Wanawake Tanzania ni Duni/Dhaifu Kiongozi, Kama Si Duni/ Dhaifu na Wana Uwezo Sawa na Wanaume, Viti Maalum vya Nini?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,179
Wanabodi,
1576229551720_0_IMG-20191213-WA0008.jpg


Nimeiangalia hii picha ya wanawake hawa wa wenzetu, na age zao, nikajiuliza sana kuhusu sisi Tanzania na wanawake wetu katika nafasi za uongozi wa kisiasa, tatizo ni nini?.

Jee wanawake wetu Tanzania ni duni au dhaifu Kiongozi wa siasa?. Kama wanawake wetu si duni na si dhaifu na wana uwezo wa uongozi sawa na wanaume, hizi nafasi za Viti Maalum ni za nini?, je Tanzania tumefika mahali nafasi hizi za Viti Maalum zifutwe?

Hivi hawa baadhi ya wanawake wetu wenye nafasi za juu za uongozi wa kisiasa, wamepata nafasi hizo by deserving au kwa kubebwa na affirmative action?.

Kama watu wawili mna uwezo sawa, kwa nini mmoja afanyiwe upendeleo wa kijinsia kwasababu tuu ya jinsia yake?.

Wanawake ni mama zetu, shangazi zetu, wake zetu, wapenzi wetu, dada zetu, watoto wetu, ni wenzetu na tunawapenda sana, lakini huu upendeleo kwa wanawake lengo lake ni nini haswa, jee hapa tulipofika, bado wanawake wetu wanahitaji upendeleo?.
Paskali

Tuacheni Kumlaumu Rais Kuteua Wanaume, TZ Hatuna Wanawake Wenye Sifa na Vigezo vya Kuteuliwa! - JamiiForums

Siku ya Wanawake Duniani: Je, Tuna Wanawake Wenye Sifa za Presidential Material?! - JamiiForums

Siku ya Wanawake Duniani: Tuwakumbuke Top Ten Wanawake Wakurugenzi Wakuu Wa Taasisi Kubwa - JamiiForums

Je, Wabunge Viti Maalum ni wa kubebwa? Mnaonaje iwe ni awamu moja tuu kisha waendeni jimboni, kupisha wengine, au waendelee kubebwa tu?

Wanawake Tanzania ni Duni/Dhaifu Kiongozi , Kama Si Duni/Dhaifu na Wana Uwezo Sawa na Wanaume, Viti Maalum Vya Nini?
 
Kwa mtazamo wa kawaida tu, kama pande mbili zina uwezo unaofanana katika kutekeleza majukumu hususani hayo ya kiuongozi, basi hakuna ulazima wowote wa kufanyika kwa upendeleo kwa upande mmoja dhidi ya mwingine.

Kwahiyo hayo yote yanafanyika kutokana na huo mtazamo kwamba upande mmoja ni dhaifu kuliko mwingine.

Tujikumbushe maneno ya Mwanafalsafa Aristotle aliyewahi kusema;

"The worst form of inequality is to try to make unequal things equal."
 
Asikudanganye mtu, hata hao wa Finland hawajafikia hapo by merit, ni quota system, na mara nyingi hizo nchi hufanya hivyo ili kutafuta sifa kama unayowapa ili waonekane wamefikia ,,usawa” wa kijinsia, ni kama Barack Obama tu USA from Mr.nobody to senator temu moja to POTUS, kila kitu kiko planned, tunalishwa matango pori tu.
 
viti maalum ni matokeo ya mfumo dume. jamii yetu inaamini mwanamke ni mtu au kitu dhaifu. wakati mwingine tunatumia maandiko ya dini tulizoletewa kuamini dhana hii. bahti mbaya sana hata baadhi ya wanawake wenyewe haukosi kuwasikia wakibwabwaja ‘mwanaume ndiyo kichwa cha familia’ kupigilia msumari wa moto.

kukomesha suala hili kwanza lazima afrika ijikomboe kiutawala. wanawake wagombee nafasi za uongozi na washinde chaguzi za kidemokrasia.

vilevile, afrika lazima iachane na siasa za ubabe na vita. viongozi takataka kama museveni, paul biya, kagame, nkurunzinza and the like wakome kutawala wawaache wananchi wachague viongozi wanaowataka. afrika ikijiongoza kidemokrasia siasa za mabavu na vita vitakoma kwa kuwa mambo haya huchochea dhana kwamba ‘pakitokea vurugu wanaoteseka ni ‘wanawake’ na watoto.

bullying: hili nalo ni tatizo jingine. matukio ya kubakwa kwa watoto wa kike, kusifiwa au kubezwa sababu ya maumbile yao all this sort of shit must stop for africa women to prosper.
 
