Wanawake: Ni wakati gani mnadhani ni muafaka kuanza kulipa gharama za mtoko (dates)........?

Ndio maana nikasema analipa kwa sababu ya PR tu maana ela yetu tunachanga Lol.
Ukizingatia tayari niko powerful nsipojishusha kwenye kadamnsasi kwa mila za kiafrika mume anaweza kudharauliwa. Lol.

sawa kabisa ila hebu tuchukulie kuna siku waweza kumwambia mr leo twende nikutoe? na je sehem kama hiyo uko free kumsave?
 
Mtambuzi mwanamume kulipia mitoko kwa mila zetu za kiafrika imejengwa kama lazima..japo binafsi siliafiki sana.
Na kwa kulitambua hili ndio maana hata sisi wanaume huwa kwenye mitoko tunapatumia sana ku'take advantage'
Kikubwa ninachokiona wanawake zetu wa kiafrika wameaminishwa kwamba ili kuona kama mwanaume anakupenda lazima akuhudumie na mitoko ikiwa included..kinyume chake unapotaka kumshirikisha kwenye gharama inaonyesha kama hauko 'stable' na in a long run anaweza hata akakumwaga bro..Lakini all in all mkishakuwa pamoja kwa muda nadhani mnaweza kuanza ku'share' costs..Kwa sababu hata ukijidanganya kwamba hulipii kumbuka zinatoka kwenye 'basket fund'..kwa hiyo nitagharamia sana mitoko but kuna sehemu na mimi ntakuachia kiaina..
 
Last edited by a moderator:
Mmmh... Mtambuzi umenikumbusha mbali kidogo.... Nilikuwa na mpenzi wangu, mara nyingi tukitoka out mie ndie nilikuwa nalipa gharama zooote kisa, nilikuwa nampenda hata sikutaka aingie gharama za aina yeyote... Alivyokuja kunitenda nikapata somo.... Mimi kulipa gharama za outing kwa boyfriend sijui mpenzi, mchumba ni MARUFUKU!! Mpaka hapo nitakapokuwa wake rasmi ( Ndoa) hapo ndio nitagharamia outing..

Unadhani hapo hawezi kukutenda?
 
Huyo alokwambia usipotumbua ela ya mumeo watakula vimada...hana akili na ulifanya vizuri kumtema...Mume achunwi bana. Na hizo mentality kwangu ni upuuzi mtupu.

Kuna mtu alishawahi nambia NK una joint account na mumeo...unawajua wanaume wewe? Nkamwambia siwajuhi wanaume namjua mume wangu. Huyo ni accountant wetu huyo na ni mama mlokole. Hapo nilikuwa ndio naolewa...basi alinambia "mi nipo utanifuata kubadili account' nkamwambia 'ushindwe na ulegee"

Nadhani bado anasubili na huu ni mwaka wa nane na sina mpango wa kubadili account.

i bet to differ with you ma honey hivi kweli, hata kama mmedefine uwe ni wa kiafrika hivi utakuwa mnyimi kisa the man wants to be treated like african king? hii naona haijakaa vyema kwangu.

btw mimi huwa nauamini sana mfuko wangu aisee manake kama hauko poa hata uniambie tutoke nachomoa lol!, kama vipi tupige stail ya kila mtu anunue kinywaji chake but tutashare sigara tu.
 
hahahahahaha lo sitihi neno kimyaaaaaaaaaa hapa it like ulikuwa unasubiri mtu alete uzi huu am tied now
 
Kila mtu hapa atakuja na kituko chake,lakini nawaambieni,kile kinachokufanya ufanye jambo lolote ndo chenye maana kubwa!
 
bora umesema, ya nini kunipeleka kwenye hotel ambazo msosi unatambuliwa kwa mboga??

Eti 'Prawns with mashed potato'

ni bora anipeleke za kiswahili ambapo msosi unatambuliwa kwa nafaka 'wali ng'ombe'

ikishindikana, hata kiosk akaninyweshe soda tu.

Tatizo si Binti wala Hotel, ila kiherehere cha kumpeleka sehemu usoweza ku afford, lol.
 
Hasara tena Mtambuzi? What is the use of money then?
Jamani nitachangia kwenye Ada za watoto, ujenzi na maendeleo mengine; lkn mtoko akuuu!

Sasa mbona hapa ndio gharama zaidi my dear Kaunga
 
Last edited by a moderator:
Huyo alokwambia usipotumbua ela ya mumeo watakula vimada...hana akili na ulifanya vizuri kumtema...Mume achunwi bana. Na hizo mentality kwangu ni upuuzi mtupu.

Kuna mtu alishawahi nambia NK una joint account na mumeo...unawajua wanaume wewe? Nkamwambia siwajuhi wanaume namjua mume wangu. Huyo ni accountant wetu huyo na ni mama mlokole. Hapo nilikuwa ndio naolewa...basi alinambia "mi nipo utanifuata kubadili account' nkamwambia 'ushindwe na ulegee"

Nadhani bado anasubili na huu ni mwaka wa nane na sina mpango wa kubadili account.

hapo dada mkubwa umenena, kuna watu huwa wanaona kwakua wao wamepitia magumu basi na wenzao ni lazima wapite kumbe si lazima bali ni nafasi tu pia kuna misimamao ambayo mtu binafsi anayo nyumbani kwake usilazimishe iwe sawa na ya kwako hapo mimi huwaga wala siangalii.

maisha yangu mimi hata kama nikiatumia kukushuhudia sikwambii fanya kama mimi neva manake bana maisha ya mtu ni yake.
 
