Wanawake Wanaweza: Muhimu Yapi ni Majukumu ya Mwanamke na Yapi ni Majukumu ya Mwanaume

Nundu_Tanzania

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
811
349
Nani anahusika na kutengeneza mambo haya: lengo ni nini?

Mwenye ufahamu wa mambo na elimu ya vitu hawezi kufikiri kwamba "wanawake hawawezi".

Hakuna sababu ya kujadili au kufanya matangazo, mikutano au kuhamasisha kuwa wanawake wanaweza.

Hili liko wazi wanawake wanaweza. Historia inaonyesha hilo ulimwenguni kote: kwenye sayansi, uvumbuzi na ugunduzi. Kwenye uongozi na siasa na kwenye maeneo yote ya kitaaluma na kijamii utawaona wanawake.

Chanzo kilichofanya mwanamke awepo duniani ndio hichohicho kimefanya mwanaume. Mwanamke na mwanaume, wote chanzo chao ni kimoja, Mungu.

Mungu aliwaumba mwanamke na mwanaume kama viumbe wake sawa mbele yake. Mwanamke hakutokana na mwanaume na mwanaume hakutokana na mwanamke, bali Mungu aliwaumba wote.

Kwa hiyo si suala kwamba mwanamke "anaweza" hilo liko wazi kwa sababu mwanamke kama alivyo mwanaume ni "sura na mfano wa Mungu".

Yeye mwanamke kama alivyo yeye mwanaume ana akili. Sasa kiumbe chenye akili kwa nini kisiweze?

Hii nguvu inayotumika popote ulimwenguni kuhamasisha kuwa wanawake wanaweza; kama vile katika historia hawakuwahi kuweza ingekuwa na maana kama ingetumika kuondoa imani potofu na tamaduni ovu dhidi ya mtu.

Suala sio wanawake wanaweza. Suala ni imani isio ya kweli ambayo humo zinatoka tamaduni ovu.

Tamaduni nyingi katika nchi za kipagani ni ovu dhidi ya mtu hasa mwanamke. Hili ndilo hasa tatizo sio tu kwa mwanamke pia mwanaume.

Imani isio ya kweli ambayo humo hutoka tamaduni ovu huharibu si tu uwezo wa kiakili bali pia mazingira yanayotakiwa na akili.

Hii ni kwa watu wote lakini inaathiri zaidi wanawake kwa sababu maumbile yao ya mwili hayawezi kuhimili vurugu ukilinganisha na mwanaume. Misuli ya mwanamke ni miembamba ukilinganisha na ya mwanaume.

Mungu hakumuumba mwanamke dhaifu na mwanaume imara, aliwaumba wote wategemeane wakamilishane.

Mungu alimuumba mume afanye majukumu haya na mwanamke afanye majukumu haya.

Hii haionyeshi kuwa mwanamke hana uwezo wa kufanya, ila majukumu.

Maandiko na mapokeo matakatifu yanaonyesha majukumu ya mume na mke.

Biblia na mapokeo yanamuonyesha mwanamume kama mwenye jukumu la uchumi na mwanamke kama mwenye jukumu la malezi.

Tunaweza kijifunza hilo kwa kuangalia pia tabia za wanyama.

Hii haina maana kuwa mwanamke asifanye shughuli za uchumi au mwanaume asihusike na malezi. Wote wanahitajiana ili kufanya majukumu ya kila mmoja kukamilika.

Mwanamume anamwitaji mwanamke katika kutekeleza majukumu yake ya uchumi. Hivyo hivyo mwanamke anamwitaji mwanaume katika kutekeleza majukumu yake ya malezi.

Mwanamke ana wajibu katika shughuli za uchumi, mume pia ana wajibu katika malezi.

Hakuna anaeweza kusema hawajibiki kwa majukumu ya mwenzake.

Majukumu ya mume na mke ni suala la asili. Asili yenyewe ndio imefanya hivyo.

Hatari iliyopo hapa ni kuwa hili wazo au hii nguvu kuwa wanawake wanaweza inaingilia majukumu.

Wanawake wanachukua majukumu ya wanaume wanaacha jukumu lao la msingi, malezi.

Hii ni hatari si tu kwa malezi yenyewe lakini pia kwa uchumi.

Ubongo wa mwanamke umeumbwa kwa ajili ya kufanya jukumu kuu la malezi tofauti na ubongo wa mwanaume. Hii ina maana kwamba mwanamke pamoja na kwamba atafanya majukumu mengine lakini ni kwa ajili ya malezi.

Hii nguvu ya kuwahamasisha wanawake kuwa wanaweza kana kwamba hawawezi inahatarisha majukumu ya uchumi na malezi.

Kuna makosa mengi. Hii ajenda ya wanawake wanaweza ni kosa lingine linalohatarisha uchumi na malezi.

Angalia kwenye jamii hasa nchi za kipagani, wanawake wameacha jukumu lao la malezi sasa wanafanya jukumu la uchumi.

Swali ni je, nani mwenye jukumu la malezi?

Kuna sababu nyingi ukiacha ajenda mbalimbali kumhusu mwanamke.

Sababu kubwa ni wanaume wenyewe licha ya kuwa ndio wenye jukumu la uchumi, lakini hawawafundishi wanawake, na hawatimizi wajibu wao inavyotakiwa.

Maendeleo hayawezi kupatikana kama hakuna maadili.
 
hili limekuwa likinisononesha sana anaposifiwa Mhe. Rais sijui hali hii huwa anaichukuliaje
 
Back
Top Bottom