Wanawake wenye umri kuanzia miaka 30 wapo kwenye hatari ya kuugua Saratani ya Matiti

Display Name

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
410
500
Wanawake walio na umri wa miaka 30 walio na historia katika familia ya jamaa zao kuugua saratani ya matiti, wanapaswa kufanyiwa ukaguzi wa kila mwaka kubaini mapema iwapo wanaugua ugonjwa huo, shirika la misaada linasema.

Breast Cancer Now limefadhili utafiti uliobaini kwamba saratani hutambulika mapema wakati wanawake wenye umri wa kati ya miaka 35 hadi 39 walio katika hatari ya kuugua wanapofanyikwa ukaguzi wa kila mwaka yaani mammograms.

Wataalamu wanahitaji kupima baina ya faida za kufanyiwa ukaguzi zaidi dhidi ya kusababihsa wasiwasi usiohitajika au kutibu ugonjwa usiokuwepo.

Wahariri wa utafiti huo, wamesema kwamba kuna uchambuzi zaidi unahitajika kuhusu hatari, gharama na faida za kuendeleza mpango wa ukaguzi.

Utafiti huo uliofanywa na watafiti katika chuo kikuu cha Manchester, kimetoa picha au scan za wanawake 2,899 wa umri huu walioonekana kuwa katika hatari kubwa na ya wastani ya kuugua ugonjwa huo baada ya kumuona daktari.

Ukaguzi huo umegundua uvimbe 35 wa ndani ya matiti, baadhi ukiwa ni mdogo na uliotambuliwa mapema - ishara kwamba haujasambaa mwilini.

Kutambua kwa ufanisi

Katika kundi lililodhibitiwa, ambalo halikufanyiwa ukaguzi, visa kidogo vya saratani viligunduliwa wakati bado ni vidogo na uvimbe mwingi ulisambaa hadi katika mfumo wa kinga.

Profesa Gareth Evans, mhariri mkuu wa utafiti huo, amesema utafiti huo unaonyesha kwamba kufanyiwa ukaguzi wa kila mwaka inasaidia katika kutambua uvimbe mapema kwa kundi hili la wanawake.

Amesema ukaguzi wa kupita kiasi - ambapo watu wanatibiwa kwa saratani ambazo huenda hazina madhara huenda sio isiwe tatizoi kwa kundi hili la vijana.

"Kwa wanawake wenye historia katika familia, kuondosha uvimbe pasi kufaniwa upasuaji huenda ni njia ya kuzuia saratani ," amesema Profesa Evans.

Utafiti huo haukujumuisha wanawake walio na aina fulani ya jeni mwilini ambayo ina uwezo ya kuongeza hatari ya kuugua ugonjwa huo.

Shirika hilo linasema scan, au picha za MRI - as is kama inavyopendekezwa sasa - ndio njia bora kwa watu walio na jeni za TP53.
Ni nani anayekaguliwa matiti?

Wanawake hufanyiwa ukaguzi wanapotimia miaka 50.Na wanastahili kufanyiwa hivyo kila baada ya miaka mitatau mpaka watakapotimia miaka 71.Kama uko katika hatari ya kuugua saratani ya matiti, huwa una jeni fulani au kama una jamaa ambao wamewahi kuugua saratani ya matiti, huenda unahitaji ukaguzi wa kila mwaka.Ni vizuri kupata ushauri wa daktari wako kuhusu hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom