Wanawake sio watu wazuri, wameondoa uhai wa baba yangu mzazi

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,428
Hawa wanawake tupo nao katika maisha yetu ya kila siku,i la ni viumbe vinavyotusababishia matatizo makubwa sana kwenye maisha.

Hawa wanawake wanatuwekea wanaume limbwata tunakuwa kama machizi na kudharau ndugu zetu kisa wao.

Hawa wanawake tukiwa na mali wanatuua na kusabisha mgogoro mkubwa katika familia na wanaukoo (rejea inshu ya marehemu bilionea Msuya na kinachoendelea huko Arumeru chini ya DC Muro).

Hawa wanawake tunajitoa kwao tunawasaidia kama kuwasomesha na kuwafanyia mambo mengine ya msingi lakini mwisho wa siku wanatuumiza.

Samson aliteswa na kuuawa kwa sababu ya Delilah.

Hivi sasa nchi yetu imekumbwa na matukio mengi ya vijana kijiua na kuua wapenzi wao wa kike kisa mapenzi.

Lakini nataka kusema wanawake wengi ni mashetani sana.

Nimempoteza baba yangu miaka 9 iliyopita chanzo mwanamke, tena mwanamke aliyempata baada ya mama yangu kufariki ila kwa tamaa zake za mali na roho yake mbaya, akamuua mzee wangu kwa kumchoma kitu chenye ncha kali na kuharibu utumbo mpana wa baba.

Uchafu ukasambaa mwilini dingi kafichwa ndani. Baada ya kaka zangu kuona mbona mzee hatumuoni wakamfuatilia nyumbani kwake wanamkuta mzee hali mbaya tumbo limejaa, mke kakimbia na mwanae wa kiume walioshiriki tendo lile.

Fasta mzee akakimbizwa hospital kubwa baada ya kupimwa ikaonekana mzee kachomwa kitu chenye ncha kali na utumbo ushaharibika hivyo awekewe utumbo bandia.

Operation ikafanyika fasta mzee akawekewa utumbo bandia. Ila kama mnavyojua tena haya maisha mzee wangu anatoka chumba cha upasuaji hakuwa na fahamu.

Kafika wodini hakukaa muda mrefu sana alizinduka mara moja alipolala tena basi akalala milele na kuniacha yatima. Chanzo kikuu cha kifo chake ni mwanamke.

Nawasihi wanaume wenzangu kuwa makini na hawa wanawake. Tusitumie gharama kubwa kuwapata kwani tukiwapata ni starehe ya muda mfupi ambayo ukiifikiria utafanya maamuzi magumu na mwisho utaishia jela na kukosa uhuru wako na kuwaacha wapendwa wako hasa baba na mama na watoto wako uraiani.

Tuwe makini na wanawake.

NB: Yule mama alishirikiana na mwanae wa kumzaa kumuua baba yangu ila mwanae alikamatwa, mama yake akakikimbia. Baada ya kupita miezi kadhaa yule kijana alifariki akiwa jela, nikapigiwa simu kupewa taarifa so kijana akazikwa na serikali kupitia jeshi la magereza. Mama yake hadi sasa sijamtia machoni.
 
Pole sana mkuu hadithi yako inasikitisha,Ila bado napata mashaka na simulizi yako,siku zote ulikuwa wapi usituhadisie paka leo baada ya kutokea matukio mawili matatu yanayo fanana na hii story yako ndio uje uandike hapa hii story yako
Naona kama unataka kutudanganya vile.

Ila pole kwa kuwa Yatima Mkuu.
 
Mmmmh kama ingekua kisa mali sidhani kama angejaribu kumuua kizembe hvyo...hlf mli angeipataje? Kwanini wakimbie? Ushawah kuwaza labda mzee alikua abusive sana so wakaamua kumfungia kazi ????
 
Sorry for your loss...
Lakini usigrneralize mambo mkuu.. hata wanaume wanaoua wanawake kwa vipigo wako kibao hadi ilishazoeleka... wanaume wansosababisha ulemavu kwa wanawake kisa vipigo wapi wengi zaidi ya wanawake wanaopiga waume zao...

Huyo mama yako wa kambo kafanya kitendo cha kikatiri lakini sio kwamba wanawake wote ni katiri..
 
Mmmmh kama ingekua kisa mali sidhani kama angejaribu kumuua kizembe hvyo...hlf mli angeipataje? Kwanini wakimbie? Ushawah kuwaza labda mzee alikua abusive sana so wakaamua kumfungia kazi ????
Kwani Wewe huwa una uaje mpaka huyu awe ameua kizembe?
 
Kwani Wewe huwa una uaje mpaka huyu awe ameua kizembe?
Afu kuna mwanaume anasema Nina mke asee so sad anawaambia nampenda sana shemeji yenu (uchizi sio kuokota makopo kuna watu wanatembea vzr ila ni machizi) so sad Kwa mumewe.................................. Over
 
Pole sana mkuu hadithi yako inasikitisha,Ila bado napata mashaka na simulizi yako,siku zote ulikuwa wapi usituhadisie paka leo baada ya kutokea matukio mawili matatu yanayo fanana na hii story yako ndio uje uandike hapa hii story yako
Naona kama unataka kutudanganya vile.

Ila pole kwa kuwa Yatima Mkuu.
We dogo au wewe ndiyo mama ake wa kambo unamuuliza maswali ili aache kukutafuta? Mleta uzi tongoza huyu akutumie picha umfananishe na mama yako.
 
Haiingii akilini.

Unaua kisa mali. Halafu unakimbia?

Lengo lako ni kuua. Unamficha ndani huyo mtu ili iweje? Kwanini usimmalizie?

Unaua kisa mali. Kwanini utumie mbinu ambayo itaacha maswali? Wataona utumbo ulipasuka, itaanza kuulizwa ilikuaje mpaka utumbo kupasuka na blah blah nyingi zitakazokuchelewesha kumiliki mali.

Unaua kisa mali. Halafu plan yako ni step 1: Choma kitu chenye mcha kali.
Step 2: Check if dead. No? Mfiche ndani.
Strp 3: Ukishtukiwa kimbia.

Now am not sayin mzee wako hakuchomwa na kitu chenye ncha kali ila sidhani kama sababu itakua ni mali. Ama ni ugomvi wa hapa na pale au ni self defence gone too far.

Kwa kumchoma kisha kubaki inamaanisha hakupanga hilo tukio kutokea, hakua hata na getaway plan ndiyo maana mwanae mkamkamata.
 
We dogo au wewe ndiyo mama ake wa kambo unamuuliza maswali ili aache kukutafuta? Mleta uzi tongoza huyu akutumie picha umfananishe na mama yako.

Na mimi nitamkubalia kwa kumuonea huruma kwa kuwa amesha sema yatima tusiwa wanyanyapae jamani.
 
Pole...

Kuna mzee kaachwa hapa mtaani akaamua kuoa barmaid.

Stori kwa ufupi.
Huyu mzee anamke wa makamo tu. Wana mtoto anafanya kazi nje ya nchi. Sasa kila baada ya muda wanaenda kumsalimia mwaka juzi baada ya kutoka kumsalimia mtoto mama kufika nyumbani akaanza visa.

Nimemmiss mwanangu nataka kwenda kumwona tena. Mzee akaruhusu..kumbe nyuma ya pazia anepata mchepuko huko mtoto alipo. Mzee akasubiri mke mwaka ukapita. Akiuliza kwa mtoto anaambiwa mama hayupo kwangu.

Miaka miwili imepita mama amekuja kuonekana viwanja na mzee mwenzake wanakula bata. Mzee akaona isiwe shaka wacha nijitwalie mrembo wa kaunta ya juu.
 
Back
Top Bottom