Wanawake Wengi Wanaojiuza Maeneo ya Manzese ni Wake za Watu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake Wengi Wanaojiuza Maeneo ya Manzese ni Wake za Watu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 11, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  IMEDAIWA kuwa wanawake wengi wanaofanya biashara ya kuuza miili yao katika maeneo ya Manzese jijini Dar es Salaam ni wake za watu na imegundulika kuwa wanaagizwa na waume zao wakafanye biashara hiyo ili wapate pesa za kujikimu. Hayo yamegundulika katika utafiti wa kina uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Madawa Afrika [AMREF]

  Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Meneja wa Mradi wa Haki za Wananchi wa taasisi hiyo, Michael Kimaryo, wakati wa semina iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa habari za Ukimwi (AJAAT) kwa kushirikiana na taasisi hiyo.

  Kimaryo alisema walibaini hali hiyo wakati walipokuwa wakifanya ufuatiliaji kuhusu mradi huo uliolenga kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya afya ya ukimwi na mambo mengine katika maeneo ya Manzese, Tandale na Kiwalani, Vingunguti na kwingineko

  Alisema wanawake hao wamejiingiza katika biashara hiyo ambayo waume zao majumbani wanatambua hali hiyo na huwaruhusu ili waweze kujipatia kipato cha siku cha kujikimu na familia zao.

  Mradi huo wa AMREF ulianzishwa mwaka 2008 ukiwa na lengo la kuwakomboa wananchi katika nyanja mbalimbali, kuwaelimisha kuhusiana na ugonjwa wa ukimwi na jinsi ya kujikinga na walioathirika kujifunza njia za kuepuka kuwaambukiza wengine.

  Mradi huo ulilenga zaidi maeneo ya Manzese na Tandale.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4463322&&Cat=1
   
 2. M

  Mundu JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Duh, hii sasa kali. Lakini yote yanawezekana chini ya jua.
   
 3. D

  Dick JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi hawa washkaji hawana hata chembe ya wivu? Sipati picha hata kidogo.
  Lakini nisichonge sana, life ni ngumu kichizi.
   
 4. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kati yao wamo "wanaoishi" na wanaume, kama mwanaume ni kibaka unategemea mke atakuwa nani!?
  Lakini sitaamini kama watu waliooana kihalali na kula kiapo wakapanga kufanya biashara ya ukahaba!....sitaamini mapaka waniletee mifano migumu. Kwanza kauchunguzi kenyewe kamekaa simposimpo tu, weka details, hii sensa ya kuuliza watu "umeolewa?" jibu:NDIYO! unatally!!!!
   
 5. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #5
  May 12, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hivi viji study vingine havina mbele wala nyuma ni kupotosha jamii tu. Maana anasema wanawake wengi hii ina maana wanaojiuza manzese kama ni 10 basi zaidi ya watano ni wake za watu na wameruhusiwa (taja na nature ya kazi za waume zao, maana lazima nao mtakuwa mmeenda kusema nao). Harafu paper yenyewe hawajaiweka wanaongea toka hewani wanaogopa tuta wa challenge. Hawa nawafananisha na mkuu wa mkoa (Sina hakika kiongozi gani ila ni singida) wa Singida ambaye mwaka 2007 alisema prevelence ya Singida ni more than 60% sikumbuki figure vizuri, Lowasa akiwa waziri mkuu alipotuma wataalamu wa wizara ya afya wakakuta kumbe jamaa alichukua waliotest HIV akagawanya kwa waliokuwa positive. Sasa na hawa wasibaki kuongea tu waweke paper hapo juu, sio kupotosha jamii.
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  May 12, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  DUh hii kali Mno. lkn nadhani si ndoa halisi, hawa wanaume wanaishi tu na hao wanawake!!!!!!!!!!
   
 7. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #7
  May 12, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  uo utafiti sijui ulitafitiwaje, au walienda mawindo wakawa wanawauliza kiupelelezi? ahahaha, OK then, hayo ndo maisha bora kwa kila mtanzania ambayo kikwete aliahidi....mpeni kura zingine ndo mtakuta nchi sasa ndo inageuka ohio street kila mkoa...watu watafanyeje sasa, hawana jinsi...inauma sana kuona mtu anafanya kitu kama hicho kwasababu hakuna namna ingine anaweza kufanya, ...too sad.
   
Loading...