Wanawake wafanye nini kuhakikisha waume zao hawapotezi hisia za mapenzi kwao?

analysti

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
729
612
ffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffff
 
as if wanawake tu ndo chanzo cha haya mafarakano au mume kutoka nje ya ndoa!!! kwa nini usiseme wana ndoa wafanya nini kuepuka hili tatizo maana matatizo mengi kwenye ndoa ni contributory.
 
Limekuwa ni tatizo katika jamii yetu,kabla ya kuoana mwanamume huwa na hisia kali za kimapenzi kwa mchumba wake, lakini baada ya kuoana, kwa wastani wa miaka miwili mitatu hivi, mume huanza kupoteza hisia kwa mke wake, na hapo ndipo huanza kutafuta vimada nje ya ndoa. Na hii imekuwa chanzo cha mifarakano mingi katika ndoa. Ni kitu gani hasa kifanywe na wanawake hawa au wanandoa hawa kuepukana na hii hali??

Mbona nimesema hilo bht??
 
Samahani:
Wewe umeoa / umeolewa?
Kama ndio, ndoa yako ina umri gani? Je hisia zako za kimapenzi kwa mme/mke wako zimebadilika?
Kama hujaolewa umejuaje haya mambo ya wakubwa?:closed_2:
 
Wana JF naomba maoni yenu kwa faida yangu na wana JF wengine!! PLZ
 
as if wanawake tu ndo chanzo cha haya mafarakano au mume kutoka nje ya ndoa!!! kwa nini usiseme wana ndoa wafanya nini kuepuka hili tatizo maana matatizo mengi kwenye ndoa ni contributory.
'

halafu cdhani kuna lolote la mwanamke afanye hapo, kama lijitu lina tamaa bac hata ufanyaje nje atatoka, sema nyie ndio mpunguza tamaa zenu kutunusuru sie na msongo wa mawazo.
 
Kumbe wanaume mkioa baada ya miaka miwili mpaka mitatu mnapoteza hisia za mapenzi kwa wake zenu nilikuwa bado kufikilia hilo..:lie:
 
1. Ndoa siyo kifungo kifungacho milango ya ufahamu. Katika ndoa mabadiliko yategemewe ila kinachotakiwa ni kujua kuwa umeshaji commit kwa mtu uliyefunga naye ndoa.

2.Mtoa hoja anauliza wanawake wafanye nini ili waume wasipoteze hisia. Sijui kama anajua kuwa hata wanawake wanapoteza hisia kwa waume zao. Its both ways. Kinachotakiwa ni kuendelea kuheshimiana, kujitahidi kupendana, na kujua kuwa ndoa ni zaidi ya hisia za mapenzi.
 
sijajua huyu mtoa hoja ni jinsia gani, ingekua vyema akauliza wanandoa wafanye nn! hebu tuchangie kwa umoja lipi wanandoa wafanye kudumisha upend katika ndoa zao
 
Limekuwa ni tatizo katika jamii yetu,kabla ya kuoana mwanamume huwa na hisia kali za kimapenzi kwa mchumba wake,

Hizi hisia huwa zinasababishwa na nini? Na huyo mwanamke? Kama si yeye anayezisababisha then itakuwa vigumu kwa yeye kuzi-control!

............ lakini baada ya kuoana, kwa wastani wa miaka miwili mitatu hivi, mume huanza kupoteza hisia kwa mke wake, na hapo ndipo huanza kutafuta vimada nje ya ndoa.
Hisia kamwe haziwezi kubaki pale pale! Zinabadilika kama aspects nyingine katika huo uhusiano zinavyobadilika na kama walivyosema wengine hapo juu, hili si kwa wanaume tu bali hata wanawake. Sasa unafanya nini kukabiliana na mabadiliko haya au kupunguza athari za mabadiliko haya, nadhani ndio suala la msingi. Ndio maana binaadamu zaidi ya kupewa hisia akaongezewa pia na utashi!
 
as if wanawake tu ndo chanzo cha haya mafarakano au mume kutoka nje ya ndoa!!! kwa nini usiseme wana ndoa wafanya nini kuepuka hili tatizo maana matatizo mengi kwenye ndoa ni contributory.
Mama Brian says thanks to bht for useful post!
 
Samahani:
Wewe umeoa / umeolewa?
Kama ndio, ndoa yako ina umri gani? Je hisia zako za kimapenzi kwa mme/mke wako zimebadilika?
Kama hujaolewa umejuaje haya mambo ya wakubwa?:closed_2:

Ingekuwa mshua wangu... ningekuita kifimbocheza kwa haya majiswali...!!
 
Kuna tofauti ya hisia kubadilika na tamaa, hapa kinchotokea ni tamaa na akili kushindwa kumudu tamaa za miili.
Kimsingi ndoa nyingi huwa na matatizo ya kukosa uaminifu katika miacha michache ya mwanzo (labda mitatu), na baada ya purukushani nyingi za hapa na pale wanandoa hupunguza tamaa na kugundua thamani ya ndoa (wandoa wanapovuka miaka 45).
Cha kufanya kuepuka tamaa hakuna......kuzishinda tamaa ni mtu mwenyewe aamue.
 
Back
Top Bottom