Wanawake, rushwa na hatima ya uongozi wa kisiasa tanzania

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
Katika taifa letu la Tanzania rushwa imeenea katika maeneo mengi hususani kwenye utoaji huduma kwa wananchi (service delivery). Kila taifa hutumia njia tofauti kukabiliana na rushwa, baadhi ya mataifa yameweka kipaumbele kwa wanawake katika nafasi za maamuzi katika jamii kama njia ya kupunguza rushwa katika kada ya utumishi wa umma. Je hoja hii ina ukeli wowote? Labda tuanze kwa kutazama baadhi ya mifano hai:

i. Nchi ya mexico hutoa maofisa wanawake katika utumishi wa umma kama njia ya kupunguza rushwa.
ii. Nchi ya india hutoa upendeleo wa asilimia 30% ya nafasi za uongozi katika halmashauri za vijiji kupitia sheria yao ya mwaka 1993.
iii. Nchi ya Rwanda nusu ya nafasi za bunge ni wanawake.

Taarifa ya benki ya dunia inaonyesha kwamba rushwa katika halmashauri za vijiji vya India ambazo zinaongozwa na wanawake ipo kwa asilimia 2.7 hadi 3.2 nchini ya kiwango kwa kulinganisha na halmashauri zinazoongozwa na wanaume.

Vilevile tathmini ya benki ya dunia ya mwaka 1999 imebainisha kwa ulinganisho ya kitakwimu (standard deviation) wa ufanisi kwa wanawake katika utumishi wa umma huongezeka kwa asilimia juu ya 9.5 na rushwa hupungua kwa asilimia 10.

Wachunguzi wanabainisha kwamba pale ambapo wanaume huwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa (political leverage) na kiutawala, mapato ya nchi huwekezwa miradi inayogharimu fedha nyingi kama ujenzi wa barabara ambapo rushwa imesambaa, kuliko kuwekeza kwenye huduma za msingi za jamii kama shule na hospitali.

Je kuna uhusino wa moja kwa moja kati ya kupungua kwa rushwa kwa ushiriki wa wanawake katika maamuzi na ubora wa utawala (quality of governance)? Je Tunadhani ni wakati sasa kwa bunge la Tanzania kutengeneza sheria ya ushiriki wa asilimia 30% kwa wanawake katika halmashauri za vijiji?

Nawakilisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom