Wanawake wapigwa na kudhalilishwa, watishiwa kuuwawa na wamiliki wa yard ya kuvuta magari jijini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake wapigwa na kudhalilishwa, watishiwa kuuwawa na wamiliki wa yard ya kuvuta magari jijini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by C.T.U, Feb 15, 2012.

 1. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  watanzania kadhaa leo wakiwemo wanawake na akina mama wamepigwa , kudhalilishwa , kuibiwa pesa na kutishiwa kuuwawa na wamiliki wa yard ya kampuni ya Mwamkinga Auction Mart,Yard hiyo ipo nyuma ya BP (PUMA) station Sinza Kijiweni yenye kazi ya kuvuta magari yanayopaki vibaya jijini
  mtiti ulianza pale watu hao walipokuwa wamepaki vibaya magari ndipo wafanyakazi hao wakaja kufunga na kuvuta magari hayo wale kina dada wakaanza kuyafuatilia kwa nyuma mpaka kwenye yadi yao walipofika kwenye yard yao wale watu ambao magari yao yalikuwa yamekokotwa walianza kupokea kipondo kutoka kwa wamiliki na wafanyakazi wa kampuni sababu ni kisa kwa kuwa wale kina dada walilamakika kuwa magari yao yamekwanguliwa katika zoezi hilo la kukokota magari
  wale wadada walipigwa, kushikwa matiti, na kutishiwa kuuwawa na mmiliki wa kampuni hiyo kwani alitoa bastola...
  Kuna mpiga picha mmoja ambaye alijaribu kupiga picha alipigwa mpaka akavimba mdomo na kamera yake haijui ilipo
  wale kina dada walipigwa mpaka wakashikwa matiti kuna mmoja kapoteza dola 30000
  vile vile inasemekana kuwa wale wadada walivyofika kwenye yard hiyo walikuta kuna watu wengine wanapokea kipondo kutoka kwa wamiliki na wafanyakazi
  hii inamaana kuwa hao wamiliki wa hiyo yard ni kazi yao kupiga watu na kuwaibia na kuwadhalilisha
  hivi serikali inajua hili?
  Inawezekana ni kampuni ya mtu mkubwa ndio maana jamaa ana jiamini kiasi hiki?
  Inawezekana jamaa anajuana na wakubwa ndio maana anajiamini kiasi hiki?
  Nashindwa kuelewa hapa tatizo ni nini mimi imeniuma na kunikera sana
  hivi watu walio juu ya sheria kumbe bado wapo??
  Je na wewe imeshakutokea hali kama hii??
  Huu ndio style ya kufanya biashara jamani watanzania??
  Naomba tulijadili na tulikemee hili.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,861
  Trophy Points: 280
  Nimesikia dada mmoja akilalamika redioni..nimeumia sana sasa sijui tatizo ni nini..mtu anaonewa akiwa kwenye nchi yake. sasa sijui wanataka tuhamie wapi? marekani au nchi za europe zenye ubaguzi wa ngozi?
  Sijaelewa kabisa kwa nini hili jambo limeachiwa hadi limefikia hii hatua. kuna mwandishi mmoja naye walimnyan'ganya kamera wakampiga sana tu na wakamuonyeshea bastola. sijui tunaekea wapi.
  Naapa mimi nikukutana na haya masahibu naenda kuvaa bomu nalipua hiyo yadi yote, huu ni ujinga mtu aonewe kwenye nchi za watu hadi nyumbani nako tena kuna uonevu. hawa jamaa nisikutane nao au wasije wakanigusa siku.
   
 3. u

  ureni JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Jamani taratibu tupunguze hasira,mie ningependa kusikiliza pia kwa upande wa pili wa mwenye yard alete utetezi wake hapa ili haki iweze kutendeka.Inawezekana hao wanawake waliochukuliwa magari wamemkata kibao mwenye yard akaamua atumie resource zake kujitetea kwa hiyo busara ni kusikiliza pande zote mbili ndio tutoe maamuzi yaliyo sahihi.
   
