Wanawake Pingamizi kwa mabadiliko ya uchumi wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake Pingamizi kwa mabadiliko ya uchumi wa Tanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kingwipa1, Aug 18, 2010.

 1. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Napenda nianze kwa kuwaomba samahani wanawake kwa kauli yangu.

  Nimefanya uchunguzi na kugundua kuwa umasikini wa nchi hii umetokana na kung'ng'ania CCM. CCM ni chama ambacho kimeshauzwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wengi wao uraia ni wa mashaka. Hao ndio wanaopanga nani wa kukaa madarakani na nani wa kwenda mahali patakatifu.

  Katika uchunguzi wangu nimegundua kuwa rushwa ya kanga za india ndiyo inayowaponza wanawake wengi na kuwafanya kuichagua sisiemu. Akina mama na akina dada zetu wamekubali kuwa cheap kiasi kinachowafanya kuendelea kuwa duni. Nasikia katika uchaguzi mdogo wa Busanda akina mama walihongwa hadi chupi za ndani.

  Naomba akina mama tubadilike ili tulete mabadiliko ya kweli yatakayoleta maendeleo kwa kila Mtanzania badala ya maendeleo duni ya kutegemea kundi la watu au mtu katika sehemu fulani.
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  unategemea wanawake wakae tu wabadilike!?
   
 3. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  CCM walijipanga miaka mingi kabla ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa. Nakumbuka wakati wa kuendesha kampeni ya kura za maoni za ama tuwe na chama kimoja au vingi vya siasa, viongozi waandamizi waliokuwa madarakani walipita mahali mbali mbali nchini wakitangaza ujio wa vyama vingi kama tishio la amani ya nchi. Walitoa mifano ya nchi kama Burundi, Msumbiji na kwingineko ambako kulikuwa na machafuko na kuhusianisha matukio hayo na uwepo wa vyama vingi.

  Katika utafiti wangu nimebaini kuwa akina mama wengi wako radhi kukichagua chama cha mapinduzi ili kuepusha adha ya vita ambayo inaathiri wa-akina mama na watoto.

  Ndugu wapenzi, napenda tuliangalie suala hili kwa makini na tuangalie namna ya kuelimisha umma wa watanzania juu ya kampeni chafu zilizofanywa na CCM ili tuweze kupata mageuzi ya kweli ya kisiasa na kiuchumi.

  Tukilifumbia macho jambo hili kuna hatari ya kuvuna mabua mwaka huu.
   
 4. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Watabadilishwa na elimu. lakini ukisoma post ya 3 utaelewa ni nini kinaendelea
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu wala huhitaji kuomba samahani kihivyo. Ulichosema kina ukweli - Umaskini uliokithiri humfanya mtu kufikiria leo tu na siyo kesho.Hujasikia hata wale wenye kufanya biashara ya ukahaba katika hali hatarishi wanavyosema ati " bora maisha mafupi matamu kuliko maisha marefu yenye mateso!" Huu ni upotofu lakini tusiwalaumu.Chunguza wanaopokea hizo khanga ni wanawake wepi? Au wanaume wanaodanganywa na shilingi 2000/=au chupa ya bia au hata sahani ya pilau ni wepi? Inasikitisha sana lakini yote haya ni matokeo ya umaskini wa wananchi walio wengi.Kinachohitajika ni elimu ya uraia kuwafanya wote wanawake na wanaume waelewe nguvu na thamani ya kura yao katika kuweza kuwapunguzia umaskini wa kudanganyika na pilau au khanga.
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  wanawake wengi tanzania bado wako chini ya himaya ya wanaume ...............hapa naona elimu ipelekwe kwa mwanamme ili aweze kusimamia uzuri himaya yake ...Au?
   
 7. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  WomanOfSubstance, nashukuru kwa mchango wako.

  Nikiwa katika pitapita zangu mtaani na juhudi binafsi ya kumuuza mgombea ambaye mimi naona anafaa kuleta mabadiliko nimekutana na pingamizi hilo ambalo nimeona ni vema nikaliweka bayana ili tuweze kuongeza nguvu.

  Katika wanaume 10 nimekuwa nikipata kumi ama kwa uchache saba, lakini katika wanawake napata mmoja ama sifuri. hilo limenifanya kuliongea kwenu ili tuweze kuziona changamoto zilizoko mbele yetu.
   
