Wanawake watakiwa kupigia kura wanawake wenzao

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Wanawake watakiwa kupigia kura wanawake wenzao

Baadhi ya Wanawake nchini wamekuwa ni watu wasiokuwa na usubutu katika kupambana na wanaume katika nyanja mbalimbali hususani ni katika nafasi za kugombea nafasi za uongozi ikiwemo kugombea ubunge.

Tatizo hili limesababisha, wanawake wengi kushindwa kujiamini na badala yake wamewapa nafasi kubwa wanaume kuzidi kushika nafasi hizo.

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za Wanawake na Watoto (Kivulini) Yassin Ally anasema umefika wakati sasa kwa wanawake kuamka na kugombea nafasi za udiwani na ubunge.

Anasema ni vizuri wanawake wakajitokeza kwa wingi kugombea katika ngazi mbalimbali ili kuleta usawa.

Yassin anasema, endapo wakajitokeza kugombea na kuchaguliwa kwenye nafasi hizo itasaidia kuleta usawa kwenye maamuzi yanayofanyika kwenye ngazi za serikali za vijiji, halmashauri, bunge na nyadhifa mbalimbali za uteuzi.

"Tukichukua kwenye takwimu asilimia 60 ya wapiga kura ni wanawake na wao ndio wanaongoza hata kwa kujiandikisha na kujitokeza kwa wingi kuliko wanaume.

"Tumeona wanawake wengi wanaoamini wanaoshika majimbo, kata na hata walioteuliwa kwenye nyadhifa mbambali wanafanya vizuri," alisema Yassin.

Pia Yassin anasema, kutokana na wanawake ndio wanaongoza kwa kupiga kura inapaswa kuona sasa mwamko wa wanawake wakiwapigia kura wanawake wenzao pindi wanapogombea nafasi hizo.

Yassin akagusia suala la viti maalumu kwa wanawake nchini, akasema sambamba kwa kuendelea kwa viti maalumu lakini wanawake wapanaswa kuamka na kugombea nafasi hizo.

Anasema kwamba uwezo kielimu, uwezo wa kimaamuzi na kiuchumi, unahitaji wanawake watawale uchumi na watawale maamuzi ndipo kizazi cha usawa na maendeleo ya sasa na ya baadae kiweze kupatikana.

Akisoma risala la wanawake wa Misungwi kwa mgeni Rasmi ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Misungwi,zote Juma Sweda, Telesia Mlaku anasema imefika wakati wanawake kuwezeshwa kiutamaduni na kisiasa ili wawe na uwezo wa kujitegemea na kuhudumia jamii.

Kaimu Mkurugenzi wa Misungwi, anasema halmashauri hiyo imezidi kutekeleza sera mbalimbali ikiwemo sera ya maendeleo duniani pia utekelezaji sheria ya fedha za serikali za mitaa na utekelezaji wa mikataba ya kimataifa inayotoa msukumo wa kutambua nafasi ya mwanamke katika kumjengea uwezo katika kutekeleza usawa.

Anasema mila na desturi za kitanzania ziliwachelewesha wanawake, na kwamba sasa imefika mwisho na kilichopo ni kuungana kwa wanawake na wanaume ili kwenda kwenye 50/50 ili kufikia malengo husika.

Jana iliadhimishwa siku ya wanawake duniani ikiwa ni maadhimisho ya miaka 25 ya wanawake, kiwilaya ya Misungwi yalifanyika viwanja vya shule ya sekondari Sanjo na kitaifa yalifanyika mkoani Simiyu

....
 
March 8, 2020
Dar-Es-Salaam, Tanzania

Mkutano wa Baraza la Wanawake CHADEMA

Jana pia mkutano wa Baraza la Wanawake la CHADEMA, yaani BAWACHA walionesha uwezo wao wa kushiriki kisawasawa katika siasa za Tanzania kupitia chama pendwa cha siasa cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA. Siku ya mwanamke duniani inatambua Demokrasia ndiyo nguzo ya maendeleo ya ngazi zote kuanzia taifa, chama na ngazi ya familia ambayo pia inahusu mwanamke.



Source: Chadema media TV
 
March 8, 2020
Siku ya Wanawake Duniani Machi 8 Kila Mwaka :ni siku ya kutathimini maendeleo ya wanawake!

Kila tarehe 8 Machi ya kila mwaka ni siku ya wanwake duniani.Siku hii inataka kukumusha matokeo chanya ya kisiasa,kijamii, kiuchumi waliyofikia wanawake.Lakini licha ya jitihada na msimamo wao bado changamoto ni kubwa katika mantiki za usawa.Tuifahamu siku hii ilianza lini na sababu zake ni zipi kuwa na mshindo mkuu namna hii.


