MEING'ATI
JF-Expert Member
- Feb 17, 2014
- 1,212
- 1,009
Wanawake wengi maarufu kama Bongo movie,na wabongo flaver kuolewa kwao na kulea familia na mume ni kazi sana. Kweli huwezi faidi zote upate umaarufu na ufaidi ndoa ni vitu viwili haviendani. Wengi wao wanabaki tu kuimbiwa na kuimbwa kama ngombe wa kimasai ila ukweli life yao inaishia kuchezewa na kuzalishwa. Hili tatizo sijui kwa nini linawakumba sana watu maarufu. Na hata baadhi ya wanaume wamebakia tu kuimba mapenzi ila ukweli maisha yao ya halisi hio kitu mapenzi hawana ila wamebaki porojo za kukariri tu. Hii maisha kweli ina makubwa ya kujifunza. Kitu mapenzi iko kwa watu ambao hata jamii haiwajui hata. Uzeeni ukiwakuta watakumwagia hazina lukuki ya hekima. Hawa wenzetu kwa uhalisia wamejaa umaigizo na mateso ya majuto baadae.