Wanawake wasomi wengi hukataa fursa bila kujua

monferee

Member
Aug 4, 2019
13
17
Habari wana JF,

Wanawake baadhi (siyo wote) wasomi wa vyuo vikuu hasa ngazi ya shahada (degree) ni waoga sana. Uoga usio na sababu za msingi.

Siku hizi kazi zinazotangazwa rasmi ni chache sana hivyo kazi nyingi hupatikana kupitia kufahamiana na watu mbalimbali.
Watu wanaojua tabia zako na kuanza kukuamini kukupa majukumu fulani.

Mara nyingi sekta binafsi hawatangazi nafasi za kazi kwa hofu ya kuajiri mtu mwenye ufaulu mzuri lakini asiweze kuonesha uwezo halisi kazini, hivyo hutumia watu mfano, wahadhiri wa vyuo vikuu na waajiri wengine wazoefu kuwatafutia vijana potential Kuja kujaza nafasi hizo.

Tatizo ni kwa hawa wasomi wanawake, baadhi yao wanapounganishwa na fursa hizo hudhani na pengine huhofia kuhitajika kimapenzi hivyo hawaoneshi ushirikiano isipokuwa wachache tu.

Nasema ni uoga usio na sababu kwakuwa, mwanamke ana uhuru wa kuamua kuhusu maisha yake ikiwemo mahusiano. Hata ikitokea ameona dalili za kuhitajika kimapenzi atakataa kwa msimamo thabiti kama anavyowakataa wengine na SIYO KUDHANI kila mtu anayemjia katika maisha yake anamhitaji kimapenzi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom