Wanawake: zijue dalili za hisia za usaliti katika mahusiano……….

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
11.jpg

Inawezekana ukawa ni mke wa mtu au una mpenzi wako ambaye mna matarajio ya kufunga ndoa na kuishi pamoja. Kuna wakati unaweza kujaribiwa na kujikuta ukikabiliwa na hatari ya kumsaliti mpenzi wako. Kujaribiwa huko kunaweza kukutokea katika mazingira mbalimbali kutegemea na maeneo yako ya kazi au mahali unapofanyia shughuli zako za kila siku. Kwa mfano inaweza ikatokea umefahamiana na mwanaume mahali pako pa kazi, anaweza kuwa ni mteja au mfanyakazi mwenzio. Inatokea siku moja anakualika kwa ajili ya chakula cha mchana, baada ya mtoko huo, unajisikia kutoka naye kwa mara nyingine…………………

Kutoka kwenu mara kwa mara kwenda kupata chakula cha mchana, unagundua kwamba huyu bwana ni mtu mwenye kiwango cha juu ya usikivu, katika mazungumzo yenu anaonekana sana kwamba ni mwelewa na mwenye subira. Hana papara katika kuzungumza na mara nyingi huwa ni msikilizaji. Huyu unaweza kumwita rafiki ingawa ni wa jinsia tofauti, (Sidhani kama ni dhambi kuwa na rafiki wa jinsia tofauti……!)

Kuna kitu wenzetu wazungu wanakiita Emotional infidelity, kwa tafsiri yangu naweza kusema ni hisia za usaliti katika mapenzi. Maana yake ni kwamba unaruhusu mtu mwingine wa jinsi tofauti azibe pengo la hisia ambalo lingetakiwa lizibwe na mpenzi wako au mume wako. Kama inavyofahamika kwamba wanawake ni viumbe wa hisia, wanapenda sana kusikilizwa, na wanapenda kuona wapenzi wao au waume wao wanawasikiliza. Inapotokea hitaji hilo halitekelezwi na mpenzi au mume wake, basi ni rahisi sana atakapotokea mtu mwingine ambaye bila kujua akamudu kuziba pengo hilo kuvutiwa naye na kuhitaji kuwa naye karibu mara kwa mara.
NetworkingManWomanLunch620480.jpg

Hapa chini nitazitaja dalili ambazo zitakuonyesha kwamba ukaribu wako na huyo rafiki utakupelekea kuisaliti ndoa yako:

1. Unatamani sana kumuona ukiwa na shauku kubwa ya kuwa naye karibu na kutumia muda mwingi kuwa naye

2. Unajikuta ukichagua mavazi na kujikagua sana ukijiuliza jinsi atakavyo vutiwa na mavazi yako pale atakapokuona

3. Unapokuwa naye unajikuta ukimweleza matatizo ya mahusiano yako na mpenzi wako au mumeo

4. Unajikuta ukimgusa gusa wakati mkiongea au kufanya naye utani unaoweza kupeleka ujumbe tofauti kwake kwamba labda umevutiwa naye kimapenzi.

5. Unawsiliana naye kwanza kabla ya kuwasiliana na mpenzi wako au mumeo pale unapokabiliwa na jambo lolote lenye kutatiza na linalohitaji msaada wa haraka au ushauri

6. Unajikuta ukiwaza jinsi gani ungekuwa na amani iwapo ungekuwa na uhusiano naye wa kimapenzi au ndoa

7. Inawezekana ukawa unamzuingumzia sana kwa mwenzi wako au kwa marafiki zako, au inawezekana ukawa humzungumzii kabisaaa na kuficha urafiki wenu.

8. Unajitahidi sana kuficha urafiki wenu na kutomzunguimzia rafiki huyo kwa mwenzi wako kwa sababu unajua kwamba jambo hilo linaweza kukuletea balaa.

Kwa ujumla unapojikuta umempata rafiki mwenye jinsia tofauti na yako halafu ukahisi kulipukwa na moyo juu yake zikiwemo dalili nilizozitaja hapo juu, basi ujue uhusiano wako na mume au mpenzi wako uko mashakani. Usipokuwa makini utamsaliti.

ANGALIZO:Wiki ijayo nitawaletea thread ya jinsi ya kushinda hicho kishawishi na ndoa au uhusiano wako ukaendelea kuwa imara. Kumbuka kwamba hakuna mwanadamu mkamilifu, inawezekana kile kilichokuvuta kwa rafiki huyo mpya ikawa ni sifa ya muda tu, baada ya kuwa naye ukagunduia mapungufu mengi sana ambayo yatakupelekea kujuta……………..
 
eeeer emotional infidelity...duh, nahc kwa dalili hzo imeshanikumba mara kadhaa lol...

haswa kwa namba 3 na 8.......

Asante kwa kunishtua ......
 
Asante kwa mada nzuri zenye mafunzo. Ki-ukweli binafsi nathamini sana juhudi zako za kuelimisha jamii yetu ya kitanzania kupitia JF. Nina imani kubwa, kwa watu wanaosoma kwa uelewa, na kuyabaini mapungufu yao na kuamua kubadilika wanaweza kuepuka adha nyingi sana za migogoro ya kimahusiano.

Thanks.
 
Duh ni ukweli mwingine mchungu au ukweli ambao hausemwagi!
Nasubiria kwa hamu hizo mbinu za kushinda nilinganishe na ninazotumia mimi, najua nitapata cha kuongezea!
 
Mtambuzi hiyo ni kweli kabisa Bro, ndoa nyingi zinaharibika kutokana na kukosa emotional support at home unajikuta automatically attached to that person who lend his ears. Kwa upande wa wa wanaume ni opposiste, ukimnyima game ataenda mtaa wa pili ataupata.

Mimi ninavyofikiri ni muhimu kwa mwanaume kujifunza kumsikiliza mpenzi wako, thats what all woman want. Sometimes we talk nonsense but we just wanna take the pressure outside. Giving the ears will just do wonder!
 
Last edited by a moderator:
Duh ni ukweli mwingine mchungu au ukweli ambao hausemwagi!
Nasubiria kwa hamu hizo mbinu za kushinda nilinganishe na ninazotumia mimi, najua nitapata cha kuongezea!
Kaunga nilikuwa na emagine jinsi ambavyo ungenipinga............... Kumbe once again leo hujanikosoa..................LOL
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi hiyo ni kweli kabisa Bro, ndoa nyingi zinaharibika kutokana na kukosa emotional support at home unajikuta automatically attached to that person who lend his ears. Kwa upande wa wa wanaume ni opposiste, ukimnyima game ataenda mtaa wa pili ataupata.

Mimi ninavyofikiri ni muhimu kwa mwanaume kujifunza kumsikiliza mpenzi wako, thats what all woman want. Sometimes we talk nonsense but we just wanna take the pressure outside. Giving the ears will just do wonder!

Namshukuru Mungu nilijifunza UTAMBUZI kabla sijawowa, leo hii Mama Ngina anajivunia ndoa yake ambayo mwezi huu tarehe 25 itatimiza miaka 8........................
 
Mkuu Mtambuzi kwa hapa sina la kuongeza..
Probably i will add some on your next uzi..
However big up aisee..mwenye macho haambiwi tazama!
 
Last edited by a moderator:
Namshukuru Mungu nilijifunza UTAMBUZI kabla sijawowa, leo hii Mama Ngina anajivunia ndoa yake ambayo mwezi huu tarehe 25 itatimiza miaka 8........................

Shule gani hiyo inatoa hayo mafunzo, uwahabarishe wengine ili nao wafaidike
 
Mtambuzi hiyo ni kweli kabisa Bro, ndoa nyingi zinaharibika kutokana na kukosa emotional support at home unajikuta automatically attached to that person who lend his ears. Kwa upande wa wa wanaume ni opposiste, ukimnyima game ataenda mtaa wa pili ataupata.

Mimi ninavyofikiri ni muhimu kwa mwanaume kujifunza kumsikiliza mpenzi wako, thats what all woman want. Sometimes we talk nonsense but we just wanna take the pressure outside. Giving the ears will just do wonder!
Sijui uliwahi kusoma huu uzi.................
https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/169165-wanawake-wanajua-kudeka-we-acha-tu.html
 
wanaume wakware wanaojua ku-fake mapozi ya kujifanya wako 'compassionate and understanding' huwa wanatumia sana hizi opportunity 'kufunga magoli ya kisigino' if you know what i mean
 
wanaume wakware wanaojua ku-fake mapozi ya kujifanya wako 'compassionate and understanding' huwa wanatumia sana hizi opportunity 'kufunga magoli ya kisigino' if you know what i mean
Sasa umeshajua, ni vyema kujihami............................
 
Hii inahusiana na ukweli kuwa ukitaka kulinda penzi lako kwa umpendae...inabidi uepuke ukaribu na jinsia nyingine...kwani inachangai kuona mapungufu ya mpenzi wako zaidi ya kuona strength yake....not to say ni invitation to treat. Lol
 
Mtambuzi habari ya kwako? Asante sana kwa mafunzo maana hii dunia kila kukicha inabidi kujifunza.
Hapo nambari nne nimeshtuka kidogo itabidi niwe makini nakutana nazo sana hizi.......lol
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom