Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Salamu,
Kwa muda mrefu nimechunguza nikagundua nchi ambazo ni strong sana kwenye mambo ya usalama, wanawake wao hauwezi kukuta wanafanya mambo ya hovyo hovyo. Nchi hizo zimefanya juhudi za makusudi kabisa kuwaendeleza kitaaluma.
Ukiangalia nchi kama za Scandinavia, Canada, Israeli na Ujerumani, wanatumia wanawake wao sana kwenye tafiti, management na usalama. Nadhani ni kutambua maeneo ambayo nature ya mwanamke ina nguvu (they have natural instinct, they are emotional beings and have unique ability to see things on a wider scale).
Bahati mbaya wanawake wetu wameachwa kuwa wa kuchota maji, kupika, kufanya biashara za uchuuzi, kulima na sasa hivi kucheza vigodoro. Juhudi za hapa na pale zinafanywa kuwaendeleza kibiashara mfano kuwasisitiza kujiunga na vikundi nk. Kwa maoni yangu, haya yote siyo maeneo ambayo kama taifa tunaweza kunufaika na uwezo wao ambao ni unique.
Juhudi za makusudi inabidi zichukuliwe kuwaokoa wanawake wetu. Naona juhudi kubwa zinawekwa kuwafanya wafanyabishara, lakini wanawake wangetumika zaidi kwenye nyanja za USHAURI na UTAFITI hasa kwenye maeneo ambayo yanagusa familia moja kwa moja mfano usalama, uzalishaji wa chakula, afya, huko ndiyo tungefaidika nao zaidi.
Kuna story nyingi katika maandiko zinazoelezea jinsi mwanamke anavyoweza kutumika na maadui. Wote mnajua story ya Samson. Kuna story ya wakati wa Musa, yule kahaba aliyewahifadhi wapelelezi wa Israel. Kwenye kitabu cha Waamuzi kuna story ya yule mwanamke alimuangushia jiwe na kumuua Abimeleki, mtu aliyekuwa na nguvu sana, na kwa aibu isijulikane ameuawa na mwanamke akamwambia mlinzi wake amchome na upanga. Kuna story ya wakati wa Daudi, yule mwanamke aliyeokoa mji wake uliokuwa unavamiwa na jeshi la Israeli akiwaambia jeshi la Israeli kuwa yule mtu wanayemtaka atawapatia ifikapo kesho yake (akiwaambia wabaki nje ya mji, kichwa cha huyo mtu watatupiwa juu ya ukuta). Hapo sijaongelea story ya Ester na nyingine nyingi tu.
Jiulize, mtu akitaka kufanya uovu hapa TZ, wanawake wetu wako kwenye hali gani kuwa na uzalendo? Ushauri wangu ni kuwa tuwatumie ipasavyo kwa usalama na ustawi wa taifa letu huku tukizingatia uwezo wao wa kiasili.