA CHA HABARI KINASE "WANAYOFANYIWA WAHALIFU WA UGAIDI GEREZA LA SEGEREA" HAPO HAPO UMEANDIKA "JE UNAFAHAMU JESHI LA MAGEREZA LINAVYOWATESA WAISLAMU SEGEREA?" WE JAMAA UNAONEKANA NI MCHOCHEZI MAANA HUJUI ULICHOANDIKA,JIFUNZE KUTOFAUTISHA KATI YA MUISLAMU NA GAIDI!!

Tabia ya kuwaita Waislam ni wachochezi wakati wanadai haki zao ni upuuzi, ujinga, ushenzi na hila za kuendeleza unyanyasaji na maonevu. Leo dunia nzima imesimama kuwatetea Waislam, Maonevu juu ya Waislamu yamezidi. Hakuna vita dhidi ya Ugaidi, hivi ni vita dhidi ya Waislamu na Uislam, ndani ya Pentagon yenyewe wamesema. Hawa Waislamu tuliowafunga bila ushahidi, ni kutokana na tabia za baadhi ya watu fulani na tabia za kujipendekeza kwa Wazungu (Vibaraka). Chuki itabadilishwa na mapenzi tuu. Tofauti gani ya hawa Waislam tuliowafunga hapa na wale waliozuiwa na Donald Trump kuingia Marekani? Aibu tupu. Tuogopeni Mungu. We condemn the people without evidence. This is a shame to our Nation. Tutafuteni amani kupitia haki sio maonevu.
 
Back
Top Bottom