 4. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  This is bongo land ukiwa na hela au ukijuana na wakubwa basi ujue upo juu ya sheria
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,861
  Trophy Points: 280
  ngoja nijaribu kuandika kile yule dada alichokuwa anaeleza redioani..japo sikumbuki maeneo gani ya ya dsm.
  huyo dada alikuwa ame park gari yake . wakaja vijana wakaipiga jeki wakamwambia kuwa amepaki sehemu ambayo sio na wanaibeba akawauliza mnaipeleka wapi? hakuwajibu..wakaondoka na ile gari ya yule dada..yule dada kuona vile akachukua boda boda ya kukodi ili kufuatilia kuwa gari yake inapelekwa wapi.
  Akawafuatilia ila walipofika katikati ya safari kuna kijana mmoja akashuka kutoka kwenye ile breakdown kitu kama hicho akarudi nyuma akailegeza ile gari ya yule dada na wakaendelea na safari..... baada ya muda ile gari ya yule dada ikadondoka ikadumbukia kwenye mtaro ... yule dada akaona ni bora awafuatilie mpaka ajue kuwa ofisi zao ziko wapi..akawafuatilia mpaka kwenye yadi yao...
  kufika kule yule dada akawauliza kuhusu gari yake na vitu kama hivyo wakamshushia kipigo na kuchukua baadhi ya vitu yake ,simu,pesa etc
  wakamshika na sehemu zingine ambazo hazitakiwi kushikwa shikwa na kial mtu
  ....sasa hapa naogopa kuwa kama hii yadi ni ya mkubwa au ina mkono wa mkubwa kwenye nchi yetu hii ambayo haina sheria huyu dada wa watu hatapata haki yake ....ndio maana mimi nikasema kuwa ikinitokea mimi kitu kama hii ..lazima nisambaratishe hiyo yadi hata kama itachukua mda gani ...ungemsikia huyo dada na jamaa mmoja ambaye alidai kuwa ni mwandishi wa habari ungekubaliana na mimi.
   
 6. rushanju

  rushanju JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 2,342
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  Pia kupark hovyo ni kosa. Upande mwingine kuvuta magari nalo ni tatizo maana hata wezi wanaweza kutumia mbinu hiyo
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,861
  Trophy Points: 280
  kupark ovyo ni kosa kila mtu anajua na sheria za Tanzania ndio zinaruhusu kupika wapi na kuharibu magari yao kisa wamepark ovyo. jamaa wanashindwaje kufanya kazi kiuzalendo zaidi
   
 8. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  hii habari niliisikia na dada aliyefanyiwa kitendo hiki kupitia clouds fm jahazi. Nilisikitika sana,gari latupwa mtaroni,watishiwa bastola,wapigwa. Jamani tanzania tumefikia hapa kisa parking za jiji ambazo hazipo hata mbunge zungu amelaani tukio hilo. Ni mara ya pili mara ya kwanza ilikuwa pale mwenge wili zimepita. maalumu
   
 9. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  ni kampuni gani iliofanya huo ******?wekeni jina lake hapa jamani
  kama huyo dada aliitaja,kwa nini nyie mtupe habari nusunusu,ileteni hapa,
   
 10. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Serikali imetafuta solution ya kesi mahakamani, makosa madogo kama wrong parking ni kipondo. Hii nchi sijui inaenda wapi, kuko kama hakuna mwenye nayo! Sasa sinza kulivyobanana hayo magari watu watapaki wapi?
   
 11. e

  evoddy JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huo ni udhalilishaji mkubwa kwa watanzania ,inafaa watu watambue kuwa chini ya serikali inayoongozwa na CCM hakuna haki.

  HAKIKISHA HUPOTEZI HAKI YAKO 2015 KUWARUDISHA SERIKALINI CHAGUA CHADEMA ;

  1.HAKI ZAKO ZIHESHIMIWE PAMOJA NA KULINDWA
  2.WATUMISHI WOTE AMBAO WANASHINDWA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI ZA RAIA WAWAJIBISHWE NA KUFIKISHWA KATIA VYOMBO VYA SHERIA
  3.HAKIKISHA MCHAKATO WA KATIBA UNASHIRIKI KIKAMILIFU ILI UPATE RAHA NA MATUNDA YA UHURU WA TAIFA LAKO KWA KUHAKIKISHA CHADEMA INASHINDA 2015


  KUTOKUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA MCHAKATO WA KUPATA KATIBA MPYA KUTAKUFANYA KUKOSA HAKI YAKO YA KUIJENGA NCHI YAKO
   
 12. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hii ni mbaya sana na nimeisikiliza vizuri sana mahojiano kati ya wale walionyang'anywa mali zao na wale wababe wa ile kampuni lakini hakika hawajatenda haki hata kidogo!

  Nina mashaka sana na hiyo kampuni na ikiwezekana uchunguzi zaidi ifanyiwe.
   
 13. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  kuna hawa jamaa wa breakdown na wale wa kufunga tairi kufuli wanakera sana ila hawa jamaa wa kufunga tairi kufuli magari siku moja waliingia choo cha kike walienda kufunga gari ya mbaba mmoja pale town yule mzee alivyokuja akakuta gari lake limefungwa kufuli akawaambie wafungue wakaleta jeuri jamaa hakuongea mara mbili alichukua bastola akapiga risasi kikufuli chao akawasha gari lake motoooo jamaa wakabaki mdomo wazi
   
 14. u

  ureni JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Huyo jamaa aliyetishia bastola ni mbaya sana manake kwenye purukushani namna hiyo anaweza akatoa bastola akakuta yule anayemtishia na hiyo bastola naye akatoa yake hapo niambie kitatokea nini?
   
 15. u

  ureni JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Sio Majembe kweli manake majembe wanapenda hizo deal sana
   
 16. L

  LISAH Senior Member

  #16
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe ndiye uliye wapiga nini?
   
 17. u

  ureni JF-Expert Member

  #17
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Ha ha haa sio mimi.
   
 18. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  inawezekana ni hao ila sina uhakika kwakuwa mtoaji taarifa hakutaja jina la kampuni
  ila mimi ninahisi ni kampuni ya serikali coz ndio yenye kampuni za kijuha kama hizi tenda wanapeana peana tu
   
 19. H

  Hhm Member

  #19
  Feb 15, 2012
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Wana jf na watanzania wenzangu hii imenikera na imeniuma sana, mimi nasema kama serekali haitamchukulia hatua za kisheria mtu huyu....haki ya Mungu naapa watanzania tutasema sasa basi....Hivi sinza pale fast food kwa remy ukitaka kula gari ukapaki wapi kama siyo pembeni mwa barabara???? Unajuwa unapoleta mambo kama haya na miundo mbinu yapaswa kuwa imekwisha rekebishwa .... Sijaona kibao sinza hata kimoja barabarani kinachoelekeza usipaki hapa au paki hapa zaidi ya vituo vya mabasi tena off loading bays siyo stand kama stand.....Mkuu wa mkowa What are you doing???? Au ndo mpaka msikie watu wameuana ndo mshughulikie hili kama ilivyokuwa mgomo wa madaktari???.....RAIS KIKWETE ANGALIA WATENDAJI WAKO , mtatueleza nini majukwaani 2015????.....!!!!!!!
   
 20. m

  majutomakuu New Member

  #20
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye bold umekosea sana, unazani anajali????? kwani nani alikuambia sasa ivi tanzania tuna serikali??? tuna washehereshaji tu. Kama huyo rahisi wako hakujali vifo vya watu kutokana na mgomo wa madaktari kwa zaidi ya wiki tatu, sembuse huyo mwanamke kunyanyaswa kijinsia? nothing will happen, kwanza ndo kesho anaruka kwenda ........................!!!!!

   
Loading...