Wanawake waliolelewa hivi ndoa zao huwa ngumu kweli! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake waliolelewa hivi ndoa zao huwa ngumu kweli!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 2, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 2, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kuna wazazi ambao pengine kwa kutofahamu hupenda kutamka maneno kama haya mbele ya watoto, ‘bila fedha dunia hii nani atakujua, ni nani atakuthamini,' watoto waliolelewa wakiyasikia maneno au kauli kama hizi mara kwa mara ndio wale watu ambao leo hawawezi kuthamini mtu mwingine hadi mtu huyo awe na fedha. Ndio wale ambao leo wanapoona mtu ana fedha hata akiwatemea machoni hufurahi na kuona fahari, wale ambao hujipendekeza kwa watu wenye fedha ni sehemu muhimu ya maisha yao.Hawa ndiyo wale watu ambao wanapokosa fedha huwa kama wagonjwa, ndoa zao huwa ngumu, uhusiano na wenzao huwa mgumu na kukata tamaa huwafikia haraka.

  Hii ni kwa sababu wazazi wao waliingiza akilini mwao imani hii ya kwamba mtu kutokuwa na fedha si lolote si chochote na kwamba mtu mwenye fedha ndiye binadamu zaidi na anastahili kunyenyekewa kwa sababu thamani yake ni kubwa. Kuna wakati wazazi huwa wanaamini kwamba mtoto hapaswi kuambiwa hapana kwa kila anachokihitaji kama uwezo wa kumpa kitu hicho upo.

  Wazazi hawa humpa mtoto kila anachokitaka bila kujali kama kinamsaidia katika makuzi yake au hapana.
  Tabia hii ni mbaya na ya hatari sana katika makuzi ya mtoto, kwani mtoto anayelelewa katika mazingira haya huja kuwa na wakati mgumu sana maishani kuhusiana na fedha. Bila shaka umeshawahi kusikia kuona watu ambao hawako tayari kusikia neno ‘hakuna' hasa kuhusu fedha. Hawa ni wale watu ambao walipokuwa watoto hawakunyimwa kitu, walipewa na wazazi kila walichohitaji. Kwa sababu hiyo wakakua wakiamini kwamba binadamu anapaswa kupata chochote kila anapokihitaji.Kama ni ndani ya ndoa wanawake waliopata malezi haya huwa wanasaidia sana kuzilegeza au hata kuzivunja ndoa zao.

  Kwa kuwa wamelelewa kwa kupewa kila walichokihitaji. Wanapoolewa huwa hawategemei hata siku moja waume zao kuwaambia ‘sina'. Wanapoambiwa ‘sina' na waume zao, wanatafsiri kauli hiyo kama ukosefu wa upendo. Kwani wazazi wao waliwapa kila kitu kwa sababu waliwapenda. Hivyo wao wanavyoamnini ni kwamba upendo ni sawa na kutoa kila kinachoombwa na mwingine.

  Bila shaka umeshawahi kusikia jinsi baadhi ya watu wanavyolalamika wanaponyimwa kitu walichoomba kutoka kwa mwingine. Hata ukiangalia mtindo wao wa kuomba ni kama vile wanatoa amri au kulazimisha wapewe, iwe ni haki yao au siyo haki yao. Hii ni kwa saabu katika makuzi ao hawakufundishwa kutofautisha kati ya utashi na hitaji. Ili kupunguza watu wa aina hii katika jamii inabidi wazazi wawe makini sana katika malezi ya watoto wao kuhusu fedha. Mtoto ni lazima aonyeshwe kwa upendo kwamba kuna wakati hawezi kupewa kila anachohitaji. Kuna wakati ni lazima anyimwe kwa upendo kitu anachohitaji hata kama wazazi wana uwezo wa kukipata kirahisi. Kunyimwa huku kutamfanya mtoto aingize akilini dhana kwamba katika maisha siyo lazima tupate kila kitu tunachokihitaji.
   
 2. A

  Aine JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Weka font size kubwa kidogo pia jaribu kuweka paragraph
   
 3. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  true
  asante
   
 4. A

  Aine JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  somo kwa wazazi wote hapa hasa wanaodekeza watoto hovyo bila kujua wao walikotoka
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  ndoa ndoano
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  thanks
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,348
  Likes Received: 418,854
  Trophy Points: 280
  Rose1980 wewe wachukia vijisenti kweli??????????????
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,348
  Likes Received: 418,854
  Trophy Points: 280
  mbona yote unayomshurutisha kesha yafanya.......................au huna la kuchangia tu...........
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,348
  Likes Received: 418,854
  Trophy Points: 280
  pesa zimewafikisha mabinti zetu kutamka hadharani ya kuwa bora aishi siku chache kwa miraha kulikoni aishi miaka mingi kwa shida.........ikiwa ni hoja ya kudandia midume ambayo inapesa lakini afya zao zina migogoro mikubwa.......................lakini watakapoanza kuumwa ndipo watalia na kusaga meno na hapatakuwepo wakuwaokoa..................
   
 10. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  yan umesema ukwel mtupu big up man umenijenga
   
 11. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  kaka umenikunbusha mbali saaaana! nakumbuka wakati nasoma o level hizi fashion zinaingia kila leo, enzi za moccassin wenzangu wamepiga moccassin mie nipo na ahsante mchagga zile za miaka ilee. ngoma ikikuwa kumwomba mzee pesa ya kiatu au suruali au shati. nilikuwa nachukua hadi wiki mbili kumwambia baba kiatu cha shule kimeisha! mzee wangu alikuwa MKALI jamani we acha tuu. akirudi kazini tukisikia gari tu kila mtu chumbani kwake! namvizia jmosi yupo home wakati wa chai asubuhi aaagh nikimwona tu nanyong'onyea maneno yote yanapotea! siku nikifanikiwa kumwambia atanibalasa mtindo mmoja mwisho anaenda kuchukua kiatu chake ile pair ambayo haitumii sana mzee napelekwa kwa fundi enzi zile wachagga wamebobea kushona viatu basi kinapunguzwa kile hahaaa nikitoja hapo miezi sita kinapiga mzigo hakuna cha sijui kukataa waka nini. mpaka bro wangu alipoanza kazi na mie sasa ndo nikaanza kufaidi kwenda na wakati. simlaumu baba yangu najua uchumi ulikuwa mdogo na tulikuwa watoto saba wote twende shule haikuwa kazi ndogo. ila kinyume chake nimeweza au ninaweza kuishi maisha yeyote yale kutokana na ile life tuliyoishi. kizazi cha sasa kinalipiza kisasi kwa kukosa kupewa kila kitu wakati wakiwa wadogo. nimeshuhudia wazazi wengi vijana wakisema ngoja nimnunulie hiki au kile mtoto wangu coz yeye alipokuwa mdogo hakupata fulsa ya kuwa nacho. mtoto mdogo wa miaka mitatu minne mpaka mitano wazazi wanamnunulia simu anakwenda nayo shule. mtoto anapewa alfu tano daily anapokwenda shule, wale wa boarding ndo usiseme wapewa mpaka kilo tano kwa mwezi. imagine huyi anakuwa mkeo halafu huna pesa utaimba kikwenu mdau
   
 12. A

  Aine JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tatizo lako unakurupuka, hukusoma mwanzo ilikuwaje muulize mwenyewe kama alipopost mara ya kwanza ilikuwaje!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 13. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #13
  Aug 2, 2011
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Tutazingatia haya, thanx
   
Loading...