Wanawake waliokuwa bega kwa bega na Mzee Mandela katika harakati za kutafuta uhuru...!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
the-women-in-Nelson-Mandelas-life.jpg


Wakati dunia bado inaomboleza kifo cha Mzee Nelson Mandela, nimeona ni vyema tukajifunza machache kwa kuangalia yale aliyoyafanya wakati wa uhai wake. najua yameshazungumzwa mengi kuhusu yale aliyoyafanya wakati wa uhai wake lakini leo nimeona nizungumzie wanawake waliokuwa naye bega kwa bega katika harakazi hizo za kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi uliodumu kwa karne kadhaa nchini Afrika Kusini.

Hapa nitawazungumzia wake zake na baadhi ya wanawake aliyoshirikiana nao kupitia chama cha ANC katika harakati hizo za kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo. Pia nitazungumzia wanawake ambao walipata ushawishi baada ya kuona harakati zake na kujiunga na harakati hizo. Wapo baadhi ya wanawake jasiri ambao waliwahi kufungwa jela kutokana na misimamo yao katika kupinga ubaguzi wa rangi na wengine ambao walikuwa bega kwa bega na Mzee Mandela katika safari hiyo ndefu ya kutafuta uhuru.

Evelyn-Mase.jpg


Evelyn Masse
Huyu alikuwa ndiye mke wa Kwanza wa Nelson Mandela. Walioana mwaka 1944. Wawili hawa walikutana kupitia kwa marafiki wa Mandela ambao walikuwa pamoja katika harakati za kupinga ubaguzi wa rangi, na si wengine bali ni Walter na Albetina Sisulu. Hata hivyo mambo yalikuwa magumu katika ndoa yao baada ya Mandela kuonekana kuyapa umuhimu mapambano ya kupigania uhuru na kusahau majukumu ya familia na hapo ndipo tuhuma za uzinzi na kukmosa uaminifu kwa mkewe zikaibuka. Evelyn ambaye alishapata watoto wanne na Mandela aliamua kuyapa kisogo mapambano ya kupigania uhuru na kuamua kufanya kazi ya Mungu kupitia katika kanisa la Jehova Witness. Waliachana rasmi mwaka 1958.

Winnie-Mandela_scalewidth_630.jpg


Winnie Madikizela-Mandela

Mwaka huo huo baada ya Mandela kuachana na Evelyn Mase, alimuoa Winnie Madikizela. Wakati huo Mandela alikuwa tayari ni kiongozi wa ANC na Winnie akawa ni mmoja wa wanawake waliosimama mara kupinga ubaguzi wa rangi akishirikiana bega kwa bega na mumewe ambaye wakati huo alikuwa akiwindwa na utawala wa Makaburu kutokana na harakati zake. Mwaka 1964 Mandela alikamatwa na kushitakiwa na hatimaye kufungwa kifungo cha maisha jela. Aliachwa na jukumu la kulea mabinti wao wawili kutokana na mumewe kufungwa na hapo ndipo alipogeuka na kuwa mwanaharakati machachari ambapo alianzisha timu yake ya mpira aliyoiita Mandela Football club, timu hiyo ilikuwa na ikiendesha vitendo vya ukatili dhidi ya waafrika weusi walioonekana kuunga mkono serikali ya kibaguzi nchini humo. Hata hivyo pamoja na vitendo hivyo vilivyokuwa vikifanywa na timu yake, lakini bado alionekana kama mama jasiri na shujaa mbele ya watu weusi wa Afrika Kusini waliokuwa wakipinga ubaguzi wa rangi, hivyo walimuita "Mama wa Taifa." Baada ya Mandela kutoka gerezani na kuchaguliwa kuwa kuwa raisi wa kwanza mweusi nchini humo alimteua mkewe huyom kuwa naibu waziri wa sanaa kabla ya kuondolewa katika nafasi hiyo mwaka 1995. hata hivyo aliendelea kushikilia nafasi ya Urais wa umoja wa wanawake wa ANC (ANC Women League) na ubunge. Mandela aliachana na Winnie Madikizela mwaka 1996.

Graca-Machel-PF.jpg


Craca Machel

Cracaz mwanasheria aliyekuwa akitetea haki za wanawake na watoto nchini Msumbiji alikuwa ni mjane wa aliyekuwa raisi wa Msumbiji Samora Machel. aliolewa na Nelson Mandela mwaka 1998 wakati akisherehekea kutimiza miaka 80 ya kuzaliwa. Lakini kabla ya kufunga ndoa hiyo Craca alikuwa ni waziri wa elimu na utamaduni nchini Msumbiji

Lillian-Masediba-Ngoyi.jpg


Lillian Masediba Ngoyi


Lillian ambaye alifanya kazi bega kw abega na Mandela, alikuwa ni mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuingia kwenye kamati kuu ya ANC (ANC Executive Board) ambapo alisaidia kwa kiasi kikubwa kuunda shirikisho la wanawake wa Afrika Kusini (Federation of South Africa Women). Lillian wakati fulani aliwahi kuwa rais wa umoja wa wanawake wa ANC ambapo alisaidia harakati za kupinga watu weusi wa Afrika Kusini kulazimishwa kubeba passbook zao mahalim popote wanapokwenda na utawala wa makaburu nchini humo. (Passbook ni kama paspot lakini zinakuwa na maelekezo yanayoonyesha ni wapi unaweza kusafiri na wapi unaweza kufanya kazi n.k.). harakati zake zilimsababishia kufungwa jela mara kadhaa. mama huyu amepewa heshima ambapo eneo la Strijdom Square yalipofanyika maandamano ya kupinga mpango huo wa kulazimisha watu weusi nchini humo kubeba passbook kupewa jina lake. Mama huyu anaweza kufananishwa na mama aliyekuwa mstari wa mbele kupigania uhuru hapa nchini Bibi Titi Mohamed.


Albertina-S.jpg


Albertina Sisulu


Huyu alikuwa ni mke wa hayati Walter Sisulu (aliyekuwa amefungwa na Nelson Mandela na kukaa gerezani kwa miaka 25 katika gereza pa Robben Island, alikuwa ni mmoja wa vigogo waliokuwa wakipinga ubaguzi wa rangi nchini Africa Kusini). Awali Albertina hakutaka kujiunga na harakati za kupinga ubaguzi wa rangi ingawa alikuwa akimsaidia mumewe katika harakati huzo. Baadaye alijiunga na harakati hizo kwa kujiunga na ANC ambapo aliongeza nguvu katika mapambano hayo. Alikuwa ni mjumbe wa kamati kuu ya shirikisho la wanawake la Afrika Kusini, na aliwahi kufungwa kwa wiki tatu kwa kuandamana kupinga amri ya serikali ya kibaguzi ya Afika Kusini ya kuwalazimisha watu weusi nchini humo kubeba passbook zao popote wanapokwenda. (Alikuwa mstari wa mbele na Lillian Ngoyi katika maandamano hayo). hata hivyo aliachiwa huru baada ya Mandela kumtetea kama mwanasheria wake. hata hivyo aliendeela kupata misukosuko kutoka katika serikali ya Kibaguzi ya nchini humo na kufungwa mara kadhaa. Mnamo mwaka 1994 alichaguliwa kuwa mbunge katika bunge la nchi hiyo lisilo la kibaguzi.


Alice-Mase-Sisulu.jpg


Alice Mase Sisulu

Huyu alikuwa ni mama wa rafiki mkubwa wa Mandela, Walter Sisulu, Mama huyu pia alikuwa ni rafiki wa karibu wa Mandela. mandela aliwahi kuishi kwa mama huyu akiwa na rafikiye Walter baada ya kupata wazo la kuhamia Johannesburg. ambapo walianza harakati zao za kupinga ubaguzi wa rangi. Alice pia alikuwa ni binamu yake na Evelyn Mase, mke wa kwanza wa Mandela (Evelyn Mase ameshafariki) kwa hiyo Evelyn kutumia ubini nwa Mase haikuwa ni nasibu.

Amina-Cachalia.jpg


Amina Cachalia

Kuna wakati kulizuka minong'ono baada ya Mandela kuachana na mkewe Winnie Madikizela kwamba alikuwa anafikiria kumuoa Amina Cachalia, hata hivyo ilidaiwa kwamba mama huyu mwenye asili ya Kiasia alikataa kwa sababu mumewe alikuwa amefariki si siku nyingi. Mama huyu alikuwa anafahamika kama rafiki wa karibu na wa siku nyingi wa Mzee Mandela. Amina alijiunga na harakati za kuopinga ubaguzi wa rangi tangu akiwa binti na alikuwa ni mwansheria wa kupigania haki za wanawake. harakati zak3e mara nyingi zilikuwa zikimuweka katika matatizo na serikali ya kibaguzi hadi kufikia kuwekwa kizuizini nyumbani kwake kwa miaka 15 kuanzia miaka ya 60 mpaka 70. Aliwahi kushika nafasi kadhaa za kisiasa kuanzia katia shirikisho la wanawake hadi kuwa mbunge.
 
amu, umewaza nini hasa mpaka ukafikiri jamaa alikuwa na mpango kando...?
 
Last edited by a moderator:
Hakuwa na nyumba ndogo?ni utamaduni wa kiafrika kuwa na small haus ujue
amu miaka yote aliyokaa jela angewezaje kuwa na nyumba ndogo....!
 
Last edited by a moderator:
^^
Mtambuzi naona umemfichia siri Winnie Mandela na aliyoyafanya!
Oo! Sorry kumbe leo unaongea na wanawake upande wa mema tu.
^^
 
Last edited by a moderator:
Madiba alikua wamo naye....naona aliikosakosa hiyo ya kihindi.... Ila wanawake wanamchango mkubwa sana kwa wanaume, hata Maria magdalena inasemekana alikua na mchango mkubwa sana kwa Yesu japo historia iliyomuandika sana ilifichwa na inasemekana kuna hadi injili yake ambayo iliongelea sana maisha ya Yesu ambayo hayajaongelewa sehemu nyingine.. Mimi hii niliifahamu kupitia Nationa Geographic Channel
 
Back
Top Bottom