Wanawake wapenzi wa jinsia moja kutoka Mwanza waachiwa kwa dhamana

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,237
2,000
Mwanza.
Washtakiwa wanne katika shauri la kufanya vitendo vinavyoashiria mapenzi ya jinsia moja na makosa la kimtandao wameachiwa kwa dhamana baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza kutupilia mbali hoja za kuzuia dhamana zao zilizowasilishwa na upande wa Jamhuri.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Wilbert Chuma leo Desemba 15, baada ya kukubaliana na hoja za mawakili wa utetezi, Mashaka Tuguta, Ogastini Kulwa na Jebra Kambole kuwa hoja zilizowasilishwa na upande wa mashtaka ni dhaifu mbele ya macho ya sheria.

Washtakiwa katika shauri hilo namba 548/2017 ni Milembe Suleiman na Janeth Shonza wanaodaiwa kuvishana pete ya uchumba licha ya wote kuwa wanawake.

Wengine ni Aneth Mkuki anadaiwa kufanikisha sherehe wawili hao kuvishana pete na Richard Fabian anayeshtakiwa kwa kosa la mtandao kwa kusambaza video za tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii.

Katika uamuzi wake, Hakimu Chuma amesema Mahakama haiwezi kufanyia kazi maelezo na vitu vya mashaka na uvumi kuwa washtakiwa wanaweza kudhuriwa na jamii iliyochukizwa na kitendo wanachoshtakiwa nacho.

“Ni uamuzi wa Mahakama kuwa dhamana ni haki ya washtakiwa na upande wa mashtaka umeshindwa kuwasilisha hoja za msingi kwa nini wanyimwe dhamana zaidi ya kutoa hoja za hisia kuwa wakiachiwa watadhuriwa na jamii bila kueleza watadhurikaje na nani haswa atawadhuru,” amesema Hakimu Chuma katika uamuzi wake

Washtakiwa wameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja mwenye kitambulisho na barua ya utambulisho kutoka mamlaka inayotambulika kisheria pamoja na kusaini hati ya dhamana ya Sh6 milioni. Shauri limeahirishwa hadi Januari 8, mwakani.mwananchi

 

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,566
2,000
IMG_20171215_153029.jpg

Washtajiwa wa tuhuma za kujihusisha na mpenzi ya jinsia moja, Milembe Suleiman (Afisa Ugavi wa GGM), Janeth Shonza pamoja na wenzao wawili waachiwa kwa dhamana.

> Walikamatwa baada ya video akiwaonesha wakivishana Pete na kubusu kusambaa mitandaoni
 

Lugeye

JF-Expert Member
Apr 18, 2011
1,684
2,000
Huyo naona alikua anaoa mke wa pili,alishwahi kuoa tena mwanamke mwenzie
IMG-20171215-WA0001.jpg
 

ras jeff kapita

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
9,100
2,000
Huyo Afisa ugavi hapo kazi Hana tena na kwa akili za Kwenye ile video Inaonekana mtu wa bata Sana hapo ndipo ataaza kuwaona ndugu na marafiki wote Wachawi. Kumbe mchawi mwenyewe
Yaa

Na bosi wake asipomchukulia hatua

anang'olewa yy kitu kingine kesi kama

hizi ambazo ushahidi upo direct wa vidio

hazitakiwi kuchukua muda mrefu mwezi

unatosha kumaliza kesi....
 

JFK wabongo

JF-Expert Member
Aug 11, 2015
3,867
2,000
Huyo Afisa ugavi hapo kazi Hana tena na kwa akili za Kwenye ile video Inaonekana mtu wa bata Sana hapo ndipo ataaza kuwaona ndugu na marafiki wote Wachawi. Kumbe mchawi mwenyewe
Ndugu kumbuka wazungu ndo wahamasishaji wakuu wa uchafu huo, kwa mantiki hiyo hawawezi hata kumkata mshahara kwa siku alizokuwa rumande! Siajabu kesi ikiisha wakamhamishia nchi zinazoruhusu ili wakaendeleze libeneke la kutumia artificial dushelele!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom