Wanawake walia Magufuli ‘kuwabania’ katika uteuzi

Simbajr

Senior Member
Apr 1, 2010
188
41
1.jpg

Mashirika yanayotetea haki za wanawake na usawa wa kijinsi nchini yamesema uteuzi wa nafasi muhimu za uongozi serikalini unaofanywa na Rais John Magufuli, hauzingatii hali halisi ya uwakilishi wa kijinsia.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam kwa niaba ya mashirika hayo, Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi alisema licha ya kupiga kelele tangu uteuzi wa Baraza la Mawaziri kuwa haukuzingatia usawa huo, bado hali inaonekana kuwa tete kwa upande wa wanawake.

Alisema katika baraza hilo, kati ya mawaziri 19, wanne pekee ndiyo wanawake sawa na asilimia 21.1 ya mawaziri wote ikilinganishwa na uteuzi wa baraza la Serikali ya Awamu ya Nne ambalo lilikuwa na mawaziri wanawake 10 sawa na asilimia 33.3.

Alisema manaibu waziri kati ya 16 waliopo, wanawake ni watano sawa na asilimia 31.25.

“Ukiangalia upande wa makatibu wakuu, walioteuliwa ni 29 kati ya hao, wanaume ni 26 sawa na asilimia 89.7 huku wanawake wakipungua kutoka watano sawa na asilimia 21.7 ya mwaka 2014 hadi kufikia watatu sawa na asilimia 10.3 kwa sasa,” alisema Liundi.

Alisema uteuzi wa wanawake katika nafasi hizo umepungua kwa asilimia 10. Katika nafasi ya wakuu wa mikoa, Liundi alisema idadi ya wanawake imeshuka zaidi, kati ya wakuu wa mikoa 26 Tanzania Bara, 21 ni wanaume sawa na asilimia 80 na wanawake ni watano sawa na asilimia mbili.

Kadhalika, alisema idadi ya wakuu wa wilaya imezidi kuporomoka ikilinganishwa na ya Februari mwaka jana ambako wanawake walikuwa asilimia 35.07: “Kwa maana nyingine, hapa uteuzi umepungua kwa asilimia saba.”

Liundi alisema mikoa mitatu ya Simiyu, Songwe na Singida haina wawakilishi wanawake kwa nafasi ya ukuu wa wilaya.

“Hii iko hata kwenye nafasi za makatibu tawala wa mikoa na wilaya na wakurugenzi wa halmashauri, hatuoni idadi ya wanawake ikiongezeka na badala yake inashuka,” alisema.

Mwakilishi wa Taasisi ya Women Fund Tanzania (WFT), Dk Dinna Mbaga alisema Tanzania ni kati ya mataifa duniani yaliyoridhia na kusaini mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda inayoweka misingi ya usawa kwa binadamu ikiwamo ushiriki katika ngazi zote za uamuzi, lakini haitekelezi mikataba hiyo kwa ridhaa mpaka isukumwe na asasi za kiraia jambo linaloleta ukakasi.

Alisema miongoni mwa mikataba hiyo ni Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu (UDHR: 1948), Mkataba wa Kimataifa wa Kutokomeza aina zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW: 1979), Mpango kazi wa Beijing (1995), Mkataba wa Ziada wa Maputo na Mkataba wa Nyongeza wa Jinsia na Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Mwakilishi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Gladness Munuo alisema Tanzania kupitia Dira ya Maendeleo ya 2025, imetambua kuwa mojawapo ya vichocheo vya ukuaji wa uchumi ni pamoja na kuwa na jamii yenye maono ya kimaendeleo na utamaduni wezeshi kwa wanawake na makundi mengine.

Chanzo: MPEKUZI
 
Magu dont believe in women. Nadhani mnakumbuka wakati wa kampeni alipomtambulisha mke wake alisemaje.

Second, magu anatokea kanda ya ziwa bila kujali ni msukuma au mkurya, most of lake zoners ni sexists, they take women as week creatures.

Msimlaumu sana.
 
Nashindwa kuelewa ktk awamu hii sisi wanawake tumewekwa wapi, kwani katika teuzi nyingi wamekuwa wakiteuliwa wanaume wanawake tukiachwa nyuma, je ni ni kuwa wanawake hawana uwezo wa kuongoza? Hawana elimu au vipi?

Kuna uteuzi mwingi umepita, wakuu wa taasisi, wakuu wa vitengo mbali mbali ndani ya serikali lkn wanawake sijasikia.....wakati hapo hapo katika vyuo mbali mbali utaona majina ya wanawake waliomaliza chuo kila kukicha...hii imekaaje..
 
Awamu iliopita hao walioteuliwa nini walifanya. ....
Uwezo ndio tatizo kilango alipewa kaishia kuharibu! !
Wenye uwezo wanapewa ambao ni wachache....ukumbuke hachagui kuwafurahisha bali anataka mtu atakaefanya kazi haswaa!!
 
Wanawake wajibu wao mkubwa ni kulea na kutunza familia, hilo limeelezwa vizuri sana kwa kila mcha Mungu ni hima alitambue hilo. Vitabu vya dini kuu zote vinaelezea vizuri hayo mambo, wanawake rudini kwenye uasiri wenu ...msijibebeshe majukumu mengine wakati yale ya msingi ya kwenu mkiyapa visogo

Ukweli ndo huo mkichukia sawa na mkinitusi pia sawa.
 
MIMI ni mwanaupinzani wa CCM ,ila kwa ili nampa hongera Magufuli. Mwanamke kutaka kulingana na mwanaume ni dhambi na kiburi ambacho sawa na kile alichoonyesha shetani kule mbinguni kutaka kulingana na mwanaume,
Mungu kukuweka mwanamke chini ya mwanaume alitazama mbali.
 
Yaani Nyama ya ubavu wangu iongoze kichwa!! Hiyo haikibaliki,Jk na Mkp ndio walileta hizo siasa uchwara za 50/50! Heko Jpm kwa hili.
 
Unataka kuteuliwa ili iweje .....uoni unadharilisha wewe mwanamke jipiganie usipende mtelezo .............hapa kaxi tu
 
Back
Top Bottom