Wanawake,ukombozi wa ndoa/mahusiano yenu huu hapa(LADIES ONLY)

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,709
Inazidi kuthibitika sasa kwamba,wanawake huwa wanatoa harufu fulani chini ya kwapa zao ambayo huwafanya wanaume kuvutika kimapenzi kwao.Harufu hiyo ambayo inafahamika kama pheromone haisikiki katika hali ya kawaida.Utafiti wa hivi karibuni kama ulivyoripotiwa na jarida la Physiology and Behavior umeonesha wanawake ambao walipakwa kemikali ambayo inaipa harufu hiyo walitokea kufuatwa sana na wanaume kuliko wakati walipokuwa hawajapaka kemikali hiyo.Kufuatwa kwao na wanaume kuliongezeka karibu mara saba zaidi kuliko ilivyokuwa kabla.Wanawake hao waliripoti kwamba,walibusiwa zaidi,walitongozwa zaidi na waliombwa urafiki zaidi na walijikuta wakikutana kimwili na wapenzi wao mara nying zaidi.Mmoja kati ya 36 waliofanyiwa utafiti aliripoti kwamba alipopaka kemikali hiyo,rafiki yake wa kiume alifanya nae mapenzi mara 4 kwa wiki ukilinganisha na mara moja ya awali.Harufu hii ambayo si mwanaume au mwanamke anaeweza kuihisi moja kwa moja bali kwa kupitia viungo maalumu vilivyo juu ndani ya pua,ina nguvu sana ya kumvuta mtu kimapenzi.Kama wataalam wameweza kutengeneza kemikali ya kuiga harufu hii,ni wazi wanawake watakuwa tayari kuinunua na kuitumia endapo itaingia sokoni!!
 
Aisee!

Nllitaka kuchangia kitu lakini kumbe hapa ni kwa wanawake tu.

Ila Angalizo: Hii thread wakishaisoma walengwa idiliti kabla mabintyi zangu hawajaisoma. Wasije wakaniletea foleni ya vidume nyumbani nikaua watoto wa watu bure.
 
Sasa kipi ni kipi, harufu ya pua ama makwapa?
Hebu edit kwanza boss usiibie watoto wa watu buree!
 
Babu ODM,usihofu,naamini malezi yako yako poa!Wataju kwamba ukifika wakati muafaka na kwa watu maalum!
 
harufu ya hiyo kemikali ni kama harufu ya kikwapa? kama ndiyo uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Kila kitu fake hadi kwenye harufu watu waliyopewa na Mungu? Waambie wasipendelee perfumes wakati fulani fulani ili hiyo harufu waliyopewa bure ijitokeze. Kila kitu fake? Nywele, kucha, rangi, makalio, sasa hadi harufu! Napita tu.
 
Research kama hizi hua zinakua zimewajenga hao wanawake Mentally, physically na hata Chemically.... Angalia tofauti....

Mwanamke ambae anahusika katika Research

Yupo alert tokana na hilo zoezi... Ni lazima atafanya usafi extra ya sehemu zake zoote za muhimu (hata yule mzembe na mchafu); kwa kujua kua aweza vutia wanaume. Unconsiously anakua more makini katika muonekano aonekane mrembo na nguo zile za kupendeza mwili wake, anakua yupo almost horny for a Kiss and a touch sababu kisha jiandaa for positive results... Yoote haya yanasomeka kwa Mwanaume wake, ama wanaume walomzunguka.... inanya huyo mwanaume kutaka kua karibu tokana na uitikio wa huyo mwanamke.... na kwa vovote the lady is so ready to sex sababu kisha kua psychologically programmed kua anavutia wanaume hivo huenda all the way.... For she is confident kua avutia. Take note; wanawake mara nyingi huzungusha kulala na mwanaume mara ya kwanza sio sababu hataki.... Lah! Ila sababu she is not confident kama atavutia kwa mwanaume wake ama lah!


Mwanamke ambae hayuko kwenye Research.

Inshort she is her normal self, not ready, she is not looking forward to kutongozwa... Saa ingine a bit careless on her usafi. She is not in the mood na it is easy for a man to tell, na saa ingine guys wachoka kila siku a demand kiss na sex from a lady hadi kumuanza aona uvivu. badala ya sex for times a week inakua once in two weeks.... Take note: Sex, mvuto, connection na chemistry kati ya wanawake na wanaume mara nyingi inakua nurtured.... haiji from nowhere....
 
Kwel hiyo harufu naijua nimeshamsifiaga dia wangu akadhani namtania
 
Kwel hiyo harufu naijua nimeshamsifiaga dia wangu akadhani namtania TEH TEH TEH RESEARCH BWAANA.
 
Dada Asha,nimependa maelezo yako kwa 40% tu,nimesema hayo coz hizo sababu zinachangia kwa kiwango kidogo kiasi hicho tu!
 
Kila kitu fake hadi kwenye harufu watu waliyopewa na Mungu? Waambie wasipendelee perfumes wakati fulani fulani ili hiyo harufu waliyopewa bure ijitokeze. Kila kitu fake? Nywele, kucha, rangi, makalio, sasa hadi harufu! Napita tu.
yaani kama huyo dada wa kwenye avatar yako hata sihitaji harufu ya ziada! hivyo alivyo naua mara nane kwa wiki! oooooh samahani kumbe ni kwa wanawake tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom