Wanawake wa Saudi Arabia waruhusiwa kusafiri bila kusindikizwa na Wanaume, Kuomba paspoti bila idhini ya Mwanaume

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,353
Wanawake nchini Saudi Arabia sasa wanaweza kusafiri nje ya nchi bila kusindikizwa na wanaume, limesema agizo la ufalme.

Chini ya sheria mpya iliyotangazwa ijumaa , mwanamke mwenye umri wa miaka zaidi ya 21 anaweza kutuma maombi ya paspoti bila idhini ya mlezi wa kiume.

Watu wazima wote wanaweza sasa kuomba paspoti na kusafiri hatua inayowapatia haki sawa na wanaume.

Agizo hilo la ufalme pia linawapa wanawake haki ya kuwasajili watoto wao wanapojifungua, kufunga ndoa au talaka.

Pia sheria hiyo mpya inazungumzia sheria za ajira ambazo zinapanua fursa kwa wanawake.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, raia wote wana haki ya kufanya kazi bila kukabiliwa na ubaguzi wowote kwa misingi ya jinsia, ulemavu au umri.

Hadi sasa, wanawake wa Saudia wamekuwa wakiomba ruhusa kutoka kwa mwanaume mlezi wa kiume, Mme , baba au ndugu mwingine wa kiume kuomba paspoti at kibali chochote cha kusafiri nje ya nchi.

Mtawala wa Saudia Mwanamfalme Mohammed bin Salman amelegeza masharti katika nchi hiyo kama vile kumzuwia mwanamke kuendesha gari kama sehemu ya juhudi kubwa za kufungua taifa hilo.

Mwaka 2016, alifichua mpango wa kufanya mageuzi ya kiuchumi ifikapo 2030, kwa lengo la kuongeza ushiriki wa wamawake kwa 30% kutoka 22%.

Hata hivyo kumekuwa na kesi kubwa za wanawake wanaotaka uhamiaji katika nchi kama vile Canada, kutokana na madai ya unyanyasaji wa kijinsia wakidai.

Mnamo mwezi January, Canada ilimpa hifadhi ukimbizi msichana Rahaf Mohammed al-Qunun mwenye umri wa miaka 18. Aliikimbia Saudi Arabia na kujaribu kutorokea nchini Australia. Alisababisha hali ya sintofahamu katika chumba cha hoteli iliyopo katika uwanja wa ndege katika mji mkuu wa Thailand Bangkok, ambako alikuwa akiomba msaada wa kimataifa.

Mashirika ya kimataifa mara kwa mara yamekuwa yakidai kwamba wanawake wanachukuliwa kama raia wa daraja la tatu nchini humo.
 
Slowly they are moving from "Objects of leisure" of men to women human beings!
 
... hatua muhimu sana hii kuelekea ustaarabu kamili kwa jamii ya wasaudia. Mwanamke alikuwa akiishi kama mtumwa katika nchi/familia yake mwenyewe; ilikuwa sheria ya kijinga kabisa! Profesa wa kike alihitaji kusindikizwa dukani na kijana mdogo wa kiume mchana kweupe!

Bado ule upumbavu wa "honor killing" ambao waathirika wakubwa ni wanawake; mwanamke anauwawa na familia kisa kaiaibisha familia kwa kukataa kuolewa na fulani kwa mfano! Ajabu sana hii kwa ustaarabu wa leo.
 
Waarabu ni washenzi sana. Wameona kuleta uislamu haitoshi wameleta mpaka sheria kandamizi mno kwa wanawake wa kiislamu. Unapishana na mwanamke kajifunika minguo kaacha macho tu yani ukimuona kwa mbali unaweza hisi msukule unakuja
 
Hawa watu tuko nao leo kimwili tu ila kifikra bado wapo karne ya nane. Very pathetic if not silly.
 
Mmarekani hapo anafurahia sana mipango yake inafanikiwa... anafanikiwa kuwabadilisha waarabu...

Ndiyo maana waKorea hawataki kusikia mambo ya magharibi wanasimamie yale yaliyo yao...

Cc: mahondaw
 
Mwanamke akiwa free bila kufatana na mwanaume level ya thamani yake inashuka. Fteedom zingine huwa zinakufanya uonekane ni mjinga tu. Alicho kikataza Mungu hata mkihalalishe kitawazuru tu.
 
Back
Top Bottom