Wanawake wengi (wazuri wachache wapo) tuna roho mbaya mno

Chakorii

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
18,579
50,669
Habari ya muda huu natumai muwazima nyote.
Moja kwa moja nisipoteze muda.

Tukio la leo(jana) limenifanya nikakumbuka miaka michache iliyopita nilipoteza fahamu katika moja ya usafiri wa umma, kizunguzungu kikali sana kilinipata nikajikuta naanza kuyumba (kupepesuka)nilikuwa natafuta nafasi ya kupata fresh air...aiseh kila niliyekuwa natua kwake alikuwa ananisukuma na kunikwepa na hao walionifanyia hayo ni wanawake wenzangu😢😢😢(hapo taratibu naanza kupoteza fahamu) nakumbuka kabla macho hayajazima kabisa nilimuona mwanaume kwa mbali akinidaka.baada ya hapo sikumbuki nini kiliendelea lakini nilijikuta hospital.

Kilichotokea leo(jana)
Mmama omba omba,kipofu na yuko na mtoto wa mwaka na nusu au miaka miwili hivi mgongoni katika harakati zake za kujitafutia mkate wa kila siku(kuomba)akawa anatafuta namna ya kutoka(sehemu aliyopo ilikuwa inawatu na mtoto alikuwa anaanza kulia)alikuwa anatumia ile fimbo yake so ikawa kila akipapasa fimbo inawagusa watu(niliona wanawake kama 15 hivi wamekaa sehemu moja.nilikuwa kwa mbali lakini niliweza ona kila kitu)cha ajabu wote walikuwa wanamkwepa(Sijui walikuwa wanajikuta nani kwa mfano)😭😭😭kwa hiyo ikawa kila akipapasa na kutembea anaparamia Watu🥺🥺..nilitamani kama ningekuwa Karibu ningemsindikiza mpka sehemu ya njia aendelee na mizunguko yake maskini ☹️☹️..

😊😊😊kwa mbali nikamuona mwanaume mmoja akimsaidia yule mama kidogo huzuni ikapungua.

Sio mara moja kuona mwanamke akishindwa kumsaidia mwanamke mwenzie au mtu mwingine yeyote ili hali uwezo wa kumsaidia anao☹😔😔😔(sizungumzii pesa wala sio kwamba wanawake wote wana roho ngumu sana hapana wachache sana wanakuwa na mioyo mizuri mpka unamshangaa!!huyu ni mwanamke kweli?)sijui ni nini mbaya na sisi jamani 😢😢
Sizungumzii kusaidia kila mtu hapana nazungumzia wale watu ambao wanauhitaji hata kwa kuwaangalia tu.

Sijaandika haya ili nionekane pengine mimi ni ni mtakatifu hapana mi mwenyewe ninamapungufu kibao lakin swala la kumsaidia mtu haliangalii mapungufu wala uhimara wa mtu.inaangalia moyo wako Na huruma na kujivalisha kiatu cha mhusika unaemuona anahitaji msaada kwa wakati huo.

Nilijaribu kuvaa viatu vya yule mama nikajikuta nashindwa kabisa huzuni ilinijaa nafsini mwangu🥺🥺🥺kuliko kawaida, najua Ni ngumu kubadilisha vitu kwa haraka taratibu wanawake wenzangu tujaribu kuvaa viatu vya wahusika(kama yule mama asiyeona)pengine inaweza kusaidia kutoa msaada wa haraka kwa wahitaji..pengine.

Sisemi wanaume wasisaidie...hapana!kati ya wanaume na wanawake,mwanaume ndie kiumbe mwenye huruma zaidi kuliko mwanamke.usiniulize utafikiti wangu nimeufanya wapi,Hata wewe unaweza jifanyia utafiti hapo ulipo kuhusiana na hili😌😌😌

Naomba nipunguze hili gazeti.
Mshukuru Mungu kwa alivyokuumba kuna mtu mwingine hana baadhi ya viungo ulivyonavyo wewe.

Tuwe ni watu wa kusaidia wengine bila mategemeo yoyote kwa kidogo tunachojaaliwa tupate thawabu kwa Mungu.👏👏

GM.
 
Mwali, huyo mwanaume aliye kudaka alikua ni mimi...😋
Ila polesana, maana ile siku ilikua kidogo ujigonge kwenye kile chuma cha kwenye kona ya seat ya bus. Bahati yako tu nilikuwahi..🤠
Hata hivyo Adam aliponzwa na mwanamke Hawa, pia Samson aliponzwa na mwanamke Delilah. Pia Mungu mwenyewe alituasa sisi wanaume tuishi nanyi wanawake kwa akili.
 
Basi kwa maelezo hayo na malizia kwa kusema

Mwanaume kaumbwa na roho mzuri kuliko mwanamke..

Mimi hata hizi harakati zenu za kumuinua mwanamke kama wanawake wangekuwa na roho ya utu km wanaume nyinyi mngekuwa mmefika mbali sanaaaaaaaaaaaaaa cha ajabu hata kwenye hizi harakati ni sisi wanaume tunashiriki kuwa push wanawake kwenye biashara either mambo ya mitaji au connection nzuri za biashara

huu ni ukweli mchungu sana
 
Roho mbaya haina jinsia usitulaumu wanawake bure, msaada ni uamuzi wa mtu
Mimi pia ni mwanamke kumbuka hilo.aya ya kwanza pale juu haikumtokea mtu baki unajua..ilinitokea mimi Chakorii na aliyedaka nilipokuwa naanza kupoteza fahamu ni mwanaume.wanawake wenzangu walikuwa wananisukuma.

Na hilo unalizungumziaje labda🎤
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom