Wanawake wapeni waume zenu unyumba pia wanaume mjirekebishe

Mama Sabrina

JF-Expert Member
Jul 30, 2016
16,621
27,567
Kumekuwa na malalamiko mengi sana ya wanawake walioolewa kuwanyima unyumba waume zao ni kwamba mnakuwa mmewazoea sana waume zenu kiasi mnakosa hamu ya tendo la ndoa? Mnakuwa mna matatizo ya homoni za vichocheo vinapungua? Tatizo nini maana hata humu nyuzi nyingi wanaume wanahalalisha kuchepuka kisa tu mke anamnyima unyumba ,wakienda kwa michepuko wanapewa sarakasi za kufa mtu.

Sasa najiuliza na nyie mtuambie ina maana hawa waume zenu wanataka kila siku au mara kwa mara kiasi kwamba mnachoka hadi kuwanyima

SWALI KWA WANAUME:mnawatumikisha mno wake zenu tendo la ndoa mpaka wanakinaiwa kiasi cha kufikia hawataki tena kuwapa tendoa la ndoa?

Maana hata kwenye mahusiano ya kawaida tu hamuwezi fanya mapenzi kila siku au mara kwa mara kuna muda mtafanya sana kuna muda mara moja moja

Au mmekosa mvuto kwa wake zenu hili nalo laweza changia mwanaume upo upo tu hata kunukia hunikii,viharufu vya kwapa tu ,mkeo haumjali kama kumbembeleza ,kumdekeza, akivaa husimfiii "mke wangu umependeza",,kumletea vizawadi vya hapa na pale ,kutoka nae kwenda kutembea maeneo tofauti na nyumbani
Tusije walaumu wanawake tu kumbe na nyie mna makosa ndani ya ndoa.
Mwanaume toka aoe hajawahi mwambia "Mke wangu nakupenda " hili neno mara ya mwisho alilisikia kipindi anatongozwa , hebu tutatue tatizo na sio kwenda kutafuta michepuko ni kujiongezea magonjwa tu, mfanye mkeo hata akiwa mbali nawe dakika kumi au lisaa moja akumiss akusumbue "mme wangu unarudi saa ngapi" mfanye mkeo ajione yeye ni tofauti na wengine aringe aone wanaume wengine huko wa nje hawakufikii hata kidogo .

Hebu Kila Mwanaume alieoa afanye hivi kwa mkewe aone mambo yanavyokuwa ndani ya nyumba na niwaambieni kitu hakuna mwanamke mgumu mbele ya mme wake kama utafanya hivi leo Mama Sabrina nawafunda kabisa mmetuchosha na lawama humu kila nyuzi nanyimwa unyumba haya sasa :

@jifunze kumuona mkeo mzuri kuliko wote hapa duniani iambie akili yako mke wangu ni mzuri,,akivaa msifie msogeze karibu yako mshike mkono mbusu,msifie ananukia vizuri,mwambie ye ni mzuri hukukosea kumuoa

@jifunze kumwambia unampenda hata mara mbili kwa wiki jamani ,kuna wanaume viburi akishaoa anakuwa mwanajeshi mkewe anakuwa kuruta wewe acha ubabe mwambie mkeo unampenda "Nakupenda mke wangu" legezeni hizo ndimi zenu ziwe laini zitaokoa vitu vingi.

@usimfanye mkeo kufuli la mlangoni toka nae tembea nae mpe muda wako sio unatoka kutafuta pesa unapitiliza bar tabia mbayaa kabisa hii ,hakuna cha maana kilichompeleka bar zaidi ya kunywa vibia tu aonekane nae yupo hakuna atakaekupa tuzo ya kushinda bar nenda kwako kakae na familia yako ,kakae na mke wako ndio rafiki yako mkubwa,kama hauna ishu za maana penda kutoka na familia yako au mkeo sio kuzurura tu na marafiki ,kuna wanaume mnawakumbatia sana marafiki siku ukipata shida huwaoni hata mmoja ,mimi huwaga nikiona marafiki wanamfata fata sana mtu wangu yaan utajua tu sipendii maana sifichii utagundua tu kwanza huwaga wanafiki sana wanakuwa wanawajua wanawake wengine wanaotembea na mumeo, awe na marafiki lakin asiwape muda mwingi kuzidi wewe mke.

