Wanawake wenzangu mnawezaje kumudu wanaume wabinafsi waongo wanaojifikiria wao tu?

Jamani hivi wamama mnawezaje kumudu hawa wanaume wabinafsi? Yaan mwanaume asiyesikia uchungu au maumivu ambaye wewe kama mwanamke wake unayapitia

Mwanaume opportunitist tu,selfish tu, anajali tu maisha yake tu

Mwanaume ambaye ni muongo kwa asilimia 99

Kudanganya kupo ila sio huyu wangu aisee kila kitu lazima adanganye hadi wazazi wake alinidanganya

Najuta kuzaa na hili jianaume looh ningejua kipindi kile cha mimba ningetoa tu ila huyu mwacheni siku yake itafika tu
Ala kumbe mada inawahusu kina mama ngoja sie kinababa tupite vile
 
Jamani hivi wamama mnawezaje kumudu hawa wanaume wabinafsi? Yaan mwanaume asiyesikia uchungu au maumivu ambaye wewe kama mwanamke wake unayapitia

Mwanaume opportunitist tu,selfish tu, anajali tu maisha yake tu

Mwanaume ambaye ni muongo kwa asilimia 99

Kudanganya kupo ila sio huyu wangu aisee kila kitu lazima adanganye hadi wazazi wake alinidanganya

Najuta kuzaa na hili jianaume looh ningejua kipindi kile cha mimba ningetoa tu ila huyu mwacheni siku yake itafika tu
Pole Sana...
Hii ni changamoto na ichukulie ni sehemu ya kujifunza..Usianze kujuta mara kutoa mimba..humtendei haki mtoto,ambaye hana hatia katika hili..
Badilisha mindset yako,focus kwa mwanao..Wakati mwingine kuwa na mtazamo chanya inasaidia amaniya moyo na kusonga mbele.Huwezi jua mwanao atakuja kua nani na pengine msaada wako..
Keep your head up..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Huyo ndiye chairman wetu tunashukuru ameitendea haki ilani yetu,

Mwanaume Ukiwa mkweli na kujifanya mtu wa kujali saana utatoswa vyakutosha mpaka masia anarudi
 
Mkuu uliachia papuchi ukitegemea atakupa hela ila amekuacha solemba...

Jifunze kujitegemea Mama..
 
Kwani hamkufunzwa wanaume wa kudate nao?

Au mnababaishwa na vile vipesa pesa vya awali kabla ya kunaswa na ulimbo!!
 
Mwanaume opportunitist tu,selfish tu, anajali tu maisha yake tu

Mwanaume ambaye ni muongo kwa asilimia 99

Sema Kweli wewe haupo hivyo??
Upo hivyo ila jamaa kakuzidi kete... unaonekana mjanja mjanja
 
Shida ni kuwa wewe hutaki kuendelea kudanganyika. Jua umedanganywa na endelea kudanganywa na endelea kukubali uongo wake. Basi maisha yanakuwa poa.

Kuhusu kutoa ujauzito mawazo uliyonayo sio mazuri. Penda mtoto wako. Na ni "wako wewe" mtunze vizuri wacha roho mbaya kama mlozi.
 
Pole sana...

Inawezekana hata hiyo mimba pia alikudanganya, kipindi mna duu alipanda mwingine kwa niaba yake...
 
Unakuwa mbinafsi mara kumi yake...mchoyo zaidi yake....

Unapita na tabia zake zile zile!!!
 
Back
Top Bottom