Wanawake wengi wameshikiwa akili na washauri wa mitandaoni?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,080
103,310
Sijui kama ni mfumo wa maisha umebadilika au lah.

Kumeibuka kundi kubwa la washauri wa mambo ya mahusiano huko mitandaoni hususasi facebook. Baadhi yao wanatumia majina ya Iddi Makengo, Chrisa Mauki na wengine wengi

Tatizo langu sio hao washauri, bali ni hawa baadhi ya watu wanaopeleka matatizo yao huko..nasisitiza baadhi,sio wote.

Baadhi ya mambo yanayoombewa ushauri yanadhibitisha wanawake wengi siku hizi wameshikiwa akili. Hawatumii tena akili-common sense katika kutatua matatizo yao.

Nasema hivyo kwa sababu baadhi ya changamoto zinakuwa wazi au mambo ya kuyamaliza ndani ya familia. Kwa lugha rahisi sio mambo magumu au makubwa kiasi cha kukimbilia mitandaoni au kwa hawa washauri.

Kwa mfano; niliwahi kusoma dada akiomba ushauri wa jinsi ya kumzuia kaka yake anayetaka kuoa mwanamke mwenye mtoto. Unajiuliza huyu anataka ashauriewe nini, kama nani? Mwingine anaomba ashauriwe kama ni sawa kuolewa na mwanaume aliyejuawa naye ndani ya miezi miwili. Unajiuliza huyu hata common sense anatumia kweli?

Binafsi naona changomoto nyingi za kifamilia zinaweza kupata msaada wa kutatuliwa na mtu anayezijua vizuri na kupata kusililiza pande zote ili kubalance. Ajabu ndugu zetu hawa wamekuwa wepesi kukimbilia mitandaoni wakiamini kupata msaada ilihali wakijua hao wanaowasimulia hawajui mengi kuhusu familia zao.

Nafasi ya wazazi
Wasichana wa siku hizi wamepuuza nafasi za wazazi kwenye changamoto za mahusiano. Badala yake mitandao imekuwa kimbilio lao kwa sababu wana mitandaoni hawana nafasi ya kusikiliza pande zote kwa hiyo wanajikuta wanaharibu zaidi.

Nawashauri wanawake kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii kusaka ushauri wa mahusiano. Badala yake tumieni wazazi, ndugu wa karibu, taasisi za dini zetu na watu wanaowazunguka wawasikilize wote na kuwapa ushauri mujarabu.

1624021784581.png

 
Wenzetu ni wepesi kuamini
Hicho tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hicho tuu. juzi kati kuna dada aliniomba ushauri anataka kuolewa na jamaa amejuana naye kama mwezi tu,anataka kwenda kwa wazazi. nikamuuliza wewe unasemaje?akaniambia hajui cha kufanya ila jamaa anaonekana ana nia nzuri naye. nikamuuliza hiyo nia nzuri umeiona ndani ya mwezi?
 
Back
Top Bottom