@Fanya mapenzi na mkeo sehemu tofauti tofauti sio kila siku chumbani kwenu tu mazingira yale yale hapana zungukeni nyumba yote muimalize tena kama hamna watoto ndio raha sasa siku nyingine hata nyuma ya nyumba ,jikoni,bafuni, kwenye kochi, (hii ni kwa wale wenye nyumba zao,nyie mlopanga sasa sijui inakuwaje )nendeni bar mkanywe kama mnatumia vilevi tumieni sio lazima, laleni huko huko mfanye sehemu tofauti tofauti inatia hamasa,,na sio kila siku mkeo unampa style moja tu hapana mpe vitu tofauti tofauti ,pigo za kistaarabu pigo za kihunii ,ongeeni wakati mnafanya mapenzi ongeeni maneno matamu yatamkeni yalivyo yanatia shamsham na kuongeza hamu mwambie yeye ni mtamu hujawahi ona hahaha

@Mpelekee vizawadi vidogo ukienda nyumbani sio unapeleka tumbo lako tu maana wengine mna vitambii khaa haya jitahidi na hayo matumbo yenu mpeleke maua ,chocolate,pafyum,viatu,vitenge,hereni,mikufu ,hakikisha unachagua viti vizuri sio unanunua nguo lonya lonya tu ,au unanunua pafyum ya kuruthumu watakupiga nayo usoni jitahidi kwa mwezi hata vizawadi viwili,maana kuna wanaume ni mwiko kununua zawadi khaaa,,mke pokea zawadi sema "Asante mme wangu" sio umevimbisha uso tu kama Puto la kisukuma

mpe pesa mkeo inajulikana wanawake tunapenda pesa toka tukiwa wadogo kweli tunapenda kabisa ,mpe mkeo pesa "Mke wangu chukua hii utanunua vitu vyako unavyopenda "usitake kujua atakavyonunua maana wengine mkeo akimuomba pesa tu heee utaulizwa unaenda kununua nini eti ajue ,wapeni wake zenu pesa sio kununua nyama tu nyumbani akila ameshiba basii,moe kutokana na uwezo ulionao

@wasaidie wake zenu kazi,kazi za nyumbani ni nyingii mno zinachosha mpaka basi,mke ahakikishe nyumba ni safi,apike mara tatu kutwa,afue nguo ,mara aende sokoni kazi zinachosha nyie kama hamna uwezo wa kuweka binti wa kazi au wa kiume msaidiane kazi wote mfue pamoja,moike pamoja sio kumuachia mke kazi zote hujaoa ili mke awe mtumwa wako jamani jueni hilo ati,na hili hapa ndio tatizo wasaidie watoto wako ,wanaume wengi kila kitu anamuachia mke,tena ukute kazalishwa timu ya mpira weee kelele za hapo home ,usiku mke analala kama mzigo unadhani atapata hamu wapiii

Ni hayo tu jitahidini jamani maisha ndio haya hayaa tu na nyie wanawake acheni viburi muwatendee yapaswayo waume zenu acheni viburii kuwa mkishaolewa ndio mmemaliza badoo tumieni nafasi zenu vizuri,chungeni hiyo midomo yenu kwa waume zenu ,fanyeni usafi kila mahala muwe wasafii ,hakikisha mmeo msafi ,,akitaka muda wowote mpe ,,,hicho ndio kilikupeleka kwa mmeo shughulika ipaswavyo mbona ni raha sana lile tendo jamani kama sio mgonjwa upo mzima mpe k mmeo aifytaue haswa haswaaa
Nimemaliza....
 
Wanaume wasaidieni wanawake kazi ila kumbukeni tu
Kuna line ndogo sana kati ya mahaba na ubwege.
Za kuambiwa changanya na zako.

Kwenye unyumba hapo, no comment
Ice acha ubishii ,,nimewaambia pale kwenye kupeana mambo ziwe sehemu tofauti tofauti ikibidi hata vitanda muwe mnabadilisha sio kitanda hicho hicho mpaka miaka 10 hatutaki
 
Jf tumekua na wakunga wengi sana na hii Mara nyng utokea ile jamii tunayoish watu akil zao wamewekeza katka mapnz kuliko maendeleo
Hii husababshwa na wanaume kupenda kufikiria kwa kchwa cha chin kuliko kile cha juu

Mama Sabrina plz fungua ofis kuhusu aya mambo nakuhakikishia wateja watakua weng sana
 
Mmmh,, hakika umenena mama sab,,, wanaume tutayazingatia ila na wake nao wajue kupenda na kujali la sivyo itakuwa utumwa
Ndio maana nimewaonya wote na wanawake waache viburi wawapende waume zao,mme akifika sarawili kama imetuna akimuita mke ni haraka aende kwa mme hataka anapika ashushe mboga chini akahudumie mme
 
Back
Top Bottom