Wanawake wengi tabia zao hubadilishwa na rafiki zao wa kike

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
4,326
2,000
Asilimia kubwa ya wanawake ambao wengine ni wake zetu, wapenzi wetu, dada zetu, mama zetu, ndugu zetu n.k.

Ila kwa uzoefu nilionao wanawake wengi ukiona kabadilika kwa mazuri au mabaya basi tambua akili yake au ufahamu wake unashikiliwa na mwanamke mwenzake, haijalishi ni ndugu, rafiki, jirani, wala tumbo moja.

Mfano: Mzuri ukiona mpenzi wako ana rafiki, ndugu, mama, jirani jinsia moja na wemeshibana mwenye tabia za ajabu au umuelewi mwenendo wake basi tambua kuna siku kitakacho kutokea kimesababishwa na hayo.

Wanawake wengi hubadilishwa na wanawake wenzao kuanzia mambo mazuri au mabaya. Visa vingi vya kubadilika kwa mwanamke ubadilishwa na rafiki au mtu wa karibu jinsia ya kike.

Kisa kimoja: Kuna jamaa alipata ajali ambayo ilimpelekea kupoteza mguu wake ila yule mpenzi wake alikuwa mzuri sana na marafiki zake waka mshauri kuachana naye ili kupata mwanaume aliye kamilika au sio mwenye tatizo.

Kweli bwana! kafanya hivyo na kupata mwanaume mwenye vigezo vya rafiki zake wanavotaka, miaka kwenda naye alikuja kupata ajari ikasababisha kukatika miguu miwili. Yule mwanaume kuona hivo naye kapiga china kuepuka mzigo wa mateso.

Sasa huyu dada anaomba kurudiana na jamaa! na jamaa kwa sasa ana familia na ndoa kwanza changa.
 

Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
7,405
2,000
Nimeiona Avatar Ya Hamza Tu
Uliyoyaandika Yanatuchelewesha Mno Ndugu Zangu
Atakua answaar suna huyu jamaa. Wale wanaoamini ukimuua rafiki yako utapata utajiri na ukienda ahera utapewa mabikra 72. Sijui anayewaandalia mabikra anafaidikaje.
 

Lenie

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
4,563
2,000
Inategemea na akili ya mtu, kama hajielewi atabadilishwa tabia hadi na tamthilia za kifilipino
 

raphael andrew

JF-Expert Member
Aug 27, 2017
557
1,000
Ni kweli kabisa hata ukiona demu wako kakukacha ghafla tu jua sio yeye ni ushauri kutoka kwa marafiki zake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom