Wanawake ni wazuri usoni ila rohoni ni wakatili sana

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,487
Nionavyo mimi na niwachukuliavyo mimi ni kuwa wanawake ni wazuri usoni wakitabasamu ila rohoni wakatili sana.

Anayepinga atueleze kama kuna mwanamke asiyetabasamu ila wapo wanaume wasiotabasamu.

Ndo hao "machoni kama watu, mioyoni hawana utu!" mnachekeana ila ni rahisi kukutilia hata sumu. Wanawake kwanini mpo hivo? Hata humu wapo kibao! Utawasikia siyo wote ila wote ndivyo walivyo. Ndiyo maana wanaume tukaambiwa tuishi na wanawake kwa akili.

Mwanaume ambaye kampani yake kubwa ni wanawake nae anakuwa kama wao, lazima awe na roho ya kibandidu.

§§§§§§§§§§§§§§§§§§§§§

TUJIFUNZE KUPITIA TUKIO
HILI

Kuna mtoto wa miaka nane
ameuawa na mama yake
kambo maeneo ya Njoro,
mjini Moshi karbu na Open
university.

Mama wa kambo alikuwa
ana miezi takribani minne
kwenye ndoa. Alikuwa
anampiga sana mtoto na
anamnyima chakula.
Siku ya tukio alimpiga mtoto
kichwani kwa kisukumio cha
chapati. Mtoto alimueleza
Baba yake aliporudi jioni
maana alikua ana maumivu
makali sn. Baba alishikwa na
hasira sana akataka kumpiga
mkewe lakini mtoto
akamwambia "Baba wewe
muachie Mungu tu, ila
kaninunulie bag la shule,
kesho shule"

Kesho yake Baba akaenda
kwenye mishemishe zake.
Mke akamtumia meseji
kwamba "rudi nyumbani
kuna dharura" Baba akarudi
akamkuta mkewe. Mke
akamwambia "namuamsha
mwanao lakini haamki"
Kumchunguza mtoto
wakakuta amefariki na
ametokwa na haja ndogo na
kumbwa kitandani.Mama
huyu wa kambo akakimbia
lakini baadae akajipeleka
polisi baada ya wananchi
kumtafuta sana.

Vipimo vya
daktari vimeonyesha kuwa
chanzo cha kifo chake ni
kupigwa na kitu kichwani.
Pia imebainika utumbo wa
mtoto huyo ulikuwa
umejikunja kutokana na
kukosa Chakula kwa wakati,
au kushinda njaa muda
mrefu. Mtoto kazikwa jana
Moshi.

FUNZO:
Wanaume chunguzeni sana
wanawake mnaotaka
kuwaoa. Baadhi ni mbwa
mwitu wenye ngozi za
kondoo. Na nyie wanawake
"Jamani mtoto wa
mwenzako ni wako, kwanini
unamfanyia ukatili kiasi hiki?
Huna utu, huna huruma,
huna ubinadamu?
Ungejisikiaje mwanao
angefanyiwa hivyo na mama
mwingine?

Wanawake mnatajwa kama
watu wenye huruma lakini
kuna wakati mnakuwa
wakatili kuliko wanyama.
Hivi mkoje? Ni mapepo au?
Kama humuogopi mumeo
wala humheshimu huyo
mtoto basi mheshimu
Mungu maana hicho ni
kiumbe cha Mungu. Pole
kwa familia iliyompoteza
mtoto huyu.!

**Wanawake siyo kabisa wala mtu asinishawishi**
 
Wanawake ni wema sana! imagine anapigwa na mumewe anateswa na mumewe japo sio wote,lakini bado anampikia mumewe bila hata kumuwekea sumu! watake radhi akina mama wote na moyoni mwako ujisute kwa kumnenea mabaya mama yako mzazi maana hata yeye ni mwanamke
 
thubutuuuu hata wewe ukitabasamu usoni, unapendeza sana ila rohoni? Duh! Kupika co sababu, mwapika kwakuwa ni wajibu ila ingewezekana kutokupika hamtapika ndo maana kuna wanaume wanapika kwa kutokupenda kupika bali kwa kukatiliwa na mkewe
 
do you know my sex?
 
Mkuu umeweza kumkana mama yako na Dada yako embu jichunguze uelekeo wako
sasa wanaotoa mimba na wanaotupa watoto wachanga si hao hao? Huo siyo ukatili? Awe mama yangu, awe dada yangu, hakuna ukatili wenye ndugu.
 
utakuwa mgeni wa wanawake ama ni wale kina bushoke huenda!

unaposema mwanamke moyoni ni katili unakosea sana,je mama yako ni katili?
kama mama yako ni katili nitakuunga mkono kuwa wanawake ni katili wana roho mbaya.
halafu mimi sio bushoke mkuu nina heshima tu kwa wanawake wote kwa vile namuheshimu mama yangu pamoja na dada zangu bhasi sina budi kuwaheshimu wanawake wote.
 
mama anayekuwa katili kwa mwanae ni wachache sana, ila kwa mumewe, wanaume wengine, na hata kwa wanawake wenzake, ni wote.
 
Bwana weeeee...dont be judgemental. Ukatili,Roho mbaya,wivu,uchafu, upole n.k zote ni tabia na hulka za mtu. Ndo maana wachangiaji hapo juu wamekuuliza kama na mama yako mzazi unamuweka group hilo hilo au..
 
Back
Top Bottom