Ukitaka kuelewa kwa usahihi jambo hili unatakiwa uangalie maisha kwa ujumla wake na kihistoria. Tangu zamani sana wanawake hawakutendewa haki kijamii. Waliachwa nyuma sana kiuchumi ndani ya familia zao na kijamii wa ujumla. Na hili ni jambo ambalo halipo kwetu tu bali hadi leo Ulaya na Marekani bado wanapambana na hili tatizo. Vipato vya wanawake Ulaya bado viko chini sana hata pale ambapo kitaalam kazi wanazofanya zinafanana kabisa.

Ukiliangalia kwa undani sana utaona kuwa hizi tofauti zilikuwa kubwa sana wakati wa vita kuu za dunia. Na hata mpaka leo hii nchi yoyote ikiwa kwenye vita wanawake huwa hawaonekani kwenye uongozi wa nchi iliyokosa amani. Lakini pindi kipindi cha utulivu kikiisha rejea na kuwepo kwa muda ya kutosha, basi wanawake huwa wanaanza kuonekana kwenye juhudi za kimaendeleo.

Kinachofanyika sasa hivi kuweka kiasi fulani cha upendeleo ni juhudi za makusudi ili kuwahamasisha kushiriki zaidi katika uongozi na uchumi wa nchi. Lazima pia kutafakari na kukubali mipango ya Mwenyezi Mungu, kwamba katika hali ya kawaida, karibu katika kila Taifa idadi ya wanawake huwa kidogo ni kubwa zaidi ya wanaume, kwahiyo kutokuwahusisha katika ujenzi wa Taifa ni kupoteza nguvu kazi. Inathibitika wazi katika nchi kadhaa duniani kuwa pale wanaposhiriki na kupewa nafasi hufanya vizuri sana haswa katika uongozi wa kisiasa na kukuza uchumi katika jamii hata kupita wanaume. Tumesikia watu wakisema ukimuelimisha mwanamke uwe na hakika kuwa familia yote itaelimika. Na hapo ndipo ilipo "strength" ya wanawake.

Taifa lolote linavyoendelea kustaarabika huzinduka na kuanza kuukiri ukweli huo na kuweka mikakati ya makusudi kabisa ya kuwa "encourage" wanawake kushika nafasi za uongozi.
 
wanawake Wa Tanzania hovyo kabisa kwenye uongozi si unaona NDALICHAKO Anavyoigeuza mfumo Wa elimu yetu Kama SHUKA LA KULALIA Leo hivi kesho vile
 
Viti maalumu vikitutwa huku chadema itakuwaje hatuta baki na wabunge 2020

State agent

Sent using Jamii Forums mobile app
hujui hata asili ya viti maalum umekalia majungu ya chadema tu mpuuzi wewe. kwa taarifa tu hayo ni makubaliano ya UN kwamba kuongeza idadi ya wanawake kwenye uwakilishi pawe na viti maalumu kwa kujua hilo ndo maana rwanda wao wanatenga majimbo kabisa kwamba hayagombewi na mwanaume wanashindana wanawake tuu. we kwa akili zako kama sio viti maalumu wale kina vulu wangemshinda nani jimboni?
 
I think recognizing how hard kuwa mwanasiasa ..kusimama majukwaani ku convince watu wakukubali sio kazi rahisi..LOL plus wider public misconception that ubunge ni complex job, wengi katika jimbo lako wanataka maendeleo wakati kuna limited resources...you need to be strong ,both mentally and physically fit..lol sasa sisi wanawake tuko vulnerable to be underpresented in Parliament,..so ku bring up equality ndio tunapewa viti maalumu...tukaringishie Mashosti😁😁😁😁..Pasko nipigie pande niwe mbunge wa viti maalumu basi..😁
 
Hivi ndivyo tunavyowatayarisha vijana wetu, hasahasa mabinti zetu, kuwa viongozi bora:




1576239073654.png


1576239350491.png




1576239911403.png


N.K., N.K., N.K.
 
Ukisha kuwa ccm lazima akili ife tu! Ile lack of independent thinking ni tatizo kubwa. Hao wazungu hali unayoisifia haikuja overnight, it took centuries kufikia ukombozi wa wanawake kama ilivyo sasa in the whole of western europe and america.Kama unavyoona Jiwe anafanya mambo ya ajabu na wewe mnakuwa praise team, the same applies to our women in the male dominated society, as Jiwe dominates the constitution and you celebrate what he is doing. The same scenario ihamishie katika hali ya wanawake nchini mwetu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom