Wanawake wa siku hizi hawataki kero, ukimkera tu umeachwa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Habari zenu wakuu,

Nawakumbusha wanaume kwamba wasiishi kwa mazoea. Siku hizi hakuna Wanawake wanaopenda tabu au kutesa moyo. Ndo maana unaona ndoa nyingi hazidumu.

Mwanamke wa siku hizi akisikia kwamba una mchepuko anakuacha, yaani hajaona just tu kusikia..

Mwanamke wa siku hizi ukimletea mapombepombe yako wakati yeye hanywi na akikukataza ukakataa unaachwa, bora uoe mnywaji.

Mwanamke akiongea muache aongee hadi hasira ziishe, huwezi mshinda kwenye kuongea hata ukimeza spika. Mwanamke akiongea ukamjibu utaishia kugombana naye halafu kesho anakuacha anarudi kwako anasema ulimpiga hata kama umemfinya tu.

Usitake kushindana na mwanamke, ukiona umeanza kushindana na mwanamke, jijue ndoa yako imeanza kuteteleka kesho yake anakuacha unabaki unashindana na baridi usiku na akiondoka unabaki unashindana na kubadilisha wasichana.

Mkeo mheshimu na umnyenyekee vinginevyo utaachwa.

Watoto wadogo watabisha lakini huu ni ushauri nawapa kutokana na experience.

Usiguse simu ya mkeo, bila ruhusa yake ukiigusa utaipasua then mtagombana atakuacha.

Umeoa mwanamke mwenye mtoto au watoto ukataka kumfuatilia anapompeleka mtoto kwa baba yake jua utakufa kwa presha kukonda kwa wivu maana yake utaachwa. Siku ukiwafumania utaambiwa alikutangulia kuniona then unaachwa.

Kama unamhitaji mkeo au unampenda na unataka kufanya naye maisha usimfuatilie.. Muache Mungu amuongoze, wewe Mwanaume dumu magotini mwa Mungu akiomba akusaidie, hakika utashinda.

Walioshindwa na ndoa au walioachika wataanza kusema amekupa limbwata.. Usijali maneno yao sababu ukiachwa watajisifia sana.

Usipofuata huu ushauri jua kesho unaachwa.

Kama huogopi kuachwa jua hujawa tayari kuwa na familia. Usoe na endelea na ubazazi, kama umeoa acha kumtesa mtoto wa watu.

Kama unaogopa kuachwa basi oa na tembea katika misingi hii upate wa kukuzika na kukulilia siku ukifa.
 
Mzee huo ni ubushoke
Sasa uanaume uko wapi hapo!!??
Yani ushindwe kurekebisha makosa kisa kuogopa kuachwa na mwanamke mkuu


Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu uanaume si kumfanya mkeo aishi amepiga magoti, bali uanaume ni pamoja na kudhibiti hasira na kuona mbele kabla ya tatizo kitokea. Uanaume sio kufoka bali kuelewana na mkeo ikiwemo kumsikiliza n akumhudumia. Ukianza uanaume wako ndani ya ndoa jua kesho unaachwa. Nani anataka kero?
 
Yaani ushindwe kum-control mkeo kisa tu unaogopa kuachwa?
Utaishia kuwa Bushoke square.

Usipotumia akili na nguvu ya uanaume huwezi kuishi na mwanamke.
Anyway, kuna mengine umeongea sawa kabisa ni ukweli.

Siku zote usiishi kwa hofu ya kuachwa na mwanamke, hutoboi hapo. Ukiishi kwa hofu ya kuachwa utapata taabu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo unamzungumzia mwanamke yupi? Mke au girlfriend?..kama ni girlfriend ukimdekeza sana atakupanda kichwani.yani uogope kumchapa makofi eti kisa atakasirika na kukuacha?
 
Hapo unamzungumzia mwanamke yupi? Mke au girlfriend?..kama ni girlfriend ukimdekeza sana atakupanda kichwani.yani uogope kumchapa makofi eti kisa atakasirika na kukuacha?
Ukimpiga anaenda Polisi dawati la jinsia then unawekwa korokoroni siku tatu usipopelekwa mahakani ukarudi nyumbani na hasira zako u ajenga chuki anagundua usivyompenda kesho yake unaachwa unakuta barua chini ya mlango. Unatafuta demu wa kupoza machungu anakuacha na gono then unamkumbuka mke wako unamfuata kwao unapigwa faini ya mbuzi then wanakurudishia mkeo baada ya kutuma watu wakuombee msamaha. Ukimpiga tena unaachwa mazima
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom