Wanawake Shinyanga walalamikia watoto wasio na bima kukosa matibabu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
1615462779572.png
BAADHI ya wanawake wenye watoto chini ya miaka mitano wilayani Shinyanga, Mkoani Shinyanga, wasio na bima ya afya ya CHF, wamelalamika kunyimwa matibabu ya watoto wao kwa kukosa kadi hizo.

Wamepaza kilio hicho kwa nyakati tofauti kwenye sherehe wanawake wilayani Shinyanga iliyokuwa na lengo la kujadili changamoto mbalimbali za kiafya pamoja na kuzitafutia ufumbuzi, iliyoandaliwa na Shirika la Thubutu Afrika Initiatives ambao wanatekeleza mradi wa USAID Tulonge Afya wilayani humo.

Mmoja wa wanawake hao, Maria Masanyiwa, kutoka kijiji cha Nduguti wilayani Shinyanga, amesema wasiokuwa na bima ya CHF wamekuwa wakinyimwa matibabu ya watoto wao na kuambiwa mpaka wawe na kadi hizo.

Amesema kutokana na usumbufu huo huamua kutafuta huduma kwenye hospitali binafsi au tiba mbadala za kienyeji.

"Tunaomba Mganga mkuu wa wilayani utusaidie hili suala, sisi akina mama wenye watoto wadogo ambao hatuna bima ya afya CHF, tumekuwa tukinyimwa matibabu ya watoto wetu, manesi wanatuambia ili kupata huduma mpaka tuwe na bima," amesema Masanyiwa.

Chanzo: Ippmedia
 
Back
Top Bottom