Wanawake wengi huomba kufanyiwa upasuaji badala ya kujifungua kawaida

Operation ndio njia yenye uhakika wa uzazi salama kwa dunia ya leo

Mijini humu unasikia vifo vya wazazi tena?..

Kupush yataka mtu ambae nyonga yake si lelemama..kuzaa natural na kifo ni suala la 50/50
Sikubaliani na wewe bali nakubaliana na biology.
 
Maisha yanabadikika kwa kasi sana na mabadiliko huwa hayakwepeki. Huko tunakoenda mambo yatazidi kubadilika na watu watazidi ku opt njia ambazo ni less painful and less complicated. Ndio maana zamani hata wanaume walikua wanatahiriwa bila ganzi lakini siku hizi mambo yamebadilika!
Dunia ya kisasa. Itafika wakati hata kubeba mimba watu watasema watumbo yao yanatanuka. Tutahamia kwenye test tube babies.
 
Kwanza kabisa ni maamuzi yake na anasababu zake. Si kila mtu anataka ku experience uchungu wa uzazi.

Pili operation haisaidi kitu katika kubakiza usichana wa mtu. Kwa maana mtu anapokaribia kujifungua njia huwa ishaanza kutanuka (if at all unadhani kuzaa kawaida kunalegeza chiu). Kama matiti kulegea huwa yanalegea tokea kipindi cha mimba unless uwe hujanenepa.
 
Ukipigwa kisu mara ya kwanza mimba zitakazofuata lazima upigwe kisu tena.. tumbo litajaa makovu kama ulinisurika ajali ya ndege
Si kweli kwamba mimba ya kwanza ukipigwa kisu basi mimba zinazofuata lazima upigwe kisu tena, inategemeana na sababu iliyopelekea ukafanyiwa operation. Kama sababu iliyopelekea ukafanyiwa CS mara ya kwanza haipo kwenye mimba ya pili unaweza kujifungua kawaida ila muhimu kuwepo hospital inayoweza kufanya operation ili ikishindakana basi ufanyiwe upasuaji haraka

Ila kama mimba ya kwanza na ya pili zote ulifanyiwa operation basi ya tatu haiitaji kusubiri ni moja kwa moja operation
 
Ooh! Kwani ukizaa kwa upasuaji ndio unakuwa na tumbo kubwa au me ndio sijaelewa hapo?
Au umemaanishaje Dr
Kuzaa kwa operation kunaweza kusababisha tumbo kuwa kubwa kwa sababu misuli ya tumbo inalegea ila sio wote wanakuwa hivyo sometimes inategemeana na mwili wa mtu
 
Hivi nasikia ukizaa kwa opereation inaacha alama hapa kwenye tumbo?

Heri nije kuzaa kwa uchungu wa kupush kuliko kubakiza alama tumboni
Siku hizi hawapasui kama ile mishono ya zamani. Unapasuliwa chini kabisa (bikini line) hata ukivaa chupi hauonekani. Na baada ya muda huwa unabakia alama kwa mbali sana na kuna dawa za kupaka unaisha kabisa.
 
Siku hizi hawapasui kama ile mishono ya zamani. Unapasuliwa chini kabisa (bikini line) hata ukivaa chupi hauonekani. Na baada ya muda huwa unabakia alama kwa mbali sana na kuna dawa za kupaka unaisha kabisa.
Yes namuona sista ...unabaki kwa mbali
 
Siku hizi hawapasui kama ile mishono ya zamani. Unapasuliwa chini kabisa (bikini line) hata ukivaa chupi hauonekani. Na baada ya muda huwa unabakia alama kwa mbali sana na kuna dawa za kupaka unaisha kabisa.
joanah naamini umepata ufafanuzi wa kina, hata operation ikikukuta umeambiwa alama itakuwa ni ndogo sana usipoitaka hata hiyo ndogo utapaka dawa.
 
Cha ajabu wanaume ndio mmekazania tuzae kawaida, mnafaidi nini wenzenu wakizaa kawaida na mnapungukiwa nini wakipata mtoto kwa C-section? Mi naona siku hizi wanaume mnashupalia sana yasowahusu.

Kama mnatuonea wivu jifungueni kwa CS na nyie 😂
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom