Wanawake Tanzania ni Duni/Dhaifu Kiongozi, Kama Si Duni/ Dhaifu na Wana Uwezo Sawa na Wanaume, Viti Maalum vya Nini?

Nafasi za kisiasa kushikwa na wanaume ni uboya hizi ni kazi za wanawake, unakuta mbunge kama Msukuma eti anaonekana jembe kuliko mwanamke engineer na daktari, huu ni upuuzi mkubwa na kuna ubunge wa kuteuliwa rais ana viti kumi vya kumpa amatake na kuna wanaume wamepewa nao ni dhaifu?
 
Tatizo P letu hapa ni utamaduni tu. Wanawake bado hawana haki sawa haswa kwenye uongozi. Angalieni mfano mdogo tu watoto wa miaka 15 wawili wafanye mapenzi na msichana akapata mimba utamaduni wetu na mila nyingi tuta mtenga msichana kumfukuza shule lakini mtoto wa kiume ataendelea. Hata watoto bado hawana akili vizuri wote wamefanya makosa lakini utamaduni wetu ndiyo tatizo. Hao uliowaweka hebu angalia huko kwao kama wameshafukuza mtoto wa kike shule kwasababu ya mimba ya kumwacha mtoto wa kiume shule na ujue hawa ndiyo wale tunaosema wana utamaduni mbaya!.

Hata kwenye jamii zetu angalia Mama na Baba nani anafanya kazi zaidi. Wazee wengi ni ubosi tu hawapiki, hawafanyi usafi, wengine hata kulima hawalimi na isitoshe wengine wanakuja nyumbani jioni baada ya kupitia vilabuni wakiwa walevi. Huku nyumbani hajaacha hata pesa anataka akute chakula, nyumba safi , watoto wameangaliwa n.k. Haya yote ni utamaduni mbovu na wa kizamani. Wenzetu ni team work wote wanasaidiana kwenye shughuli za maendeleo Mama na Baba na nguvu za wawili ndizo zinasadia maendeleo.

Tukiona wabunge na viongozi wa kike wachache tujiulize sababu ni zipi maana si kweli kwamba wanaume wana akili zaidi, si kweli kwamba wanaume ni wachapakazi zaidi na si kweli kwamba wanaume ni wengi zaidi. Lakini kingine kwasababu ya utamaduni hata wanawake wakifanikiwa hatujui mfano wafanya biashara wengi Arusha ni wanawake lakini watu hawajui hilo maana tulishajenga picha fulani kwenye akili zetu. Na hata nchi zilizoendelea bado wanawake wanakuwa wananyanyaswa hivyo itachukua generation nyingine kurekebishika
 
Ni wanawake wachache sana wenye uwezo wa kusimama mbele za watu na kuhutubia , kuvumilia matusi na vijembe, wenye ujasiri huo wengi wao ni ma "tomboy" (wana tabia za kidume dume)
 
Na vile vile wanaume wengi hawapendi wake zao washiriki siasa , wanawake wakishaukwaa ubunge hawaheshimu waume wao, na kwenye siasa kuna uhuni mwingi,
 
na vile vile wanaume wengi hawapendi wake zao washiriki siasa , wanawake wakishaukwaa ubunge hawaheshimu waume wao, na kwenye siasa kuna uhuni mwingi,
Uhuni huo huwa unaisha kwa wakati jinsi wanawake wanavyoongezeka katika siasa. Hii movement iliyoanza huko Marekani #MeToo* imeleta balaa kwa miamba wa kujiamini, wanasiasa na matajiri wamepukutika imepelekea hata wengine kujinyonga wakiwa mahabusu. Hivyo ndivyo jamii hustaarabika.
 
Spika mstaafu wa bunge mama Makinda amesema wakati umefika wa kuweka ukomo wa mbunge wa viti maalum kuhudumu kwa upendeleo huo.

Makinda amedai utaratibu wa viti maalum ulianzishwa ili kuwaandaa wanawake waweze kwenda kugombea majimboni lakini sasa mbunge anakaa zaidi ya miaka 10 katika viti maalum hii si sawa. Hawa ving'ang'anizi wanawanyima fursa wanawake wengine walio wengi.
Yaelekea Makinda anasoma jf, hili aliliona humu
last week

Je, Wabunge Viti Maalum ni wa kubebwa? Mnaonaje iwe ni awamu moja tuu kisha waendeni jimboni, kupisha wengine, au waendelee kubebwa tu?

Wanawake Tanzania ni Duni/Dhaifu Kiongozi , Kama Si Duni/Dhaifu na Wana Uwezo Sawa na Wanaume, Viti Maalum Vya Nini?

P
 
Marekani wanawake walianza kupiga kura zaidi ya miaka 200 tokea uhuru wao.

Miaka 100 tena baadae ndipo Hillary Clinton akapitishwa kupeperusha bendera na kama sio Russian intrusion bila shaka leo she could be madam President.

It won't be easy.

Mama Makindaa awaache dada zetu, mama zetu wainjoy viti maalum. Kuogombea kutoka jimboni sio jambo jepesi.

Wewe mwenyewe kwenye bandiko lako uchaguzi wa Busanda ilionesha wazi kuwa Lolensia Bukwimba bila msaada wa JPM akiwa waziri, alikuwa ashashidwa kwenye uchaguzi mdogo.
 
Wanabodi,
View attachment 1290764

Nimeiangalia hii picha ya wanawake hawa wa wenzetu, na age zao, nikajiuliza sana kuhusu sisi Tanzania na wanawake wetu katika nafasi za uongozi wa kisiasa, tatizo ni nini?.

Jee wanawake wetu Tanzania ni duni au dhaifu Kiongozi wa siasa?. Kama wanawake wetu si duni na si dhaifu na wana uwezo wa uongozi sawa na wanaume, hizi nafasi za Viti Maalum ni za nini?, je Tanzania tumefika mahali nafasi hizi za Viti Maalum zifutwe?.

Hivi hawa baadhi ya wanawake wetu wenye nafasi za juu za uongozi wa kisiasa, wamepata nafasi hizo by deserving au kwa kubebwa na affirmative action?.

Kama watu wawili mna uwezo sawa, kwa nini mmoja afanyiwe upendeleo wa kijinsia kwasababu tuu ya jinsia yake?.

Wanawake ni mama zetu, shangazi zetu, wake zetu, wapenzi wetu, dada zetu, watoto wetu, ni wenzetu na tunawapenda sana, lakini huu upendeleo kwa wanawake lengo lake ni nini haswa, jee hapa tulipofika, bado wanawake wetu wanahitaji upendeleo?.
Paskali



Norway: share of women in the Parliament 1945-2017 | Statista

Norway kupitia mfumo wao wa bunge toka 1945 mpaka uchaguzi wa mwisho unafanyika 2017 walikuwa hawajatoboa 50/50.

Mama Makinda pia ajuzwe kunaga ubaga, kwenye Uspika kama sio JK kusema safari hii ni zamu wa mwanamke wakasimama na mzee wa Standard and Speed alikuwa hatoboi.
 
Marekani wanawake walianza kupiga kura zaidi ya miaka 200 tokea uhuru wao.

Miaka 100 tena baadae ndipo Hillary Clinton akapitishwa kupeperusha bendera na kama sio Russian intrusion bila shaka leo she could be madam President.

It won't be easy.

Mama Makindaa awaache dada zetu, mama zetu wainjoy viti maalum. Kuogombea kutoka jimboni sio jambo jepesi.

Wewe mwenyewe kwenye bandiko lako uchaguzi wa Busanda ilionesha wazi kuwa Lolensia Bukwimba bila msaada wa JPM akiwa waziri, alikuwa ashashidwa kwenye uchaguzi mdogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Freddie Matuja, kwanza nimefurahi kwa reference yako ya Mhe. Lolensia Bukwimba, ni kweli mwanzo kwenye ule uchaguzi mdogo alitoboa kwa kubebwa na JPM, tena kampeni ziliendeshwa kwa lugha ya Kisukuma mwanzo mwisho, bila hivyo asinge toboa haswa kwa kuzingatia Wasukuma ni moja ya makabila yenye male chauvinism na kudharau wanawake. Lakini baada ya kuingia Bungeni, akajenga uwezo, 2010 na 2015 akasimama mwenyewe na akatoboa.

Hivyo Mama Makinda ana hoja ya msingi sana, lengo la viti Maalum liwe ni kujenga tuu uwezo kwa a single term, kisha waende jimboni na sio kubebwa na kuendelea kubebwa tuu!.
P
 
Leo siku ya wanawake, wanawake wetu, angalieni wenzenu, sisi tunakwama wapi?.
P
 
: Wabunge wa Viti Maalum

1. Maida Hamadi Abdallah
2. Munde Tambwe Abdallah
3. Rose Vicent Busiga
4. Mwantum Dau Haji
5. Agnes Elias Hokororo
6. Dkt. Christine Gabriel Ishengoma
7. Zainabu Athumani Katimba
8. Fakhari Shomari Khamis
9. Mariam Nassoro Kisangi
10. Amina Iddi Mabroud
11. Catherine Valentine Magige
12. Maryprisca Winfred Mahundi
13. Angelina Malembeka
14. Agnes Mathew Marwa
15. Mary Francis Masanja
16. Aysharose Ndoholi Mattembe
17. Lucy Thomas Mayenga
18. Taska Restituta Mbogo
19. Subira Khamis Mgalu
20. Neema William Mgaya
21. Easter Lukago Midimu
22. Jackline Ngonyani Msongozi
23. Bupe Nelson Mwakang'ata
24. Maryam Azan Mwinyi
25. Shally Joseph Raymond
26. Oliver Danieli Semuguruka
27. Juliana Daniel Shonza
28. Fatma Hassan Toufiq
29. Rose Cyprian Tweve
30. Martha Jachi Umbulla
31. Tecla Mohamed Ungele
32. Mwantum Mzamili Zodo
33. Wanu Hafidh Amei
34. Jackline Kainja Andrea
35. Martha Festor Bariki
36. Tauhida Galos Cassian
37. Josephine Thabita Chagula
38. Pindi Azara Chana
39. Ghati Zephania Chomete
40. Suma Ikenda Fyandomo
41. Martha Nehemia Gwau
42. Saada Mansour Hussein
43. Asha Abdallah Juma
44. Dkt. Rita Enespher Kabati
45. Santiel Eric Kirumba
46. Ester Edwin Maleko
47. Janeth Mauris Masaburi
48. Hawa Chakoma Mchafu
49. Minza Simon Mjika
50. Bernadeta Kasabango Mushashu
51. Neema Mwandabila
52. Nora Waziri Mzeru
53. Mariamu Ditopile Mzuzuri
54. Irene Alex Ndyamkama
55. Josephine Genzabuke
56. Mariamu Madalu Nyoka
57. Asya Sharifu Omar
58. Zulfa Mmaka Omary
59. Maimuna Ahmad Pathan
60. Regina Ndege Qwaray
61. Kabula Enock Shitobelo
62. Zaytun Seif Swai
63. Mwanaisha Ulenge
64. Anastazia James Wambura
65. Zuwena Athumani Bushiri
66. Aleksia Asia Kamguna
67. Dkt. Christine Christopher Mnzava
68. Nancy Hassan Nyarusi
69. Husna Juma Sekiboko
70. Amina Daud Hassan
71. Furaha Ntengo Matondo
72. Janeth Elias Mahawanga
73. Stela Alex Ikupa
74. Hadija Shabani Taya
75. Ummy Hamisi Nderiananga
76. Bahati Keneth Ndingo
77. Najma Murtaza Giga
78. Juliana Didas Masaburi
79. Lucy John Sabu
80. Asia Abdukarimu Halamga
81. Judith Salvia Kapinga
82. Ng'wasi Damas Kamani
83. Sylvia Francis Sigula
84. Munira Mustafa Khatibu
85. Latifa Khamis Juakali
86. Amina Bakari Yussuf
87. Amina Ali Mzee
88. Dkt. Paulina Nahato
89. Dkt. Thea Medard Ntara
90. Mwanaidi Ali Khamisi
91. Dkt. Alice Karugi Kaijage
92. Janejelly James Ntate
93. Neema Kijichi Lugangira
94. Khadija Hasani Aboud
 
Usiwe na haraka, hii process inaitwa affirmative action ili kupromote makundi ya watu ambo waliachwa nyuma na mfumo. Imetokea sehemu nyingi sana duniai - hata huko Norway unakotoa mfano huo, na inapofikia makundi yote yako level ground ndipo inafutwa. Kwa Tanzania wanawake wengi waliachwa nyuma kielimu, wengi wao wakiwa wanatayalirishwa kuolewa na kuzaa tu, kwa hiyo waliofuata hawakuwa na role models kielimu na kimadaraka. Sasa hivi tumepiga hatua kidogo lakini bado, tunahitaji kama miaka 15 hivi ili tuwe level ground; Magufuli alifanya jambo zuri sana kumteua mwanamke kuwa Makamo wa rais ili kuharakisha mwendo huo; angalia siku hizi akina Ummy Mwalimu wanavyochachafya kiutendaji.
 
Wanabodi,
View attachment 1290764

Nimeiangalia hii picha ya wanawake hawa wa wenzetu, na age zao, nikajiuliza sana kuhusu sisi Tanzania na wanawake wetu katika nafasi za uongozi wa kisiasa, tatizo ni nini?.

Jee wanawake wetu Tanzania ni duni au dhaifu Kiongozi wa siasa?. Kama wanawake wetu si duni na si dhaifu na wana uwezo wa uongozi sawa na wanaume, hizi nafasi za Viti Maalum ni za nini?, je Tanzania tumefika mahali nafasi hizi za Viti Maalum zifutwe?

Hivi hawa baadhi ya wanawake wetu wenye nafasi za juu za uongozi wa kisiasa, wamepata nafasi hizo by deserving au kwa kubebwa na affirmative action?.

Kama watu wawili mna uwezo sawa, kwa nini mmoja afanyiwe upendeleo wa kijinsia kwasababu tuu ya jinsia yake?.

Wanawake ni mama zetu, shangazi zetu, wake zetu, wapenzi wetu, dada zetu, watoto wetu, ni wenzetu na tunawapenda sana, lakini huu upendeleo kwa wanawake lengo lake ni nini haswa, jee hapa tulipofika, bado wanawake wetu wanahitaji upendeleo?.
Paskali

Tuacheni Kumlaumu Rais Kuteua Wanaume, TZ Hatuna Wanawake Wenye Sifa na Vigezo vya Kuteuliwa! - JamiiForums

Siku ya Wanawake Duniani: Je, Tuna Wanawake Wenye Sifa za Presidential Material?! - JamiiForums

Siku ya Wanawake Duniani: Tuwakumbuke Top Ten Wanawake Wakurugenzi Wakuu Wa Taasisi Kubwa - JamiiForums

Je, Wabunge Viti Maalum ni wa kubebwa? Mnaonaje iwe ni awamu moja tuu kisha waendeni jimboni, kupisha wengine, au waendelee kubebwa tu?

Wanawake Tanzania ni Duni/Dhaifu Kiongozi , Kama Si Duni/Dhaifu na Wana Uwezo Sawa na Wanaume, Viti Maalum Vya Nini?
Hivi viti maalum, vinatuletea songombingo, napendekeza vifutwe!.
P
 
Back
Top Bottom