Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Sio mimi Mtambuzi, bali hata utafiti uliowahi kuripotiwa kwenye jaridala That's Life! ambalo huaminika kwa kuandika habari za wanawake ulithibitisha juu ya jambo hili.
Imebainika kwamba, wanawake wengi wako tayari kudanganya kwenye jambo lolote maishani mwao. Nusu ya wanawake huwa wanadanganya karibu kila siku katika masuala mbalimbali.
Lakini pia imebainika kwamba, wanawake tisa katika kila kumi huwa wanadanganya kwa mambo ambayo wala hayana maana, yaani mambo ambayo mtu anashindwa kujua ni kwa nini wadanganye kuhusiana nayo. Kiasi cha wanane kati ya kila kumi, huwa wanajua kwamba, wanasema uongo, lakini uongo huo husemwa ili kuchokoza hisia za wengine. Hata kulia kwa uongo ili kuvuta hisia za wengine hutumiwa sana na wanawake.
Susan Quilliam, ambaye ni mtaalamu wa saikolojia anasema wanawake wengi kuongopa ni dalili kwamba wanashinikizwa na maisha ya kifamilia, kikazi na hata kwenye uhusiano. Kwa hiyo, hudanganya ili waweze kukabiliana na mazingira hayo magumu, ili waweze kuishi kwenye maisha haya ya kasheshe.
Lakini, Je, wanawake hudanganya kwenye mambo yapi hasa? Haya yafuatayo ndiyo ambayo wanawake hudanganya sana kuhusiana nayo. Kuna ununuzi wa vitu. Huonesha kwa waume zao kwamba wamenunua vitu kwa bei rahisi wakati siyo. Hudanganya kuhusu fedha, kuhusu mahali walipokuwa, kuhusu kuwa wanaumwa wakati siyo, kuhusu hisia zao, ambapo husema wanampenda mpenzi wakati siyo.
Kuhusu kunywa pombe, husema hawajanywa au hawanywi, wakati wamekunywa au ni wanywaji wazuri, hudanganya kuhusu uhusiano wao wa nyuma, na mengine ya aina nyingi tu. Kuhusu mapenzi, wanaume ni waongo zaidi , lakini kuhusu masuala mengine ya kimaisha hasa fedha na vitabia vingine, wanawake hawaaminiki kabisa.
Ukitaka kujua mengi juu ya jambo hili waweza kubofya hapa: To tell the truth, women lie | Mail Online