Kila tarehe 8 Machi ya kila mwaka ni Siku ya wanawake duniani, ambapo siku hii inataka kukumbuka na kutafakari juu ya matokeo ya kisiasa, kijamii, kiuchumi waliyofikia wanawake na msimamo wao imara katika ngazi ya kijamii kwa ujumla. Je ni kwa nini zaidi ya karne sasa watu duniani wamekuwa wakisherehekea siku hii? Siku ya wanawake duniani ilianza kutokana na jitihada za wanawake 15,000 mwaka 1908 walipoandamana mjini New York Marekani wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, ujira wa kuridhisha na haki ya kupiga kura. Kilikuwa ni chama cha kisoshalisti cha Amerika kilichotangaza kuwa ni siku ya kwanza ya kitaifa ya wanawake, mwaka mmoja baadaye. Wazo la kuwa siku ya kimataifa lilianzishwa na mwanamke kwa jina la Clara Zetkin. Yeye alipendekeza wazo hilo mwaka 1910 katika mkutano wa kimataifa wa wafanyakazi wanawake huko Copenhagen Denmark.
Wanawake 100 kutoka nchi 17
Kulikuwa na wanawake 100 hapo kutoka nchi 17 na wakakubaliana kwa pamoja. Kwa mara ya kwanza ilisheherekewa mwaka 1911, Austria, Denmark, Ujerumani na Switzerland. Sherehe ya miaka 100 ilifanyika kunako mwaka 2011. Suala hilo likawa rasmi mwaka 1975 baada ya Umoja wa Mataifa kuanza kusherehekea siku hiyo na baadaye kubuni kauli mbiu. Ya kwanza mwaka 1996 ilikuwa “furahia yaliyopita, panga kwa ajili ya baadaye”. Kwa hakika siku ya kimataifa ya wanawake duniani imekuwa siku ya kutathimini maendeleo ya wanawake katika jamii katika nyanja za siasa na uchumi, kulikuwa pia na migomo na maandamano yaliyoratibiwa kwa ajili ya kusisitiza masuala ya usawa.
Tarehe 8 mwezi Machi
Wazo la Clara Zetkin la Siku ya kimataifa ya wanawake duniani halikuwa na tarehe maalum na haikuwa rasmi mpaka kipindi cha vita ya mwaka 1917 wakati wanawake wa kirusi walipodai Amani na kufanyia kazi tatizo la upungufu wa chakula (Waliimba Amani na Mkate). Siku nne za mgomo, zilifanya watawala wa Urusi kuwapa wanawake haki ya kupiga kura. Tarehe ambayo mgomo ulianza ulikuwa kwenye kalenda ya Julian, ambayo ilikuwa ikitumika Urusi wakati huo, ilikuwa siku ya Jumapili tarehe 23 Mwezi Februari. Siku hii katika kalenda ya Gregoriana ilikuwa tarehe 8 mwezi Machi na ndiyo siku hii inayosherehekewa kila mwaka.
Chereko za Sherehe za siku hii,kupeana maua, maandamano ya kudai haki na usawa
Siku ya kimataifa ya wanawake ni siku ya mapumziko katika baadhi ya nchi nyingi ikiwemo Urusi, ambapo mauzo ya maua huwa mara mbili zaidi wakati wa siku tatu au nne kabla ya siku yenyewe, ambapo wanaume na wanawake huwapa maua wapendwa wao wa kike na wafanyakazi wenzao. Nchini China, wanawake wengi hufanya kazi nusu siku tarehe 8 Machi, kama ilivyoshauriwa na Baraza la nchi hiyo ingawa waajiri si mara zote wanatekeleza utamaduni huo. Nchini Italia, siku ya kimataifa ya wanawake au “La Fiesta della Donna” inasheherekewa kwa kupeana maua chanzo cha utamaduni huu hakifahamiki lakini inaaminika ilianzia Roma baada ya vita ya pili ya dunia. Nchini Marekani, Mwezi Machi ni mwezi wa historia kwa wanawake. Rais hutambua kila mwaka na kuthamini mafanikio ya wanawake wa Marekani. Lakini na zaidi sasa wanawake wengi kila mwaka mamilioni ya waandamanaji kila nchi duniani kote ushuka barabarani huki wakipaza sauti kuhusu haki za wanawake.
Kumbuka kuwa Siku ya wanaume duniani ipo japokuwa bado haijatambuliwa na Umoja wa Mataifa
Hata hivyo tunakisikia siku ya wanawake kuvuma sana na wengi wa wanaume hawatambui kuwa hata wao wana siku ya wanaume duniani. Siku hii inaadhimishwa kila tarehe 19 Novemba, lakini maadhimisho haya yameanza miaka ya hivi karibuni , kwani yalianza tangu miaka ya 90 na bado haijatambuliwa rasimi na Umoja wa Mataifa. Watu huiadhimisha katika nchi zaidi ya 60. Lengo la siku hii ni kutazama afya za wanaume na wavulana, kuimarisha mahusiano ya jinsia, usawa wa jinsia na kutathimini jinsia ya kiume kama mfano watu wa kuigwa.

Makala hii kwa hisani kubwa ya :
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
source: Siku ya wanawake duniani:ni siku ya kutathimini maendeleo ya wanawake! - | Vatican News
 
Machi 8, 2020

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA : TAMKO LAKE SIKU YA KUADHIMISHA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI

Tunapoadhimisha kumbukumbu ya siku ya Mwanamke Duniani hii leo Machi 8, 2020 ikiwa ni miaka 25 tangu wanawake kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wakutane jijini Beijing, China kujadili maendeleo ya wanawake,Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inapenda kuungana na Watanzania wote katika kusherehekea maadhimisho haya ambayo kimsingi yanatoa fursa kwa wanawake kufanya marejeo ya hatua mbalimbali zilizofikiwa katika kuboresha mustakabali wa wanawake nchini.

Tume inatambua kuwa, Tanzania kama nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa imeridhia mikataba ya haki za binadamu kuhusu wanawake ikiwemo makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa beijing mwaka 1995.

Miongoni mwa maeneo ambayo Serikali imeyafanyia kazi kwa ufanisi mkubwa wakati tunaadhimisha siku ya mwanamke mwaka huu ni pamoja na usawa wa kijinsia katika kushiriki kwenye kufanya maamuzi, upatikanaji wa huduma za afya kwa mama na mtoto, kukemea ukatili wa kijinsia kwa mtoto wa kike na kuwajengea mifumo ya kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Kama kaulimbiu ya mwaka huu inavyosema “kizazi cha usawa kwa maendeleo ya Tanzania kwa sasa na baadae”. Serikali imepiga hatua kubwa na mpaka sasa tunashuhudia kuongezeka kwa ushiriki wa wanawake katika ngazi mbalimbali za maamuzi.

Tume inatumia fursa hii kupongeza kwa dhati jitihada za Serikali katika kujenga mifumo sahihi kwa mwanamke kujiletea maendeleo yake.

Aidha, katika kuyapa kipaumbele masuala ya wanawake Tume inaendelea kutekeleza Mpango Kazi wake wa Miaka Mitano (2018/ 2023) ambapo moja ya malengo yake ni kuhakikisha wanawake wanaweza kufikia mifumo ya kupata haki kwa urahisi zaidi.

Licha ya juhudi za Serikali na Wadau za kahakikisha haki za wanawake zinapatikana kwa usawa na watu wengine, bado kuna changamoto ya ukatili kwa wanawake na kutokuwateuwa kwa wingi kugombea nafasi za kisiasa. Hivyo, Tume inatoa mapendekezo kwa Serikali, Wadau na jamii kwa ujumla kama ifuatavyo;

Tume inaiomba Serikali iendelee kuweka mazingira mazuri kwa wanawake kwa kuwaongezea nafasi zaidi katika ngazi za maamuzi ili kuweza kufikia maendeleo ya kweli ifikapo mwaka 2025.

Tume inazishauri mamlaka za umma na binafsi kuongeza juhudi za kuelimisha jamii kuhusu kuachana na mila zote potofu dhidi ya mwanamke ili kumpa fursa nzuri ya kuweza kujiletea maendeleo yao wenyewe.

Tume inashauri vyombo vinavyosimamia upatikanaji wa haki hususan Mahakama na jeshi la Polisi kuimarisha na kuongeza kasi ya ushughulikiaji wa mashauri yanawayohusu wanawake.

Tume inaishauri Serikali pamoja na wadau wa haki za binadamu kupitia sheria zote zinazowagusa wanawake ikiwemo sheria za kimila kwa madhumuni ya kuzifuta, au kuzirekebisha ili ziendane na Katiba ya Nchi, Azimio la Beijing na mikataba mbalimbali ya kimataifa na ya kikanda.

Tume inawatakia Wanawake Maadhimisho mema.

Imetolewa na:


(SIGNED)

Jaji (Mst.) Mathew P. M. Mwaimu
MWENYEKITI

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Machi 8, 2020

source:
Tamko la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Machi 8 , 2020
 
Nimeishia hapo tu niliposoma kwamba Mkurugenzi mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za Wanawake na Watoto (Kivulini) ni Yassin Ally ambae pia sio mwanamke.
Hii inatupa picha na tafasiri pana hasa sisi wakina Thomaso.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
March 7, 2020

Katibu Mkuu CHADEMA awataka wanawake wapige kelele kudai Tume Huru ya Uchaguzi :

Katibu Mkuu alisema hayo alipokutana na kina mama ktk mkutano wa kuwawezesha kuhusu masuala ya uongozi, siasa na hali ya kisiasa nchini toka 2015 n.k ili waweze kushiriki siasa kusimamia chama na pia kuwania nafasi za kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi



Source: Chadema Media TV
 
Back
Top Bottom