Wanawake Saba watamshika mtu mume mmoja wakisema tutakula chakula chetu na kuvaa nguo zetu lakini niitwe kwa jina lako inamaana gani kwenye isaya 4:1

yakobo11

JF-Expert Member
Aug 10, 2016
510
736
Habarini za leo wanajamvi,

Wanawake Saba watamshika mtu mume mmoja wakisema tutakula chakula chetu na kuvaa nguo zetu lakini niitwe kwa jina lako inamaana gani kwenye isaya 4:1.

Hebu mwenye kuelewa jamani, atuelezee nini maana yake
 
Najaribu kuwaza kwa sauti tu!
Ndiyo maana nimependa kushirikisha wadau...
Mimi binafsi nimeoa nina mke mmoja.
 
Mwanamke anayeitwa kwa jina la mumewe ndo anayeheshimiwa, na wanawake wengi hawapendi kuzalishwa tu, bila kuwa na mume ili wasiitwe viruka njia/malaya na waheshimike kwa jamii.

Sasa kutokana na ongezeko la singlemaza na namna watakavyoanza kuzaraulika kutokana na kutokuwa na waume. Ndo wataanza kujichombeza au kujichomeka wenyewe kwa wanaume au waume za watu ilimradi mwanaume huyo aonekane ndo baba watoto wake walau nao wajipatie heshima kwa jamii.
 
Habarini za leo wanajamvi


Wanawake Saba watamshika mtu mume mmoja wakisema tutakula chakula chetu na kuvaa nguo zetu lakini niitwe kwa jina lako inamaana gani kwenye isaya 4:1.

Hebu mwenye kuelewa jamani, atuelezee nini maana yake
“Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.
” — Isaya 4:1 Jifunze kunukuu neno zima kwanza usipote maana yake.

Nirudi kwenye mada uwezi elewa nini kilikuwa kinamaanisha kama hutosoma sura nzima kuanzia Isaya 3 na 4 vyote kwan ndipo kisa kinapo anzia na ndipo hio aibu wanayoomba iondolewe inapoanzia.

Isaya 3:11-26
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹¹ Ole wake mtu mbaya; shari itakuwa kwake, kwa maana atapewa ijara ya mikono yake.
¹² Katika habari za watu wangu, watoto ndio wanaowaonea, na wanawake ndio wanaowatawala. Enyi watu wangu, wakuongozao wakukosesha, waiharibu njia ya mapito yako.
¹³ Bwana asimama ili atete, asimama ili awahukumu watu.
¹⁴ Bwana ataingia katika kuwahukumu wazee wa watu wake na wakuu wao; Ninyi ndinyi mliokula shamba la mizabibu; vitu mlivyowateka maskini vi ndani ya nyumba zenu.
¹⁵ Ni nini maana yake, ninyi kuwaonea watu wangu, na kuseta nyuso za maskini? Asema Bwana, Bwana wa majeshi.
¹⁶ Bwana akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienenda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao;
¹⁷ Basi, kwa hiyo, Bwana atawapiga binti za Sayuni kwa pele za utosini, na Bwana ataifunua aibu yao.
¹⁸ Siku hiyo Bwana atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao;
¹⁹ na pete za masikio, na vikuku, na taji zao;
²⁰ na dusumali, na mafurungu, na vitambi, na vibweta vya marashi, na matalasimu;
²¹ na pete, na azama,
²² na mavazi ya sikukuu, na debwani; na shali, na vifuko;
²³ na vioo vidogo, na kitani nzuri, na vilemba, na utaji.
²⁴ Hata itakuwa ya kuwa badala ya manukato mazuri kutakuwa uvundo, na badala ya mishipi, kamba; na badala ya nywele zilizosukwa vizuri, upaa; na badala ya kisibau, mavazi ya kigunia; na kutiwa alama mwilini kwa moto badala ya uzuri.
²⁵ Watu wako waume wataanguka kwa upanga, na mashujaa wako vitani.
²⁶ Na malango yake yatalia na kuomboleza, naye atakuwa ukiwa, atakaa chini.

Huu ndio mwanzo wa aibu ya hao wanawake, na sura ya 4 inaonesha malipo ya wale waliokuwa wakionewa baada ya kukombolewa toka kwenye uonevu.

Mm ndio uelewa wangu umeishia hapo Ngoja wajuzi zaid waje
 
Habarini za leo wanajamvi


Wanawake Saba watamshika mtu mume mmoja wakisema tutakula chakula chetu na kuvaa nguo zetu lakini niitwe kwa jina lako inamaana gani kwenye isaya 4:1.

Hebu mwenye kuelewa jamani, atuelezee nini maana yake
Mkuu kwa nini usiende kwa mchungaji wako au shemasi, atakufafanulia vizuri zaidi
 
Kitabu cha lsaya ni cha unabii, kiliandikwa kwa mifano. Kwa ufupi ni hivi.
Mwanamke inawakilisha kanisa
Mume inawakilisha Mungu
Chakula inawakilisha neno la Mungu

Hivyo Basi,anaamnisha kwamba,siku hiyo ya mwisho wa Dunia,patachipuka makanisa(wanawake) mengi ambayo yatajitungia mafundisho ya Imani Yao yenyewe yasiyoendana na neno la Mungu(chakula)huku yakijificha kwa jina la Mungu, yaani yaitwe kuwa ni makanisa ya Mungu(mume).
Pia,maana ya saba ni idadi timilifu yaani nyingi Sana kwa kiasi isiyoweza kujulikana idadi.
 
Kitabu cha lsaya ni cha unabii, kiliandikwa kwa mifano. Kwa ufupi ni hivi.
Mwanamke inawakilisha kanisa
Mume inawakilisha Mungu
Chakula inawakilisha neno la Mungu

Hivyo Basi,anaamnisha kwamba,siku hiyo ya mwisho wa Dunia,patachipuka makanisa(wanawake) mengi ambayo Yao wenyewe waliojitungia(chakula)huku yakijificha kwa jina la Mungu(mume).
Pia,maana ya saba ni idadi timilifu yaani nyingi Sana kwa kiasi isiyoweza kujulikana idadi.
Mkuu kumbe huku napo uko vizuri sana!
 
Back
Top Bottom