Wanawake wanapitia mateso na manyanyaso makubwa sana kwa wanaume zao

Haya ndio matatizo ya kulelewa na upande wa mama , au kukaa na mashangazi. Mtoto wa kiume unakuwa na hoja za kike kike.

Kwahiyo unatuhusishaje na mahusiano ya watu wengine as if tulikuwapo wakati wanatongozana?! ''

Kwanza majority ya hao wanawake, hao wanaume waliwachagua wenyewe kwa akili zao timamu. Hawakuwekewa pistol kichwani. Walitongozwa pengine na potential husband wakachomoa tena kwa nyodo na mapozi, then wakawachagua hao walio nao. Sasa why the blame on all males....?!

Siku zote utalala kitanda ulichotandika.
 
Hilo neno linaukweli sana sema tu ni kwa muda tofauti,
Wanawake wengi huwa na vituko ktk ndoa zao mpaka wafikishe miaka 40-45 na muda huo ndiyo mwanaume naye anaanza vituko kipindi mke anamuhitaji Sana wawe karibu kulea watoto.
Wanasubiria utamu uishe ndipo wakitulize sasa.
 
sawa kabisanakubaliana na wewe
mm sasa hivi ndio ninamsaidia X wangu ambaye tulidumu kwenye uhusiano kwa miaka 6
kipindi chote hicho alikataa nimuoe na mimba akawa anatoa akisema bado
mwaka wa 7 yake nikamuacha huku nikiwa bado ninampenda sana 7bu miaka yote hiyo alikuwa ananitesa sana kwenye uhusiano na ilichukua mwakamnzima kumsahau
Basi nikaoa nikaanza maisha na mwanamke mwingine naye akaamua kuzaa na jamaa alokuwa mwenyewe anampenda
Ebwana eeeh salaleee niliambiwa maisha ya kusikitisha anayoishi lkn sikumtafuta 7bu nitaanzaje
ila ikafika stage ikabidi anitafutee aisee alikuwa anaumwa sana imagine ana mtoto miezi 3 anaumwa jamaa yake wanaishi pamoja lkn ana mpango wa kumpeleka hosptari
nikamuambia hosptari tu sawa twende nikampeleka akatibiwa baada ya mwenzi mmoja akapona kabisa
sasa kipindi anaendelea na tiba akafunguka mengi sana kuhusu jamaa yake
ila kuna kauri moja aliongea nikajua yes sasa DUNIA imemfunza alimiambia

MZIMU wako kolelo nimeamini kweli we ulikuwa unanipenda kweli na ninaamini haitatokea tena chini ya JUA kupendwa kama ulivyonipenda

nikauliza kwann

akajibu yale niliyokuwa nakufanyia mimi basi ndicho huyu bwana ananifanyia sasa
namna ninavyoumia na nikikumbuka jinsi nilivykuwa nakufanyia haya huwa mpk ninatokwa na machozi
sio nalia kwa7bu ya haya mambo ya AJABU huyu bwana anayonifanyia
hapana
ninalia kwa jinsi nilivyokuwa nakufanyia lkn still hukuninunia na ukawa unazidi kunipenda na kunivumilia hakika nilikuwa nakutesa na hichi ninachokipata sasa ninastahili na ninahisi ni malipo yangu
Mimi YATIMA tangu nazariwa lkn MWENYEZIMUNGU akanipa wewe ila nikashindwa kukutumia na madhira yanayonikuta sasa sina hata pakukimbilia zaidi yakwako
lkn hata nikwambie turudiane sidhani km inawezekana nina mtoto wewe una familia
na hata nikisema nimuache huyu bwana nina mtoto mdogo nitakwendwa wapii sina mbele sina nyuma
HAKIKA ninateseka lakini yote haya nimeyataka mwenyewe

basi mimi wala sikusema chohote zaidi ya kumwmbia pole sana
nikamuambia tu ukiwa na shida utaniambia tukaachana hvyo

ni miaka mingi sasa imepita na mtoto wake kashakua amekuwa SINGLE MAMA anatangatanga na Dunia


So kwa story hiyo kwa uchche utagundua
MWANAMKE ukiona anateseka kwa mwanaume na kunyanyasika kayataka mwenyewe 7bu kaingia sehemu kusiko stahili 7bu ya tamaa au ulimbukeni na kusahau THAMANI YA UANAMKE wake
Hapo anakwambia hayo maneno ya uchungu mdomoni ila ndani ya nafsi anasema kosea tu kunielewa unipokee tena nikunyooshe tena....

Katika kitu nimejifunza ni kutompa mpa second chance mwanamke anapokesea. 99% jua atarudia kosa na ataomba tena msamaha akijua wewe ni mjinga kwake na atakupeleka atakavyo. Sharti ni moja, anapokosea, unamsomea mashitaka, na kutoa hukumu bila rufaa. Kwamba what's done is done, move out of the way.
 
Subilia umri usogee utasikia nimewasomesha kwa kujinyima, stress juu nakuanza kulalamikia wake zao eti wamewalisha watoto simu wakati mateso walikuja wanayapata na kuyaona
Wewe acha uongo, wanaume hawanaga hizo tabia. Mwanaume akijua kuwa hakuwapo katika malezi ya watoto huwa hawatungi maneno hata siku moja.

Cha zaidi atakesha akiomba msamaha na kujipendekeza kwa moja kwa moja kwa mtoto wake. Hawezi mchafua bi mkubwa maana atakuwa anakwepa vita ya kuchafuliwa.

Hii kitu ipo kwa akina mama zaidi. Maana wao ndio huchonga ngenga sana. Mtu hakuwahi kufanya hata kazi ya kulipwa mshahara ila utasikia anasema yeye ndie alikuwa ana nunua mahitaji ya mtoto.

Wanawake wamekuwa wabinafsi sana miaka hii.
 
Kuwa makini na wakina mama linapokuja suala la kumuonea huruma.....ni wajanja sana kwenye kuchukua sifa na lawama kuzipeleka kwa mwanaume, na wanaaminika kirahisi haswa kwa watoto.

Juzi nimemkuta mwanangu anamwambia mama yake nikikua ntakusaidia kulipa ada za wadogo zangu na ada huwa nalipa mm. Nikacheka ila ss nitabadili mfumo wa ada. Nitalipa kisha nimpe mwanangu risiti, mama yake abaki kuwa mpenzi wangu tu.
Nimeona wanaume wengi wanafanya hii. Mpelekec mtoto shule mwenyewe na umpe risiti aone ili mama yake asije kuleta shudu baadae.
 
Wanaume tunawatesa sana hawa wanawake inafikia stage hadi mwanamke anaongea mwenyewe jinsi gani anapitia magumu kwa mwanaume wake

Wanawake wanapitia mateso na manyanyaso makubwa sana kwa wanaume zao

Unakuta majukumu yote anaachiwa mwanamke huku mwanaume akiponda starehe bila wasiwasi wowote huku hajui watoto wanakula nini wanavaa nini

Hawa wanawake tunawabebesha mizigo mizito sana hata mwanaume ukipewa huwezi kuibeba yote

Mwanaume una unatelekeza watoto na familia bila kujua wanaishi vipi na wanapitia yapi wewe mwanaume unajijali wewe na nafsi yako huu ni ubinafsi wa hali ya juu

Mwanaume unamfanyia vitu ambavyo vinamdhalilisha mwanamke na unaona ufahari

Mwanaume unampa kimada chako kila kitu anachotaka wakati familia yako huwezi kuwafanyia kitu kama hicho

Mwanaume unamkataa mtoto au watoto wako kwasababu ya tamaa zako zisizo na umuhimu wowote

Mwanaume unamdharau mwanamke kwasababu una uwezo au kwasababu umemzalisha na kapoteza Muonekano wake wa awali

Wanaume tupunguze tamaa ambazo zitatutenganisha na familia zetu

Wanaume tupunguze UBINAFSI nikiri hili Wanaume sisi ni WABINAFSI SANA tunajilali wenyewe bila kuangalia familia

Wanaume tuwapende na tuwajali wake zetu ndo wenye umuhimu kwenye maisha yetu

Wanaume tupende na tujali familia zetu

Wanaume tuache kutelekeza damu zetu na kuzikataa kwaajili ya tamaa na ubinafsi

Wanaume tuache kuwanyanyasa wanawake na kuwatwisha mizigo mingi ambayo hawastahili kuibeba

Wanaume punguzeni ulimbukeni wa Wanawake hiyo michepuko haitokufikisha sehemu na hawatokuwa nawe kwenye kipindi utakachopatwa na matatizo

Wanaume kumpiga Mwanamke huo ni Ushamba, Ujinga na upumbavu

Hivi Wanaume unapataje nguvu ya Kunywa pombe wakati Familia yako hata cha kula hawana


Wanaume kuweni na Upendo Kwenye familia zenu kuanzia watoto na Mke wako (Family first)
Wanawake watakapotambua kwamba kiburi sio uungwana basi wataacha kujitesa wenyewe. Unakuta sababu ya kiburi anaamua kuwatesa watoto hataki kumwambia mwanaume ambaye ni baba wa watoto atume matunzo endapo wametengana unasikia sitaki hata shilingi kumi yake Nina uwezo wa kuhudumia wanangu.

Kwani Nani amekataa kwamba sio wanao he na huyo baba sio wanae? Kiukweli wapo wanaume wengi sana ambao wanataka kuhudumia family zao Ila wamama ni tatizo .
 
mzee tunakwama sana
Leo nilikuwa hospital mama anaongea mwenyewe mwanaume hatoi hata hela ya matibabu kwa mtoto wake
Acha kutetea hawa washenzi wasiokuwa na shukurani unateseka unaamka usiku kutafuta lenyewe limelala harafu linaleta dharau
 
Back
Top Bottom