Wanawake wenye sura hii hawajali na wanajua kupenda…!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,395
black-woman-laughing.jpg

Unaiona sura hiyo hapo juu? Hiyo ni sura ya mwanamke ambaye anacheka. Lakini hata kama angekuwa hacheki, bila shaka ungeweza kuibaini sura yake kama unavyoibaini hivi sasa.

Mwanamke mwenye sura kama hiyo ni mwanamke smati sana, yaani anayajua sana maisha. Hii ina maana kwamba huyachukulia maisha kama yanavyokuja. Hukubaliana na kile ambacho kwa wakati huo ndicho kilichopo.

Mwanamke wa sura hiyo ni mchapa kazi na asiyejali sana kuhusu kazi gani anafanya, bora mkono unaenda kinywani. Ni sura ya kipaji na mara nyingi ni kipaji cha usanii au urembo. Anapobaini kipaji chake hufika mbali sana, lakini kwa namna alivyo anaweza kuonewa sana pia.

Ni mwanamke mwenye kujua upendo hasa, yaani akimpenda mtu, hampendi kwa kile alicho nacho na wala hampendi kwa masharti. Kumpenda mtu kwa masharti ni kuonesha upendo kwa msimu tu, yaani pale ambapo mtu amekutendea wema na wewe ndio unatenda.

Mwanamke wa aina hii hupenda bila kujali ametendewa nini na mpenzi. Lakini akiona mpenzi mwenyewe habebeki huamua kuondoka. Mwanamke wa namna hii huwa hajali sana kuishi mwenyewe, hajali sana kupoteza mpenzi, kama ni lazima ampoteze. Lakini ujue hapo amejitahidi kumsaidia huyo mpenzi hadi kufikia kumpoteza.

Hebu tazama zaidi midomo kuliko sehemu nyingine. Kwa kawaida hiyo ni midomo ya ucheshi na uelewa na ni midomo ya mzaha na masihara mengi yasiyoumiza. Maringo yapo kidogo lakini yanafichwa na huruma. Sura ya namna hiyo ni sura ya huruma na kujibainisha.

Kama mwanaume ametulia na kupata mwanamke wa aina hii anaweza kufurahia sana ndoa yake kwa sababu hatasumbuliwa na vijilawama vya hapa na pale, hatazongwa huku na kule na hataziriwa. Sura hiyo haijui kuzira, inajua kukasirika hapohapo na kugeuza hasira kuwa mzaha.

Lakini kwa bahati mbaya, kama sura hii imezaliwa na kulelewa kwenye familia yenye majivuno au yenye ugomvi miongoni mwa wazazi, hugeuka na kuwa mtu mwenye majivuno, dharau, hasira za haraka na kutojua kupenda. Lakini hii sio mara nyingi sana.

Sura hii ni ya mwanamke asiyejali sana kuhusu ngono, hasa kama amelelewa mahali ambapo ngono haikutiliwa nguvu sana. Lakini kama amelelewa mahali ambapo fedha ziliwekwa mbele na ngono ikatajwa kama kitu cha kawaida, hupenda ngono ajabu ya Mungu. Lakini pia idadi ya hawa siyo kubwa sana.
 
Ni Mzuri ni wale niwapendao nikikutana nao lazima kieleweke .....................!:bowl:
 
Wewe subiri, kuna siku utaiona sura yako hapa live na vijitabia vyako......

NAsubiria kwa hamu sana uiweke

Hahahaa Zamadamu weye....chezeiya Kongosho teh teh teh..................!

Mwenzangu, hadi najiogopa sasa

Hivi sura yako ikoje Kongosho, inafanana na ya bi kidude? Tehe tehe teheee au ...?! Post picha yako hapa Mtambuzi akufanyie mambo maana nahisi sura zote anazo na maelezo yake!

He he he, bi kidude inahu? Bishanga kutwa kucha ananililia
 
Last edited by a moderator:
Wewe subiri, kuna siku utaiona sura yako hapa live na vijitabia vyako......
Mh Mkuu Mtambuzi sijui umeniona ndiyo ukaamua kuweka hapa jinsi nilivyo? maana 99% ya tabia hizo ninazo Duh! nimeshangaa sana. unazitoa wapi?
 
Unafikiria Bishanga analilia sura pekee yake? Tehe tehe tehheeeeee, muulize vizuri!!!!

Analilia sura na kinginenajua, ujue nilikia ananifuta machozi kwa leso gani??

HorsePower nilitaka nimuulize swali hilo hilo Bishanga sidhani hata kama anaijua vyema sura ya Kongosho ila muulize mengine yote atakuwa anayajua

Ananijua vyote vyote, hasa lips lol

Hapana...kwa sababu wewe umepitwa na wakati.
Ujue unaniumiza mtima kusema maneno hayo??
Ngoja nije niweke avatar yangu orijino
 
black-woman-laughing.jpg

Unaiona sura hiyo hapo juu? Hiyo ni sura ya mwanamke ambaye anacheka. Lakini hata kama angekuwa hacheki, bila shaka ungeweza kuibaini sura yake kama unavyoibaini hivi sasa.

Mwanamke mwenye sura kama hiyo ni mwanamke smati sana, yaani anayajua sana maisha. Hii ina maana kwamba huyachukulia maisha kama yanavyokuja. Hukubaliana na kile ambacho kwa wakati huo ndicho kilichopo.
hiyo hapo ni kweli kabisa huwa siwazi sana kuhusu maisha na huwa yananiendea vizuri tu.

Mwanamke wa sura hiyo ni mchapa kazi na asiyejali sana kuhusu kazi gani anafanya, bora mkono unaenda kinywani. Ni sura ya kipaji na mara nyingi ni kipaji cha usanii au urembo. Anapobaini kipaji chake hufika mbali sana, lakini kwa namna alivyo anaweza kuonewa sana pia.

Yaani kaka mtambuzi hapo kwenye point hiyo ni kweli kabisa mm nilikuwa sijui kama naweza kuwa MC lkn nimegundulika na kwa sasa naifanya vizuri sana.

Ni mwanamke mwenye kujua upendo hasa, yaani akimpenda mtu, hampendi kwa kile alicho nacho na wala hampendi kwa masharti. Kumpenda mtu kwa masharti ni kuonesha upendo kwa msimu tu, yaani pale ambapo mtu amekutendea wema na wewe ndio unatenda.

Mume wangu hakuwa na kazi ila mm nilikuwa na kazi nikamvumilia mpk sasa tunakila kitu

Mwanamke wa aina hii hupenda bila kujali ametendewa nini na mpenzi. Lakini akiona mpenzi mwenyewe habebeki huamua kuondoka. Mwanamke wa namna hii huwa hajali sana kuishi mwenyewe, hajali sana kupoteza mpenzi, kama ni lazima ampoteze. Lakini ujue hapo amejitahidi kumsaidia huyo mpenzi hadi kufikia kumpoteza.

Hebu tazama zaidi midomo kuliko sehemu nyingine. Kwa kawaida hiyo ni midomo ya ucheshi na uelewa na ni midomo ya mzaha na masihara mengi yasiyoumiza. Maringo yapo kidogo lakini yanafichwa na huruma. Sura ya namna hiyo ni sura ya huruma na kujibainisha.

Kama mwanaume ametulia na kupata mwanamke wa aina hii anaweza kufurahia sana ndoa yake kwa sababu hatasumbuliwa na vijilawama vya hapa na pale, hatazongwa huku na kule na hataziriwa. Sura hiyo haijui kuzira, inajua kukasirika hapohapo na kugeuza hasira kuwa mzaha.

Lakini kwa bahati mbaya, kama sura hii imezaliwa na kulelewa kwenye familia yenye majivuno au yenye ugomvi miongoni mwa wazazi, hugeuka na kuwa mtu mwenye majivuno, dharau, hasira za haraka na kutojua kupenda. Lakini hii sio mara nyingi sana.

Sura hii ni ya mwanamke asiyejali sana kuhusu ngono, hasa kama amelelewa mahali ambapo ngono haikutiliwa nguvu sana. Lakini kama amelelewa mahali ambapo fedha ziliwekwa mbele na ngono ikatajwa kama kitu cha kawaida, hupenda ngono ajabu ya Mungu. Lakini pia idadi ya hawa siyo kubwa sana.

Ugomvi wangu mkubwa na mume wangu ni Ku do! huwa sipendelei sana , na hata hapa kazini sikupandishwa cheo kwa miaka 5 kwa sababu nilimyima boss K.
 
Kuna mmoja namfahamu alimkimbia mume wake na mtoto akatokomea abroad na mzungu..km miaka 4 hivi imepita.
 
Sura kama hizo ni adimu kwanza,Sura za skuhizi makovu kibao kama lami ya mlandizi-chalinze.Hebu nipe forecast ya sura hii hapa chini,bila shaka hawa wenye sura hii ni wadokozi wa mboga.
 
Attachments

  • funny_faces_14.jpg
    funny_faces_14.jpg
    40.8 KB · Views: 139
Back
Top Bottom