Wanawake wa Saud Arabia sasa kuruhusiwa kwa mara ya kwanza kupiga kura na kugombea serikali za mitaa

The Dude

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
1,029
449
Sheria sasa itatambua na kuruhusu wanawake wa Saudi Arabia kupiga kura ama kugombea kwenye chaguzi za serikali za mitaa..Nimeshangaa kwa kweli..kumbe kipindi chote hawa wanawake hawana haki ya kushiriki uchaguzi!

Kwa taarifa nlizopata ni kwamba hata kuendesha magari wanawake wa Saudia hawaruhusiwi..strange!
 
Ndo manaake mkuu katika karne hii ya 21 kuna watu wananyimwa haki zao za kimsingi kwa mwamvuli wa dini hahahaha
 
Mi nadhani si dini sana bali ni sera za nchi tu..nimejiuliza mbona waislamu wengine nchi nyingine ikiwemo bongo wanavote na kucontest?Inapunguza uislamu wao na kuwa fanya less muslims?
 
hili suala la haki za wanawake katika uislamu ni contradictory, kwa sababu utaona haki anazopewa mwanamke katika nchi fulani ya kiislam inayotawaliwa kwa sharia ndio haki hizo hizo anazonyimwa mwanamke katika nchi nyingine ya kiislam inayotawaliwa kwa sharia! sasa huwa najiuliza hizi sharia zinatokana na mwongozo wa kitabu kimoja au tofauti? na kama ni kitabu kimoja kwanini wanatofautiana? na je saudi arabia kwa miaka yote hiyo ambapo wanawake walinyimwa haki hizo,je ilikuwa ni kwa mujibu wa sharia ipi? na sasa wanapowapa haki hizo ni kwa mujibu wa sharia gani? au sharia nazo zimepata 'agano jipya'?
 
Sheria sasa itatambua na kuruhusu wanawake wa Saudi Arabia kupiga kura ama kugombea kwenye chaguzi za serikali za mitaa..Nimeshangaa kwa kweli..kumbe kipindi chote hawa wanawake hawana haki ya kushiriki uchaguzi!

Kwa taarifa nlizopata ni kwamba hata kuendesha magari wanawake wa Saudia hawaruhusiwi..strange!

Duh walikuwa hawajapata hizo haki zao za msingi? Je kuendesha gari wamesharuhusiwa?
 
Saudi King Abdullah bin Abdelaziz has given the Kingdom's women the right to vote for first time in nationwide local elections, due in 2015. The king said in an annual speech on Sunday before his advisory assembly, or Shura Council, that Saudi women will be able to run and cast ballots in the 2015 municipal elections.

Abdullah says women will also be appointed to "join the all-male" Shura Council, which is selected by Abdullah.

Saudi Arabia held its first-ever municipal elections in 2005. The kingdom will hold its next municipal elections on Thursday, but women are not able to vote or run at this time.

Source: AP

kwa kuwa wanaongoza na dini yao,na dini yao inamregard mwanamke kama asset,na kiburudisho,ndio sababu wamekaaa muda mrefu bila kuwapa uhuru wa kupiga kura,swala la kuendesha gari bado hawajakubaliwa
 
hili suala la haki za wanawake katika uislamu ni contradictory, kwa sababu utaona haki anazopewa mwanamke katika nchi fulani ya kiislam inayotawaliwa kwa sharia ndio haki hizo hizo anazonyimwa mwanamke katika nchi nyingine ya kiislam inayotawaliwa kwa sharia! sasa huwa najiuliza hizi sharia zinatokana na mwongozo wa kitabu kimoja au tofauti? na kama ni kitabu kimoja kwanini wanatofautiana? na je saudi arabia kwa miaka yote hiyo ambapo wanawake walinyimwa haki hizo,je ilikuwa ni kwa mujibu wa sharia ipi? na sasa wanapowapa haki hizo ni kwa mujibu wa sharia gani? au sharia nazo zimepata 'agano jipya'?

Mkuu katika uislam pia kuna madehebu nadhani mawili au matatu Shia , Sun ..etc. nadhani hapo ndipo tofauti ya sharia inapotokea. Wajuzi watatujuza zaidi
 
Sheria sasa itatambua na kuruhusu wanawake wa Saudi Arabia kupiga kura ama kugombea kwenye chaguzi za serikali za mitaa..Nimeshangaa kwa kweli..kumbe kipindi chote hawa wanawake hawana haki ya kushiriki uchaguzi!

Kwa taarifa nlizopata ni kwamba hata kuendesha magari wanawake wa Saudia hawaruhusiwi..strange!
Mkuu hiz habari si za kweli hata kidogo, kwa sababu Saudia hakuna kitu kinachoitwa kupiga kura. Hakuna demokrasia hata kidogo si kwa wanawake tu bali hata wanaume hawapigi kura. Kuhusu wanawake kutoruhusiwa kuendesha magari hilo ni kweli kabisa. Wao wanadai ni haram kwa mwanamke kukaa kwenye usukani wa gari!!
 
Mwanangu dini zingine noma. Haki za watu wengine hazitambuliki kabisa. Thanks to Arab wakening!
 
Mkuu hiz habari si za kweli hata kidogo, kwa sababu Saudia hakuna kitu kinachoitwa kupiga kura. Hakuna demokrasia hata kidogo si kwa wanawake tu bali hata wanaume hawapigi kura. Kuhusu wanawake kutoruhusiwa kuendesha magari hilo ni kweli kabisa. Wao wanadai ni haram kwa mwanamke kukaa kwenye usukani wa gari!!

Ni habari ya kweli. King Abdulah ametangaza juzi hiyo kitu, ingawa utekelezaji wake unaweza usianze mara moja. Pamoja na hiyo wale jamaa wa SUNi aka msimamo mkali wanapinga suala hilo kwa kuwa wamezoea kuwakandamiza wenzao
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom