Wanawake wa mjini Mbeya na Mkorogo

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,855
8,253
Salaamu naam nipo Mbeya mjini kama wiki moja sasa ,kwa hakika nimeshtuka sana kuwaona akina dada, mama wengi hapa mjini wamejichubua, ukiangalia kwa asilimia kati ya wanawake 10 utakaokutana nao 7 wamejichubua ,hata wanawake watu wazima kwa kweli nimefadhaika sana na hali hiyo sijui ni kutoelewa madhara ya tokanayo na kutumia hizo dawa au ndo wenyewe wanaona ni fashion nashindwa elewa.

Pia kitu kingine nilichoona ni kuwa mkoa wa Mbeya ndi kitovu cha madawa ya kuharibu ngozi wenyewe wanaita vipodozi ,kwa kuwa mkoa unaopakana na nchi za Malawi na Zambia nchi ambazo hivyo vipodozi hupitia naona ndio sijui imekuwa sababu ya hawa mama na dada zetu kutumia hiyo mikorogo,ukiangalia hizo sura zilivyosinyaa na mtu kuwa na rangi mbili yaani usoni mweupe na miguuni mweusi,pia wengi wameota ndevu loh!.

Jamani dada na mama zangu wa Mbeya hiyo tabia tuiache ,urembo sio mkorogo,mikorogo ina madhara makubwa huleta kansa !
Loli nswigile mwe !
 
nafikiri nilikuwa peke yangu katika kushangaa hilo.

itabidi elimu itolewe kwa watu hao.na pia kukataza matumizi ya vipodozi hivyo maana wengine wanaungua kama wamechomwa na mafuta ya maandazi
 
Jamani hata mimi nawasikitikia,hayo unayosema ni kweli kabisaaa,Mbeya inaongoza kwa wamama wanaojichuna.

Halafu utakuta wengi wa wanawake hao wana ndevu,sasa pata picha mkorogo na ndevu itakuwaje.
 
jamani kwa asili mbeya kuna baridi kali, na asilimia ya watu wengi ni weusi, hivyo nao wanautaka weupe wafanyaje sasa?
 
jamani kwa asili mbeya kuna baridi kali, na asilimia ya watu wengi ni weusi, hivyo nao wanautaka weupe wafanyaje sasa?

Siamini, mpaka mpwa Geoff aje anithibitishie. Yuko vekesheni maeneo hayo. I hate mikorogo.

Wanawake natural huwa nawapendaga sana, ni vile tu wao hawajui.
 
Siamini, mpaka mpwa Geoff aje anithibitishie. Yuko vekesheni maeneo hayo. I hate mikorogo. Wanawake natural huwa nawapendaga sana, ni vile tu wao hawajui.
Huo ni ukweli,yani umesahau tukitoka Swanga huwa tunapitia mbeya kusalimi wajomba??

Na mie nimekulia kwa wajomba hapo mbeya,halafu nikabahatika kuukwepa mkorogo.
 
we si umemuona hata bahati bukuku?, hakua vile yule, weupe kaununua ule.
 
Huo ni ukweli,yani umesahau tukitoka Swanga huwa tunapitia mbeya kusalimi wajomba??Na mie nimekulia kwa wajomba hapo mbeya,halafu nikabahatika kuukwepa mkorogo.

yeah! That much I know! Si ndio maana nakupendaga? Au bado kujua?
 
Yeah juzi juzi nilikuwa vekesheni huko MBY dah si unajua mtu mweusi akijichubua anakuwa mbaya balaaa niliona wengi wanawake wamepaka au kunywa vidonge vya kutaka weupe hawajui siku hizi mablack beauty ndo wapo kwenye soko!
 
Jamani hata mimi nawasikitikia,hayo unayosema ni kweli kabisaaa,Mbeya inaongoza kwa wamama wanaojichuna.Halafu utakuta wengi wa wanawake hao wana ndevu,sasa pata picha mkorogo na ndevu itakuwaje.

Kale kausemi cha Juu fwanta chini Pwepsi bado kanaendelea
 
Yeah juzi juzi nilikuwa vekesheni huko MBY dah si unajua mtu mweusi akijichubua anakuwa mbaya balaaa niliona wengi wanawake wamepaka au kunywa vidonge vya kutaka weupe hawajui siku hizi mablack beauty ndo wapo kwenye soko!

Mpwa leo umeamka vizuri. Safari hii nimekugongea thenks. Kathibitishe.
 
Yeah juzi juzi nilikuwa vekesheni huko MBY dah si unajua mtu mweusi akijichubua anakuwa mbaya balaaa niliona wengi wanawake wamepaka au kunywa vidonge vya kutaka weupe hawajui siku hizi mablack beauty ndo wapo kwenye soko!

Aliye jichubua mie nasikiaga kinyaa utafikiri nyama live pwaa
 
Madhara ya kupakana na Malawi na Zambia. Vipodozi vingi vinatokea Zimbabwe na kuingia Mbeya kupitia boda ya Kyela (Malawi) na Tunduma (Zambia). Wafanyabiashara wengi wa Mbeya wanafanya biashara ya vipodozi na kwenda nchi hizo kununua na kuwamwagia dada zetu pale Mwanjelwa (kama bado ni soko).

Pia tatizo madreva wengi wa transit trucks (wajaluo) wanapenda mabinti weupe, na mabinti wa Mbeya ili wawachune hawa madereva kiraisi inabidi wajichubue. Si mnajua mwisho wa siku 'the end justifies the means'!!

Hivi hili suala la kwamba wanawake weupe ndo wazuri ni la kweli wadau????
 
Aliye jichubua mie nasikiaga kinyaa utafikiri nyama live pwaa


mie hakuna mtu anaenitia kinyaa kama mtu kuonekana uso mweupe, shingo njano mikono meusi, hivi kwanini hawatukuzi uumbaji wa muumba wao?halafu na wanavyobabuka cjui ungua mashavu na hizo cjui ni cream...kwa kweli wanachukiza basi tu hawajijui.
 
Back
Top Bottom