Wanawake wa CHADEMA wamejitolea kuwatoa gerezani wanasiasa wasio na hatia

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Mbele yetu tunawaona akina mdee na wenzake kama wasaliti wa nafsi zetu lakini tunasau sisi ni wasaliti wa Kwanza kutokea.

Toka uchaguzi umalizike tumekaa kimya tukiandika mitandaoni na kushangilia wanachofanya wanasiasa wa upinzani bila kutilia maanani kwamba wapo watu wapo gerezani kwa sababu tu yakututetea sisi.

Tukio la jana la Nasrat na wenzake kutoka gerezani na kufutiwa kesi kisha leo kuonekana viunga vya Bungo linatoa tafsiri kubwa sana kwa watu wanaotafuta haki ndani ya ardhi yetu.

Tusiwalaumu akina Mdee kwa sababu nao ni wanadamu, wanatupigania lakini wanapaswa kuwa na mbinu zaidi ya moja. Tunaweza jiuliza wasingekwenda bungeni Nini kingetokea chenye mabdailiko chanya kwetu? Ukweli ni kwamba hakuna ambacho kingetokea kwa sababu baadhi ya waliopewa dhamana hawana roho wa Mungu ndani yao bali kwao maslahi binafsi ni muhimu.

Leo hii tunaweza kuwalaumu CHADEMA lakini ukweli ni kwamba wamefanya mengi na wataendelea kufanya mengi ikiwemo kuiondoa CCM miyoyoni mwa watu.

Leo hii ukiitafuta CCM haionekani inaonekana dola, si kwa sababu nyingine bali ni kwa sababu ccm ilishashindwa kusimamia maslahi ya watu, ilishapoteza wanachama na wafuasi ilishapoteza misingi.

Niwaombe tuwaonee huruma Wafungwa waliopo gerezani ambao kutoka kwao si kwa nguvu ya sheria bali ni kwa maamuzi ya mtu mmoja. Tukiona Jambo hili katika angle ya kukosekana haki tutaelewa aina ya Vita wanayopigana wanawake wa viti maalumu wa nchi hii.

Naamini waliopo magereza wataachiwa na kurejea kwenye familia zao, naamini waliopo Zanzibar pia wanasubiri maalim seif aungane na watawala ili binadamu wachache na wasio na hati waweze kuwa huru ndani ya Taifa lao na kuzisimamia familia zao Kama ambavyo Mimi na wewe tunazisimamia familia zetu.

Hakuna Jambo la muhimu kuliko imani, ukiabudu Mali, madaraka,heshima ya Dunia ipo siku utaondoka na waliobaki wataacha kukuheshimu.

Huu tuseme ni ushindi wa wafungwa na mahabusu wa kisiasa ambao Uhuru wao unatokana na viumbe wachache wanaoamini pumzi wanatoa wao na bila wao hatuwezi kupumua. Tuendelee kupumua tukisubiri kipindi chao kipite maana tayari walishajitwalia imaya hii.

Haya yanayotokea hayaui upinzani yanaiua ccm kimya kimya.....ogopa kuwa na taifa la wenye njaa.
 
Mdee ni shujaa wangu, Kama Kuna mtu yupo msituni anapambana kutafuta tume ya uchaguzi mpya aseme tumwambie Halima na wenzake warudi nyuma, tangu mwanzo nilisisitiza viti maalumu waende bungeni Kama watanzania wanataka kujitetea endeleeni kujitetea mpate mnachotaka siyo kuwaita Halima wasaliti wakati wanasimama Kila siku tunawaona.
 
Katafute Utetezi mwingine, sisi sio wanaccm kila kifanywacho na viongozi wao wanashangilia. Ukienda kinyume na misimamo yetu sio mwenzetu. Kama ni kuwatoa hao watu wangeenda mahakamani, sio kuungana na shetani kwenye bunge la wamwaga damu na wezi wa kura. Halima Mdee amekuwa mbunge kwa miaka 15, kama kuwa mbunge ndio kuwatoa hao watu gerezani, wangeenda ambao hawajawahi kuwa wabunge kabisa. Sisi sio Mabwege wa hivyo dada
 
WaTanzania wengi walaaniwe kwa kutojitokeza kwa wingi kupiga kura na ndiyo maana wakaona haya na pia kukosa msukumo wa kufanya maandamano ya amani baada ya uchafuzi wa chaguzi za serikali za Mitaa November 2019 na ule uchafuzi wa Uchaguzi Mkuu wa 28 October 2020.

Siasa ni mchezo usiohitaji hasira na ni fluid kwa maana mazingira yake yanabadilika kufuatana na hali halisi ya wakati. WaTanzania hasa wanaoamini ktk Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu wengi wao kazi yao kubwa ni kuwa watazamaji tu bila kushiriki kufikia lengo na kile wanachoamini au kuwa na tamaa kitokee.

Lakini waTanzania hawa wanakuwa wepesi wa kulaumu wale majasiri wanaojitwisha kufanya maamuzi mazito kama makamanda hawa Tundu Antipas Lissu, Freeman Mbowe, Halima Mdee, Peter Msigwa, Mdude, Sugu n.k ambao waliwataka waTanzania wajitokeze kwa wingi kupiga kura na kukitokea uchafuzi wapige kelele, kuandamana maandamano yasiyo ya kikomo ya amani lakini hili pia limeshinda.
 
Back
Top Bottom