Wanawake wengi ndio wanaolisha familia siku hizi, tatizo akina baba mbona wanafeli?

Wanashinda vijiweni kuondoa stress walizosababishiwa na wake zao kifupi wanaenda kufuata faraja...

Chunguza mtu aliyeoa ndoa ambayo haina mwaka,mda wote anashinda kwa mkewe akitoka job anarudi nyumbani kupata faraja kutoka kwa mkewe.

Sasa ikipita miaka 3 hivi akianza kupata stress kazini na nyumbani ndo anarudi kijiweni na km sio kijiweni kwa nyumba ndogo...

Maisha ya mwanaume ni stress tupu ndo mana tuna michezo mingi ya kutuburudisha na kutuondoa msongo wa mawazo kuzidi wanawake

Ikitokea amani na furaha inatoweka nyumbani basi mkombozi ni baa,kijiweni au kwa michepuko km amani ipo mda atakaoshinda huko unapungua sana..

Kuhusu kutafuta hela kijiweni kuna deal nyingi labda kama hujawahi kukaa kijiweni ila kama hauna kazi maalumu ni bora ukakae kijiweni unaweza kupata deiwaka kuliko ukishinda nyumbani na mkeo...

All in all,hamna mwanaume ana nguvu ya kuhudumia familia km mke anampa stress.Mwanaume akiwa na mahusiano mabaya na mkewe hata kazini utamuona tu alivyo na mawenge..

Hapa sijazungumzia wazee wa mwambao huko waliotega chuma ulete zao njia panda.

Tusisahau mwanaume anaoa kupata faraja na kuondolewa stress.Maisha ya mwaanume ni stress tosha .
 
Hakuna kilichonigusa hapo ndugu, labda hizi kelele nyingi kwenye majukwaa yao ndio zinakuchanganya uone ni wataftaji kuzidi wanaume. Niseme tu umepotoka ndugu yangu, yawezekana jamaa zako wa karibu inawatokea hiyo hali sasa usijumuishe kwa mji mzima.

Yaani mfano wako ni hao wanaotembeza bidhaa barabarani(na ndio data zako zimeishia hapo😂😂) we jamaa bna.
Nimekuambia tafiti hupingwa kwa tafiti, fanya tafiti. Fanya utafiti utapata majibu. Tatizo lako unadhani ni kuwa familia zote wanalishwa na wake zao. Kumbuka miaka ya nyuma ilikuwa nadra kukuta mwanamke analisha familia huku wewe unashinda unabet.
 
Wamama wana mtaji Wa ziada(pupuchi)ina lipa.

Sisi tuna bet tujaribu kuongeza kipato kwenye familia bw/bi idungude.
 
Kwetu hakuna 50/50. Hii ipo kwa wasio jitambua. Kwanza aibu kwa mwanaume kumtegemea mwanamke. Kwanza inakuwaje na mtu unaanzaje ?
Kwani mwanamke kutafuta pesa ndo kutegemewa!!?? Vipi kama Baba anatafuta na Mama anatafuta? Tatizo lenu mnapigania haki sawa lkn bado hamjawa tayari.
 
Ukitembea kila mji mkubwa au mdogo hapa Tanzania utakuta akina akina mama wapo busy kutafuta maisha, utakuta akina mama wauza uji, wauza karanga, wauza uji na mihogo wakiwa na watoto wao migongoni. Wakipata kipato wanalisha watoto na baba zao. Hii ni kasumba imeanza lini hapa Tanzania?

Akina baba wanashinda vijiweni wakipiga soga huku wakichati na masmatifone, hivi hamuoni aibu? Kwa nini msirudi kijijini?
Siku hizi?mama ni nguzo
 
Nimekuambia tafiti hupingwa kwa tafiti, fanya tafiti. Fanya utafiti utapata majibu. Tatizo lako unadhani ni kuwa familia zote wanalishwa na wake zao. Kumbuka miaka ya nyuma ilikuwa nadra kukuta mwanamke analisha familia huku wewe unashinda unabet.
"Tafiti hupingwa kwa tafiti"
Aisee ndugu yangu una safari ndefu ya kujua kufanya hizo unazoziita tafiti. Umetoa maoni na mtazamo wako baada ya kuona kinamama mtaani wanauza hizo bidhaa. Ungekua umefanya tafiti ungekuja na walau majina ya hiyo miji, walau na idadi ya hao wavivu na wachapakazi hata kwa makadilio tu. Hata sisi tunaishi hiyohiyo miji, labda watu unaokutana nao au unaoshinda na ni hao kinamama wanaofanya hizo biashara hapo lazma uone kweli ndio wanaongoza kulisha familia zao, lakini huku mtaani ndugu yangu wanaume tunapiga kazi aisee.
 
Hv mtoa mada unajua baamedi wote, malaya wote Tanzania wanaishi kwa nguvu za wanaume? Wanawake wengi kimchepuko wanategemea wanaume?Ulishajiuliza hilo? . Msikuze Mambo sana bila kuangalia kwa upana wake
 
Kwani mwanamke kutafuta pesa ndo kutegemewa!!?? Vipi kama Baba anatafuta na Mama anatafuta? Tatizo lenu mnapigania haki sawa lkn bado hamjawa tayari.
Uwe makini unapo mquote tu,siamini katika haki sawa,bali naamini katika stahiki ya haki,yaani kila apate haki yake ila si usawa wa haki wala kufanana kwa haki. Kama kuna utofauti kati ya mwenye akili na asiyekuwa na akili,vipi kuwa na usawa wa haki kati ya mwanaume na mwanamke ?

Sasa kama Mwanamke anapata kila anachokokitaka kwa mume,anaenda kutafuta pesa ili iweje na watoto au familia anaachiwa nani ?
 
Ukitembea kila mji mkubwa au mdogo hapa Tanzania utakuta akina akina mama wapo busy kutafuta maisha, utakuta akina mama wauza uji, wauza karanga, wauza uji na mihogo wakiwa na watoto wao migongoni. Wakipata kipato wanalisha watoto na baba zao. Hii ni kasumba imeanza lini hapa Tanzania?

Akina baba wanashinda vijiweni wakipiga soga huku wakichati na masmatifone, hivi hamuoni aibu? Kwa nini msirudi kijijini?
Sisi ni mwili mmoja
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom