Wanawake walia kubaguliwa katika nafasi za uongozi hapa nchini

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797



Masoud Masasi,Dodoma yetu blog

WANAWAKE wamesema dhana ya usawa wa kijinsia hapa nchini hasa katika nafasi za uongozi kwenye vyama vya siasa na serikali bado umekuwa ukimbagua mwanamke katika kuumpa fursa ya kuongoza nafasi hizo lichaya wao kuwa wengi katika idadi ya watu hapa nchini.​

Hayo yalibainishwa na Katibu wa shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia haki za wanawake la WOWAP Fortunata Makafu wakati
alipokuwa akiwasilisha mada katika mdahalo wa dhana ya usawa wa jinsia kwa maendeleo ya jimbo la Dodoma mjini lilolofanyika mjini hapa.

Makafu alisema kwenye vyama vya siasa hapa nchini nafasi zote za juu za uongozi zimeshikiliwa na wanaume ambapo amesema hakuna hata chama kimoja ambacho nafasi hizo zimeshikwa na mwanamke. Alisema kwa upande wa serikali nafasi za mawaziri,makatibu wakuu na wakurugenzi asilimia kubwa zimeshikwa na wanaume ambapo wanawake ni wachache huku akisema idadi ya wanawake waliosoma ni kubwa lakini wamekuwa wakibaguliwa katika kupata fursa hizo.

"Ukiangalia nafasi zote za juu katika uongozi wa vyama vya siasa hapa
nchini zimeshikwa na wanaume pekee kwa upande wa serikali baraza la mawaziri wanawake wachache lakini wanawake ni wengi katika idadi ya watu Tanzania lakini hawapatiwi fursa ya kutosha katika nafasi za uongozi"alisema Makafu.

Alisema hatua hiyo inatokana na jamii kumwangalia mwanamke katika jicho la kumuhukumu kuwa hawezi kuongoza hata kama ana uwezo mkubwa kuliko mwanaume.

"Wakati mwingine jamii inakuwa inamukumu mwanamke kuwa hawezi kuongoza hata kama ana uwezo mkubwa kuliko mwanaume lakini tumekuwa tuna uwezo mkubwa katika nafasi chache tulizopewa na kuonyesha uchapa kazi"alisema.

Alisema pia kwa upande wa ajira kazi na madaraka makubwa yenye
mishahara mikubwa hushikwa na wanaume huku wanawake wakiwa chache sana waliopatiwa fursa hiyo hapa nchini.
 
Issue ni kubwa haswa Income inequality na Salaries kuwapendekeza Wanaume kupata Mishahara Mikubwa zaidi ya Wanawake
 
Back
Top Bottom