Halafu ndio imetokea umempeleka binti Hoteli kama Kilimanjaro Grand Hyatt, pale soda tu shilingi 5,000, bado hujasoma menu, ikitokea kaagiza Lobuster, mai weee..........!

Ha ha ha...kitu lobster...halafu kinachouma zaidi lobster mwenyewe anaguswaguswa tu juu juu,robo tatu nzima mnaacha mezani hapo
 
kiukweli naskia raha akilipa yeye, sana tena sana.

Mie nitacompasate kwenye matumizi mengine home, ila kama ananitoa out acha nideke japo nina mvi.

Mwanamme akitoa ina raha yake bwana, unakuwa unajisifia unaona 'jembe' langu, saa hizo mie 'toto' nimetulia tuli.

Ila kama najua hana, hapo nitarekebisha tokea huko nyumbani, akae nazo pesa basi atalipia yeye, ila awe hana.
Ila tena, kama hana ananialika twende wapi???

i bet to differ with you ma honey hivi kweli, hata kama mmedefine uwe ni wa kiafrika hivi utakuwa mnyimi kisa the man wants to be treated like african king? hii naona haijakaa vyema kwangu.

btw mimi huwa nauamini sana mfuko wangu aisee manake kama hauko poa hata uniambie tutoke nachomoa lol!, kama vipi tupige stail ya kila mtu anunue kinywaji chake but tutashare sigara tu.
 
Mialiko ya hivyo ipo...na ni special places si kule tunakokwenda mara kwa mara. Lakini inategemea na timing maana mume wangu always yuko kamili tukienda mahali kwani anajua yeye ndie mlipaji. Narudia tena kwangu sioni kama namuumiza jamaa kulipa kwa kuwa ela yangu ni yake na yake ni yangu. Hiyo ndo point kubwa...sasa nani kalipa haibadili ukweli kuwa ela yetu imetumika.

sawa kabisa ila hebu tuchukulie kuna siku waweza kumwambia mr leo twende nikutoe? na je sehem kama hiyo uko free kumsave?
 
Kila mtu hapa atakuja na kituko chake,lakini nawaambieni,kile kinachokufanya ufanye jambo lolote ndo chenye maana kubwa!

hapa mdogo wangu umesema kweli kabisa, na hapa watu wengi huwa tuna ova look hili. mfano mim nikisema namtoa hubby yaweza ikawa ni gia ya mimi kuwin jambo kwake mwingine akisema anamtoa sababu ainaweza ikawa ni ziada aliayao nayo, wakati mtu kama aneth akisema ana mtoa hubby ni just kumuonyesha kwamba anampenda na anatamani sana kuona mumewe anapata raha.
 
Umeona eeh...Kitendo cha mwanaume kuingiza mkono mfukoni na kutoa ela kina heshima yake bwana. Waswahili hawakawii kusema yule mwanaume anamtegemea mkewe. Lol.

kiukweli naskia raha akilipa yeye, sana tena sana.

Mie nitacompasate kwenye matumizi mengine home, ila kama ananitoa out acha nideke japo nina mvi.

Mwanamme akitoa ina raha yake bwana, unakuwa unajisifia unaona 'jembe' langu, saa hizo mie 'toto' nimetulia tuli.

Ila kama najua hana, hapo nitarekebisha tokea huko nyumbani, akae nazo pesa basi atalipia yeye, ila awe hana.
Ila tena, kama hana ananialika twende wapi???
 
Hasara tena Mtambuzi? What is the use of money then?
Jamani nitachangia kwenye Ada za watoto, ujenzi na maendeleo mengine; lkn mtoko akuuu!

Ni kweli mtoko aliyeuchokoza ndiye anayepaswa kulipa. Mara nyingi ni mwanaume. Kuna mambo mengi ya kulipia sio mtoko tu. Kwa hiyo mwanamke bado anaweza kujazia mchango wake kwenye mahitaji mengine ya kifamilia. Sometimes wakati wa mtoko, katika hali ya kimapenzi kabisa huenda bibie akaagiza kitu fulani baada ya kumwambia mpenziwe:ungepena kula.... Au kunywa...? Kwa kuwa kajitolea mwenyewe basi inabidi alipie.
 
Jamani mualikaji si ndio analipa bill?
Wanaume wengine hawapendi hasa kwa huu mfumo jike unaoanza.

Ila kiukweli inapendeza mwanaume ndio alipie, naweza compasate kinamna nyingine; kama kununua kitu cha thamani kwa ajili ya nyumbani!

Raha ya mtoko, hubby atoboke! LOL

Aaaha, nimecheka hap kwa red
 
Back
Top Bottom