 8. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  ni kweli kabisa, lakini je, inawezekanaje kwa mwanaume kumshawishi mke wake katika mazingira ambayo yeye (mwanamke) anaona anakaribisha vita?
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  Aug 18, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  wanaume wakielimika na wakaweza kuangalia vizuri himaya zao..............basi nafikiri hata namna ya kumwambia mwanamke asipokeee kanga kipindi cha kampeni ataweza
   
 10. D

  Dick JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lakini kuna ka ukweli fulani!
   
 11. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2010
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Ni ukweli mtupu.

  Uongo wa CCM unawafanya kutawala nchi bila ridhaa ya wananchi.
   
 12. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Elimu kwa wanawake bado duni katika nyanja zote, mwanaume akielimishwa haimsaidii sana mwanamke. Cha muhimu ni kila jinsia ielimishwe kwa mapana yake kulinganna na vile wanadanganywa na CCM. Ukienda vijijini utawahurumia mno, jamani si ndio kwetu huko???? Tunaelewa vyema. Pata muda uende kufanya utafiti mdogo vijijini nini kimetokea katika kura za maoni za CCM. Ni vichekesho tupu!!!!!!!!!!!! Maana utashangaa kuwa hadi rushwa ya chumvi ya robo kilo imetolewa kwa akina mama. achilia mbali kaka ambazo ni bei aghali.
   
 13. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haya ndio madhara ya mfumo dume uliokomaa africa....wanawake fursa zao kielimu zimefinyangwa na wamebaki kama wives na kazi zao zimeelemea kuelewa watoto ref mabala and kamazima ( Today's girls tommorow women).
  Mfumo huu una baraka za wanawake wenyewe na wanaume ...umeendekezwa na kukubaliwa kwa kiasi kikubwa matokeo yake ndiyo....KIZAZI CHA MACHANGUDOA, KIZAZI CHA WAPIGA KURA HARAMU....na bado tutegemee kuona mengi sana maana TUNADHANI MWANAMKE KUWA NYUMA AU KUWA NA LOW SOCIAL STATUS NI AFADHALI YA WANAUME
  Inakula kwetu soooote....taratibu tutaamkaa wakati tumeshaloose sana.
  mix with yours
   
 14. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #14
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  kaka umenena, mtaji na jeuri yote ya CCM ni kwa kina mama. Kina mama wakiamua mabadiliko basi yatatokea bila wao NO CHANGES in this country i confirm. Ukweli lazima tuuseme.
   
 15. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #15
  Aug 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  elnino kina mama hawawezi kukaa tu wakaamua mabadiliko ..............lazima kuwe na kitu au mfumo wa kuwabadilisha.

  kutoa blames tu za kuwa wanawake wanahongwa kanga na kutoa kura hakujawa solution bado.

  tujiulize mwanamke atabadilishwa vipi?
   
 16. N

  Nyanzura Member

  #16
  Aug 19, 2010
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Watanzania (wanawake wakiwemo) wanadanganyika kwa sababu hawahusishi, hawaoni uhusiano kati ya ya ugumu wa maisha yao na serikali wanayoiweka madarakani. Watanzania hatujui sukari na Unga kwa mfano vikipanda bei ni kwa sababu serikali imelega katika kusimamia mfumuko wa bei, hawajui wakienda kununua chumvi wanalipa kodi ambayo serikali hiyohiyo haisimamii vizuri, matokeo yake haiwezi kuwafikishia jamii huduma muhimu, maisha bora yanakuwa ndoto.
  Watanzania hawajui kama umasikini, huduma za jamii mbovu mbovu, na hata uchafu wa miji/majiji tu ni kwa sababu ya serikali yao haiwajibiki, ikiwajibika inafanya geresha tu kuwadanganya, wanadhani ni Mungu ndo amependa wawe maskini waishi katika mazingira ya hivyo. Kwa hiyo wao wakipewa hivyo vitu vidogo dogo wanaona wamepata, hawafikirii kama wanaotoa hizo chumvi, sukari, kanga na kofia n.k ni wezi tu wa kodi zao.
  Suala la muhimu tu/wanatakiwa tu/waelimishwe(waelimishaji ni mimi na wewe maana mabadiliko yanaanza na sisi wenyewe) wakipewa wale(wachukue) lakini kura wawape wagombea wanaofaa (Kula ccm KURA CHADEMA vingine ni vi-ccm-B).

  Mkuu Kingwipa1, Usichoke ndugu yangu endelea na moyo huo, unaowahoji jitadi kuwaelezea, hata wasipokubali hapohapo ujumbe unakuwa umefika, baadaye watafikiria na kufanya maamuzi sahihi.

  Tusisahau kupiga kura pia, Vote for Dr. Slaa tumaini na nuru mpya,
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Aug 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Katika kupiga kura, wanawake wengi huvutiwa zaidi na sura ya mgombea kuliko uwezo. Sijui kwa nini wanashindwa kupambanua vitu viwili hivyo – uwezo na sura.

  Nakumbuka siku ile mapema Mei mwaka 2005 baada tu ya kumalizika mkutano mkuu wa CCM Dodoma uliokuwa ukipiga kura kumteua mgombea nilikuwa sehemu fulani ya starehe tukifuatilia zoezi hilo kwenye TV. Alipotangazwa tu Dr Salim kuishika nafasi ya pili (ikiashiria Kikwete ndiyo No1 – mshindi), mlipuko mkubwa wa vigelegele na ndremo zilitoka kwa wanawake waliokuwapo kuliko kwa wanaume.

  Mtaniwia radhi akina mama, lakini nyie ndiyo mko wengi kuliko wanaume na mara nyingi mnaweza ku-swing votes – na hivyo mustakabali wa nchi. Lakini mnapiga kura kutokana na maamuzi ya myoyo yenu, kuliko kutoka kwenye vichwa vyenu.

  Leo hii kama mtu ana uwezo wa kuzuia nusu ya akina mama waliojiandikisha kupiga kura wasiende vituoni October 31 kupiga kura – CCM itakuwa kwenye hatari kubwa ya kuanguka – tena kubwa sana.

  Lkn pamoja na uwezo huo wa ku-determine serikali ziingiazo madarakani, wenyewe wanawake hawana uwezo wa kuongoza kama vile wanaume, pamoja na kelele nyingi za kutaka kuleta uwiano wa 50-50. All this is empty talk na hata wale wanaume wanaokampeni kutaka uwiano huo wanajua udhaifu walio nao dada zetu -- aka the fairer sex.

  Isitoshe hata wanawake wenyewe kwa wenyewe hawajipendi, wanajionea wivu sana, wagombea wao hupigiwa kura za ndiyo kutoka kwa wanaume zaidi kuliko kutoka kwa wanawake wenyewe.

  Mfano mzuri ni uchaguzi wa Marekani mwaka 2008 uliomuingiza Obama. Pamoja na kwamba Blacks kule ni asilimia 30 tu ya Wamarekani wote, idadi kubwa ya Wamarekani hao waliona ni bora kuwa na rais mwanaume – ingawa ni mweusi, kuliko mwanamke mweupe!

  Nilisoma makala moja ktk tovuti wakati ule kwamba ki-jinsia, wnawake wengi weupe walimpigia kura Obama kuliko Hillary Clinton katika kura za maoni za chama (primaries) cha Democrats.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu nimekusoma toka mwanzo lakini kidogo umeleta utata ktk maelezo yako kiasi kwamba inaonyesha unasema Ni kazi ya wanaume kuwabadilisha wanawake as if hawa kina mama hawana akili ktk maamuzi ya busara bila....
  Sijui pengine nimekuelewa vibaya..
   
 19. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #19
  Aug 19, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Itasaidia kwa kiwango, lakini nadhani wengi wao inatokana na kutotaka kujihusisha tu na yale yanayopelekea wao (na sisi sote) kuwa katika hali hiyo. Kuna baadhi ya marafiki zangu, wengine kutoka hapa hapa JF wakike, nikiongea nao kuhusu mambo ya uchaguzi na mapendekezo yao... walaa, hawajali kabisa, as if hiyo ni field ya wanaume pekee. Inasikitisha kwa kweli.
   
 20. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #20
  Aug 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Heshima mbele Mkuu Zak -- umesema yalio sahihi kuhusu wanawake. Marekani yenyewe ilikuwa inawatazama wanawake with suspicion kuhusu uwezo wa maamuzi wanawake kupiga kura na kugombea nafasi kwa kupigiwa kura. Wanawake waliruhusiwa kupiga kura kule Marekani (na kupigiwa kura) mwaka 1920, yaani miaka 144 baada ya kujitangazia uhuru. Nchi ya kwanza duniani kuruhusu wanawake kupiga kura ni Finland -- mwaka 1906.

  Lakini pamoja na 'ruhusa' hii bado wanawake wanashindwa kufanya maamuzi ya busara katika masuala ya kupiga kura -- na kama usemavyo wao husukumwa zaidi na maamuzi ya myoyo yao kuliko akili zao za kichwani! Wao sura mbele kuliko uwezo -- na hapo humwambii kitu kabisa.
   
Loading...