Wanawake Wasioolewa Nitawapa Mume' - Mgombea Urais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake Wasioolewa Nitawapa Mume' - Mgombea Urais

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 21, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mgombea wa urais nchini Kazakhstan amekuja na kampeni ya urais ya aina yake duniani kwa kutamba kuwa atawapatia waume wanawake wote wa nchini humo ambao hawajaolewa.
  Mgombea urais wa nchini Kazakhstan, Amantay Asilbek amewaahidi wanawake nchini humo kuwa atahakikisha wanawake wote ambao hawajaolewa wanapata waume.

  "Nchini Kazakhstan kuna wanawake wengi ambao hawajaolewa, hili ni janga la taifa kwani tunawapoteza akina mama wa baadae", alisema Asilbek wakati wa mahojiano na gazeti moja nchini humo.

  Asilbek aliendelea kusema kuwa tatizo la wanawake wengi kukosa waume litapatiwa ufumbuzi kwa kuwaruhusu wanaume kuwaoa wanawake zaidi ya mmoja.

  Asilbek mwenye umri wa miaka 70 alitamba kuwa hata yeye mwenyewe pia amefikiria kuongeza mke wa pili.

  Pamoja na kusapoti wanaume kuoa wanawake wengi, Asilbek alionyesha wazi hataki kumuudhi mwandani wake kwa kumletea mwenzake kwa kusema"
  "Wasichana wengi wamekuwa wakija nyumbani kwangu wakiwa na ndoto za kuwa wake zangu, lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kuwa na kiwango cha ubora kama cha mke wangu", alitamba Asilbek.

  Asilbek alisema kuwa atapigania kuruhusiwa kwa wanaume kuoa wanawake wengi ili kuondoa tatizo la wanawake wengi kubaki majumbani mwa wazazi wao wakiwa wamekosa wanaume wa kuwaoa.

  Asilbek, alijaribu kugombea nafasi ya kuwania urais mwaka 1998 lakini aliikosa nafasi hiyo. Alikubaliwa kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2005 lakini aliangushwa vibaya.

  Safari hii Asilbek amejitosa tena kugombea urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 3 mwezi wa nne mwaka huu.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kweli hiyo ni kampeni ya aina yake!
   
 3. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huyu jamaa kiboko, sasa angeonesha kwa yeye kuongeza kwanza!!!!
   
 4. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hii hii na uhakika watu wa nchini kwake especially wanawake hawatadanganyika kirahisi hivyo....angesema anaenda nchi nyengine na kuwaleta wanaume kwenye malori wawaoe labda angepata kura LOLS!:mullet::mullet:
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Inaonekana kuna shortage ya wanaume kwenye hiyo nchi!
   
 6. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hivi kwa bongo idadi kubwa ni wanawake au wanaume?na nchi ikiwa na wanawake wengi hivyo ina maana hata vitendo vya ubakaji havitakuwepo!
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Afanye mpango wa kukaribisha wavulana wa kichina. Huko China kuna wavulana ni wengi kuliko wasichana, kwa hiyo wasichana ni nyodo kweli
   
 8. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Aiseee!!!
   
 9. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kampeni ya aina yake,kwa hiyo atatunga sheria ya kulazimisha wanaume kuwa na mke zaidi ya mmoja au ? akapumzike tuu na yeye miaka 70 anataka uraisi?
   
 10. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kutokana na hili nimegundua kwamba Uisilamu una majibu ya matatizo mengi ya dunia itafika wakati wanawake ndio wataandamana mitaani kutaka wanaume waowe mke zaidi ya mmoja najuwa kwa sasa wanalipinga hilo ila ipo siku watalikubali na kuhusu china kuwa wanawake ni wengi kuliko wanaume ni kweli lakini hilo linasababishwa na wachina wenyewe kwa vile hawataki watoto wa kike na wanatowa sana mimba wakingundua mimba ni ya mtoto wa kike
   
 11. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,851
  Likes Received: 1,336
  Trophy Points: 280

  Dunia nzima kuna shortage ya wanaume, kuna wanawake wengi duniani kuliko wanaume.

  Dawa ya matatizo haya ni kuoa zaidi ya mke mmoja kwa wenye uwezo tu.

  Ama kweli Dini ya kiislamu haijakosea.
   
 12. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  We unao wangapi?
   
Loading...