Wanawake wengi ndio wanaolisha familia siku hizi, tatizo akina baba mbona wanafeli?

Daah hizi tafiti siku hizi aisee
Miji gani hiyo mikubwa wanawake wanachakalika halafu wanaume wanapiga umbea.

Si kweli mkuu wanaumea ndio wanaolisha familia nyingi na hao wanawake wanaochakalika sana hii miji mikubwa ni single mothers. Ndio hivyo asipochakalika mwanae atakula nini.

Mwanaume mwanaume tu aisee.
Fuatilia upate jibu
 
Ukitembea kila mji mkubwa au mdogo hapa Tanzania utakuta akina akina mama wapo busy kutafuta maisha, utakuta akina mama wauza uji, wauza karanga, wauza uji na mihogo wakiwa na watoto wao migongoni. Wakipata kipato wanalisha watoto na baba zao. Hii ni kasumba imeanza lini hapa Tanzania?

Akina baba wanashinda vijiweni wakipiga soga huku wakichati na masmatifone, hivi hamuoni aibu? Kwa nini msirudi kijijini?
Wanakula jeuri yao
 
Nahisi study yako umeifanyia mbeya,
Kina baba wa mbeya ndio wamezoea sana kulishwa na wake zao.
 
Ahaaa, najua imekugusa. Nakupa nafasi na wewe fanya alafu utapata jibu. Andaa dodoso alafu tafuta data.
Hakuna kilichonigusa hapo ndugu, labda hizi kelele nyingi kwenye majukwaa yao ndio zinakuchanganya uone ni wataftaji kuzidi wanaume. Niseme tu umepotoka ndugu yangu, yawezekana jamaa zako wa karibu inawatokea hiyo hali sasa usijumuishe kwa mji mzima.

Yaani mfano wako ni hao wanaotembeza bidhaa barabarani(na ndio data zako zimeishia hapo😂😂) we jamaa bna.
 
Yaan mwanamke mmoja akimlisha mwanaume mmoja tena kwa wkt flani tuu basi kelele mji mzima duh?
Ndivyo walivyo mkuu tuwazoee.
Bahati mbaya/nzuri wamepata wanaume wengi wanaowatetea ndio kabisaa utaonekana hujari, umetelekeza familia , una roho mbaya, hukufaa kua baba n.k n.k

Na hapo kanunua mboga siku 1 bahati mbaya hujaacha pesa ya matumizi 😂😂
 
Pamoja na yote hayo bado anataka mwanamke huyo huyo amtii na kumuheshimu,tena kama mwanamke anapokea mshahara ampe yeye aupangie matumizi...chaaa!!!
Its okay kumlea mwanaume asiye na kazi ukaendelea kumuheshimu bila kumshusha hadhi

Mbona sisi tunalea wanawake mamasikini wamekata ringi na mtaani hatutangazi?
 
Back
Top Bottom