Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Ninaposema wanawake wazuri nina maana pana sana na yenye utata kwa kiasi kikubwa kwa sababu uzuri kama dhana dhahania inachanganya sana. Je wanawake wazuri ni wenye sifa zipi na hasa ni wazuri kwa akina nani na sio kwa wengine? Lakini kwa kusudi la kufikisha ujumbe huu naweza kusema wanawake wazuri ni wale ambao watu wengi wakiwatazama hukubali kwamba wana maumbile au sura ambazo zinakubaliwa na maoni yao au maana ya uzuri kwa viwango ambavyo akili zao zinaamini.
Kwa kuwa wanaume wa dunia hii wamelelewa na kujengewa dhana kuwa mwanamke ana kazi kubwa moja tu ambayo ni kumstarehesha mwanaume, humtazama mwanamke kama wanavyo tazama ua au mapambo mengine na huenda mbali zaidi na kumtazama mwanamke kama mashine ya kuwakatia kiu ya tamaa ya miili yao. Inakuaje?
Wanaume wengi wanaamini kwamba wanawake wengi wazuri wa sura na maumbile (labda) huwa wana matatizo ya kuwaringia wanaume. Kuwaringia wanaume kuna maana ya mwanamke kutokua tayari kuwa mtumwa wake na kifaa chake cha kukatia kiu ya kimwili. Kwa imani hiyo wanaume huwa waangalifu sana katika kushughulika na wanawake wazuri kwani huogopa kwamba watakua wakiteleza pale watakapokuwa wakitaka kuwabana.
Inawezekana kabisa wanawake wazuri hawana tatizo hilo. Bali wanaume ndivyo wanavyo amini. Kuamini ndiko kunapopelekea waogope kuwaoa. Wanaume huwa wanasema mwanamke kama yule hafai kuoa labda kuchezea tu kwani ukimwoa atakusumbua sana Kauli kama hii ina maana kwamba mwanamke mzuri ukimwoa atataka kuwa na kauli kwa sababu ni mzuri nawe itabidi ukubali hili.
Lakini kwa upande wa pili wanawake wazuri nao wanapogundua kwamba ni wazuri huku wakiwa wanaamini kwamba uzuri wao ni silaha ya kuwapigia wanaume kamwe hawawezi kuolewa au wanaweza kujikuta ndoa zao hazidumu. Hii ni kwa sababu kwa kuamini kwao hivyo hufanya mambo kwa kiwango cha kupindukia. Huwatenda wanaume yasiyopendeza kwa kuamini kwamba kwa sababu ni wazuri hawawezi kuachwa na hata wakiachwa wataolewa baada ya mda mfupi.
Bila shaka umeshawahi kusikia hata wanawake wenyewe wakisema flani anautumia uzuri wake vilivyo anawaburuza kweli wanaume Hii ina maana kwamba uzuri wao ni silaha nzuri ya kuwashikisha adabu wanaume.