Wanawake wengi siku hizi hawajui au hawataki kuonesha mahaba

nyaggad

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
1,160
692
Habari wakuu!

Nimefanya kautafiti kangu kadogo nimegundua wanawake wengi siku hizi hawaonyeshi mahaba yani kwa ujumla hawako "Romantic". Wanawake wengi siku hizi akipata mwanaume anaona amepata mtu wa kumsaidia shida zake kwa hiyo hata akiwa ndani ya mahusiano anafikiria zaidi kutatuliwa shida zake kuliko mahusiano yenyewe.

Wanawake wa siku hizi wengi, kwa mfano umemtoa out kidogo mkapate walau msosi sehemu nzuri, mkianza kula mpaka mnamaliza hakumbuki hata kukulisha kidogo kimahaba. Unakuta anakula msosi kimpango wake utafikiri anakula na kaka yake. Mnatoka kidogo mnatembea unakuta anatembea na wewe utafikiri anatembea na kaka yake; yani unaweza ukamuacha nyuma kidogo au akawa mbele yako anashindwa kujiongeza kupitisha mkono wake kwenye kikwapa chako na kukushika kimahaba.

Wakati mwingine anakuona jasho linakutoka usoni anashindwa hata kukufuta kimahaba anakutazama tu utafikiri wewe ni kinyago cha mpapure. Wakati anakuaga anaondoka utafikiri anamuaga kaka yake hakupigi hata busu. Mwanamke unazungumza nae hakushiki hata ndevu zako kimahaba, mwanamke unakuwa nae hakufunyii massage wala hakukati mara moja moja kucha zako kimahaba.

Wakati mwingine unakuta umekaa nae mwaka mzima kwenye mahusiano lakini hajawahi kukwambia neno "Nakupenda"mpaka wewe uanze kumwambia kwanza.

Wanawake wengi wa siku hizi wanapenda kudekezwa, kubembelezwa na kupewa pesa ndio maana wengi utasikia wakisema "nataka mwanaume Romantic na mwenye pesa" lakini hawajiulizi je, wao ni Romantic? Au sisi wanaume hatuhitaji hayo mahaba ya wanawake?

Asili ya mwanamke ni mfariji mkuu wa mwanaume lakini siku hizi wanawake wengi wamekuwa stress kwa wanaume.

Note: Hakuna mwanaume mbahili kwa mwanamke Romantic.
 
Wote wote tuu hatuna mahaba.

Wewe mwenywe wakati unakua unawaza namna ya kumgegeda tuu. Yeye anawaza namna ya kukuingiza kwenye kuminanae za kuchunwa
Hahah!,Duh,Hiyo kali mkuu kwa hiyo ngoma Droo.
 
Yote hayo namfanyia babe wangu tukila namlisha ,namnywesha tunashea kinywaji ,namuogesha,namfuta jasho,, namkiss popote hata mbele za watu,tukitembea namshika mkono au nashika bega ,akitaka mambo muda wowowte nampatia bila hiyana,nadhan hao wanakuwa hawana hisia na wapenzi wao mi mapenzi kama ya mtu na baba ake siyatakii mie
 
Back
Top Bottom