Wanawake wengi hawajui tabia za wanaume!!!!

Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
612
Kati ya mambo ambayo wanawake wengi wanakosea au hawajui ni tabia za wanaume. Kimsingi binti au mwanamke anaposhawishiwa na mwanaume na kuwa na uhusiano wa kimapenzi, mara nyingi hupanga malengo ya mbali zaidi bila kujaribu au kutaka kujua kuwa uhusiano ulioanzishwa malengo yake ni yapi. wanawake wengi ni waoga au wanasita kuwauliza lengo la uhusianao wanaotakiwa na hatima yake itakuwa nini.

Wanawake wengi huamini kuwa uhusiano unapopamba moto, hicho ni kigezo tosha kuwa huo uhusiano mwelekeo wake ni mpaka ndoa au kuishi pamoja kama mme na mke. Wanawake wengi wamejeruhiwa wameumizwa kwa kuamini hivyo, hili ni kosa kubwa ambalo wanawake wengi hujikuta wamelifanya na huweza kuwaumiza maishani mwao mwote.

Kitu ambacho wanawake wanatakiwa wakijue fika ni kuwa wanaume waliowengi kinachowasukuma kutongoza si upendo wa dhati walionao bali ni matamanio ya mwili ndiyo humsukuma aanzishe uhusiano, ndiyo maana wanaume waliowengi wapo tayari kufanya mapenzi dakika hiyohiyo kama atakubaliwa ilimradi tu amalize matamanio yalioinuka wakati huo na baada ya hapo anaishia zake.

Kwa wanawake ambao wameshapelekwa sehemu ya faragha watakubaliana na mimi kuwa mwanaume anapomaliza shida yake kinachofuata ni kuondoka na hakuna mjadala wowote utakaotakiwa kuendelea hapo, hii ni kutokana na ukweli kuwa tamaa ya kufanya tendo la ndoa imeisha na hakuna kilichopo moyoni. kwa mwanamke ambaye sio kahaba hii ni tofauti sana kwani baada ya zoezi zima la tendo la ndoa angependa kusikia au kuonyeshwa upendo zaidi, ni wakati huo mwanamke angependa kusikia mustakabari wa uhusiano huo lakini hilo kwa wanaume wengi ni jambo wanaloliepuka na wengi hawapendi kujadili mustakabari wa uhusiano kwani kilichomsukuma sio upendo bali ni tamaa.

kutokana na wanawake kuwaamini na kujitoa kiujumla kwa wapenzi kwa kuamini kuwa huenda ndio mwanzo wa maisha ya mme na mke wengi wamejikuta wakiingia katika matatizo na hasara kubwa ya kimaisha. wanawake wengi wamepoteza mwelekeo na kujikuta wakitaabika kutokana na kipengere hiki cha kuamini mambo ambayo wapenzi wao hawayaamini wala kuyachukulia tahadhari.

Mimba nyingi zisizotarajiwa zimepatikana kwa kosa hili la wanawake wengi kutojua tabia za wanaume hivyo kujikuta wamekwama. Ugonjwa wa UKIMWI ambao ni tishio umekuwa ukienea kwa kasi kubwa ambapo moja ya sababu zinazosababisha ni hili la wanawake kuwaamini kupita kiasi wanaume hata kukubali kufanya mapenzi bila kutumia kondom wakihadaika kuwa uhusiano uliopo ni wa kudumu hivyo hakuna sababu za kutoaminiana.

Pamoja na hali halisi ya maisha, ni lazima wanawake wasiwe wavivu kutaka kujua tabia za wanaume na kuchukua tahadhari, vinginevyo mahangaiko, kujeruhiwa, kukosa mwelekeo wa maisha, kuambukizwa magojwa ya hatari kama UKIMWI hayo yote yatakuwa mwiba kwao.
 
cheusimangala

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
2,585
492

thanks Anold.
hapo nilipo-underline,mwanamke aliyeko makini atauliza hilo swali lkn anaweza kudanganywa.
Hata hivyo umeongelea jinsi ambavyo wanaume wakishapata tendo la ndoa wanasepa sbb hawakuwa na mapenzi ya dhati bali tamaa.
lkn sio wanaume wote wako hivyo,kwa vile unaongelea juu ya tabia za wanaume,ungeelezea pia jinsi gani ya kuzijua tabia za mwanaume anayekupenda kwa dhati,ambaye hatakimbia baada ya tendo.
 
Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
612
Nakubaliana na wewe kabisa ''cheusimangala'' kuwa sio wanaume wote wako hivyo, ila wengi wana tabia hiyo. Nitaeleza namna ya kukabiliana na hilo baadae kidogo tuendelee kutembelea JF.
 
MADAM T

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,036
2,204
Kitu ambacho wanawake wanatakiwa wakijue fika ni kuwa wanaume waliowengi kinachowasukuma kutongoza si upendo wa dhati walionao bali ni matamanio ya mwili ndiyo humsukuma aanzishe uhusiano, ndiyo maana wanaume waliowengi wapo tayari kufanya mapenzi dakika hiyohiyo kama atakubaliwa ilimradi tu amalize matamanio yalioinuka wakati huo na baada ya hapo anaishia zake.

Kwa wanawake ambao wameshapelekwa sehemu ya faragha watakubaliana na mimi kuwa mwanaume anapomaliza shida yake kinachofuata ni kuondoka na hakuna mjadala wowote utakaotakiwa kuendelea hapo, hii ni kutokana na ukweli kuwa tamaa ya kufanya tendo la ndoa imeisha na hakuna kilichopo moyoni. kwa mwanamke ambaye sio kahaba hii ni tofauti sana kwani baada ya zoezi zima la tendo la ndoa angependa kusikia au kuonyeshwa upendo zaidi, ni wakati huo mwanamke angependa kusikia mustakabari wa uhusiano huo lakini hilo kwa wanaume wengi ni jambo wanaloliepuka na wengi hawapendi kujadili mustakabari wa uhusiano kwani kilichomsukuma sio upendo bali ni tamaa.
Anoo, hapo umeongea kweli tupu, ila sasa tutawezezaje kupima kwamba hapa ni tamaa na hapa ni upendo wa kweli, maana naona methods ni zile zile, help!:A S-rose:
 
Somoe

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
754
277
Hivi kuna mwanamke hasie jua kuwa wanaume wanachotaka? Mie nazani wanawake wengi ukubali kwa tamanio yao ya kimwili au kipesa. Au wanatatizo la kupata mwanaume. Mie nazani wanawake wanajua kuwa wanaume kudanganya wanawake ndio kazi yao, ila wanajaribu kukubali hovyo ili waone matokeo.
 
Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
612
Nimekupata MADAM T. ni kweli medhods ni zilezile na mitego ni mingi sana ambayo bila kuwa mwangalifu (sana) ni vigumu kugundua. Ila utakubaliana na mimi kuwa UMAKINI katika jambo lolote kuna uwezekano mkubwa wa kuleta matokeo chanya.

Hebu tafakari mambo haya.

1. Ni wasichana wangapi ambao wanamuda wa kutaka kujua kwa kina undani wa mpenzi
wake kabla ya kufanya tendo la ndoa?

2. Kama atabahatika kujua undani wa mpenzi wake je yupo tayari kumuuliza nia na lengo la
uhusiano anaotakiwa wauanze? anania ya kuoa au ni urafiki wa kawaida? (kwa nchi za
ulaya wengi wanajitahidi kujua aina na uhusiano uliopo jambo ambalo linawasaidia sana)
(angalizo): kama utamuuliza mpenzi mtarajiwa swali hili (nini malengo ya kutaka uhusiano kwako ni urafiki au ni kutaka kuoana) ukiona anaanza kupiga chenga kwa sababu yeyote be careful.

3. Kukubali kufanya tendo la ndoa kwa sababu zozote zile ni kosa baya ambalo linafanywa
na wanawake. wanawake wengi hudhani kuwa kwa kufanya tendo la ndoa ndiyo njia ya
kumuonyesha mpenzi wake kuwa anampenda. (inawezekana) ila ukishajirahisi ujue hilo
tu linaweza kudhorotesha/kuchelewesha hatma ya huo uhusiano. Inawezekana
unamapungufu fulani ambayo kwa mwonekano wa nje sio rahisi kugundulika sasa
ukishajitoa na kujulikana kila eneo hilo nalo ni hatari kwako.

#### endelea kujiunga na JF. nitaweka mambo mengine muhimu!!!! aidha utapata kujua tofauti ya UPENDO na KUTAMANI
 
Baba Mtu

JF-Expert Member
Aug 28, 2008
871
165
Anoo, hapo umeongea kweli tupu, ila sasa tutawezezaje kupima kwamba hapa ni tamaa na hapa ni upendo wa kweli, maana naona methods ni zile zile, help!:A S-rose:

Mwambie apeleke barua ya posa nyumbani na hakuna kula uroda mpaka ndoa. Mkweli utamjua na muongo utamjua, mara nyingi muongo atatoka nduki. Au mwambie twende tukapime ukimwi afu uone kama atakubali.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom